Waziri Ummy Mwalimu atoa maagizo mazito kwa Halmashauri 8 zenye hati chafu na zisizoridhisha kwenye ripoti ya CAG

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za kinidhamu kuwachukulia hatua wakuu wa vitengo vya ukaguzi wa ndani wa halmashauri 54

Waziri Ummy amesema wakuu hao hawakukagua hesabu za mwisho kabla ya kuziwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ambapo amesema wakaguzi wa ndani kutokagua Hesabu ni ukikwaji wa kanuni za fedha za mamlaka za serikali za mitaa

Katika hatua nyingine ametaka wataalamu wenye CPA walioko kwenye Halmashuri zenye hati mbaya na hati zenye shaka wabainishwe na wafikishwe katika bodi ya wakaguzi (NBAA) ili wachukuliwe hatua stahiki

Ummy Mwalimu ameyazungumza hayo Aprili 9, 2021 jijini Dodoma alipokuwa anazungumza kuhusu ripoti ya CAG kwa Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI

====

WAZIRI UMMY ATOA MAAGIZO MAZITO KWA HALMASHAURI 8 ZENYE HATI CHAFU NA ZISIZORIDHISHA KWENYE RIPOTI YA CAG​

5a5d69f1-1288-4069-bd9f-1a634bcb7ee7.jpg
726652de-d5f5-41db-a697-ca93353a9ca6.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 9,2021 jijini Dodoma wakati akitoa maelezo kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyotolewa juzi kwa umma ikionesha Halmashauri nane zilipata hati chafu huku 53 zikipata hati zenye mashaka.

Kutokana baadhi ya halmashauri kupata hati chafu na nyingine kupata hati isiyoridhisha katika ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali CAG, Waziri ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo 10 kwa mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo Leo April 9,2021 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amezitaja Halmashauri nane zilizopata hati mbaya kuwa ni Halmashauri za Wilaya za Itigi, Singida, Shinyanga, Momba, Igunga, Sikonge, Urambo na Manispaa ya Tabora.

Waziri Ummy amesema kutokana na Wakurugenzi kuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa taarifa za hesabu za mwisho zinaandaliwa kwa usahihi, ameshauri Mamlaka ya uteuzi wao kuchukua hatua stahiki kadiri ya itakavyoona inafaa.

“Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Nidhamu zihakikishe kuwa hatua stahiki zinachukuliwa kwa Wakuu wa Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani wa Halmashauri 54 ambao hawakukagua taarifa za hesabu za mwisho kabla ya kuziwasilisha kwa CAG,”amesema Waziri Ummy.

Amesema Wakuu wa Mikoa wahakikishe Wanashiriki Mikutano Maalum ya Mabaraza ya Madiwani katika Halmashauri kujadili taarifa za CAG na kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yote ya CAG pamoja na kuratibu kufanyika kwa uhakiki wa majibu ya hoja zote za ukaguzi na Ofisi yake ipate taarifa za utekelezaji na mpango kazi kabla ya Mei 31, mwaka huu.

“Halmashauri zilizopata hati mbaya na hati zenye shaka ziwabainishe, Wataalam wa Fedha wenye CPA (T) ambao walisaini taarifa za hesabu za mwisho kuthibitisha kwamba taarifa hizo ni sahihi na hazina makosa wafikishwe bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) ili wachukuliwe,” amesema.

Pia ameagiza kupitiwa upya mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa lengo la kufanyia kazi dosari zote zilizobainishwa na CAG kuhusu mfumo huo na pia vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya vinavyojengwa sasa, vihusishe uwekaji wa mfumo wa kielektroniki wa GoTHOMIS.

Waziri Ummy pia amebainisha kuwa anakusudia kuandaa mikataba ya ufanisi kwa Wakuu wa Mikoa ili kuongeza uwajibikaji katika maeneo yao ya kazi.

Kuhusu kutorejeshwa kwa mikopo inayotolewa kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Waziri huyo ameagiza Halmashauri kusimamia utekelezaji wa kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo za mwaka 2019 na kuchukua hatua stahiki kwa kikundi kitakachoshindwa kurejesha mkopo.

Credit: Alex Sonna akiwa Dodoma
 
If you literally translate, local government you will end up with machoka, marungu, mapanga na mishale

Kufanya kazi kwenye local government sio tu inahitaji kipaji tu ila ni discpline fulani hivi au science and art

Serikali za mitaa kusikie tu jamani, huku hata kama una PhD yako inaweza kukaliwa na diploma holder na usifanye chochote
 
If you literally translate, local government you will end up with machoka, marungu, mapanga na mishale

Kufanya kazi kwenye local government sio tu inahitaji kipaji tu ila ni discpline fulani hivi au science and art

Serikali za mitaa kusikie tu jamani, hulu hata kama una PhD yako inaweza kukaliwa na diploma holder na usifanye chochote
Chanzo cha Hati chafu sio Wahasibu pekee
Kuna halmashauri fulani (inasemekana) mhasibu aligomea kuidhinisha 'rafu' ya mkurugenzi, ikiwa mkurugenzi ana direct access na The Top Boss, mhasibu 'akakatwa' kichwa.
Hizi halmashauri zisikieni tu kwenye makaratasi.
 
Tunahitaji kuangalia namna nzuri ya kupata viongozi bora, tuna viongozi wengi sana hawakuandaliwa kuwa viongozi bali ni bahati tu na ujanja ujanja tu..

Tunahitaji watu serious kwenye mifumo...sio hizi blah blah, Nyerere aliandaa watu angalau tukawa na descipline kwenye utendaji pamoja na matatizo yote...hizi kazi zinazopatikana kwa connection ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa..
 
Kwamba pesa anatumia muhasibu tu

Wwnasiasa bhana ,upuuzi .mwingii

Ina maana mkurugenzi hajaoneka na wakuu wa idara wengine hawajaonekana wameonekana wahasibu tu

Mwambie ummy kaingia tamisemi na mguuu mbaya atatoka na mguu mbaya
 
Haya ndio madhara ya kumpa mtu cheo ambacho hana taaluma nacho.

Kazi ya mkaguz wa ndan ama mkaguzi wa nje, yaani akishakuwa tu ni mkaguzi, ieleweke kuwa hana authority au mamlaka yoyote juu ya jambo flani, yeye ni mkaguzi tu.

Kama vile unavyoona CAG hawez kumfukuza kaz mfanyakaz yoyote yule wa umma, ama kama vile ambavyo hawezi kulazimisha shirika flan ama taasisi flani ifanye matumiz flani, ndivyo ambavyo mkaguz wa ndani alivyo.

Ukaguzi sio cheo chenye mamlaka ndan ya Ofisi, yaani kusema kwamba mkaguzi ataniwajibisha au kitu flan hakiwezi kwenda pasipo mkaguzi.

Naona Waziri ameongea kihuni tu, wakurugenz ama bodi inachukua hatua ya kumpa mzabun tenda flan pasipo ushindani, mhasibu anaruhusu fungu litoke kwa amri ya bod au mkurugenzi. Sasa mkaguzi hapo anahusika na nini? Akija mkaguz wa nje yeye ataandika tu tenda flan yalifanyika makosa flani.

Labda shirika flani linaenda kununua madawa ya milion 200, wameenda huko hawajapewa risit au wamekiuka utaratibu, sasa mkaguzi atakagua nini? Mkaguzi kama jinsi anavyoitwa ndivyo anavyotenda, yeye ni mkaguzi tu.

Mfano mmenunua computer 100, je atahakiki 100 zipo? Na documents ni halali? Kabla ya kununua ilifanyika quotation sehemu tofauti? Aliyeauthorize hayo malipo ni mhusika n.k

Sasa mkaguz yeye ni wa kuletewa documents tu ofisin, hana mambo mengi kama tunavyowafkiria.

Tatizo ni mifumo iliyopo katika mashirika na sio mkaguzi.

Ngoja niishie apa
 
Tangu mwanzo nilisema viatu vya Jaffo na Katibu mkuu wake HAVIWATOSHI hawa watu wapya wizarani watu mkanizodoa.Ona sasa huu upuuzi??
 
Mbona kama anatafutwa mbuzi wa kafara ? Angeanza kuwawekea kinga wahasibu. Kwanza, mamlaka yake ya nidhamu asiwe mkurugenzi. Pili, mchakato wa kumuondoa mhasibu uwe mgumu sana.Tatu, idara ya fedha iwe independent
Kama mhasibu alisababisha CAG ashindwe kukagua hesabu sababu ya kukosekana nyaraka lazima kichwa kiKate ili wajifunze kutoa ushirikiano kwa auditor
 
Haya ndio madhara ya kumpa mtu cheo ambacho hana taaluma nacho.

Kazi ya mkaguz wa ndan ama mkaguzi wa nje, yaani akishakuwa tu ni mkaguzi, ieleweke kuwa hana authority au mamlaka yoyote juu ya jambo flani, yeye ni mkaguzi tu.

Kama vile unavyoona CAG hawez kumfukuza kaz mfanyakaz yoyote yule wa umma, ama kama vile ambavyo hawezi kulazimisha shirika flan ama taasisi flani ifanye matumiz flani, ndivyo ambavyo mkaguz wa ndani alivyo.

Ukaguzi sio cheo chenye mamlaka ndan ya Ofisi, yaani kusema kwamba mkaguzi ataniwajibisha au kitu flan hakiwezi kwenda pasipo mkaguzi.

Naona Waziri ameongea kihuni tu, wakurugenz ama bodi inachukua hatua ya kumpa mzabun tenda flan pasipo ushindani, mhasibu anaruhusu fungu litoke kwa amri ya bod au mkurugenzi. Sasa mkaguzi hapo anahusika na nini? Akija mkaguz wa nje yeye ataandika tu tenda flan yalifanyika makosa flani.

Labda shirika flani linaenda kununua madawa ya milion 200, wameenda huko hawajapewa risit au wamekiuka utaratibu, sasa mkaguzi atakagua nini? Mkaguzi kama jinsi anavyoitwa ndivyo anavyotenda, yeye ni mkaguzi tu.

Mfano mmenunua computer 100, je atahakiki 100 zipo? Na documents ni halali? Kabla ya kununua ilifanyika quotation sehemu tofauti? Aliyeauthorize hayo malipo ni mhusika n.k

Sasa mkaguz yeye ni wa kuletewa documents tu ofisin, hana mambo mengi kama tunavyowafkiria.

Tatizo ni mifumo iliyopo katika mashirika na sio mkaguzi.

Ngoja niishie apa
Jibu swali Ummy yuko sahihi kwa nini auditor did not review the draft financial statements preceding presentation to CAG.Hiyo ni ippf requirement, mnawatetea auditors kwa nini. Ummy kakamata pènyewe. Reasonable assurance was required by management from the internal auditors. Kula vichwa Ummy
 
Namuunga Mkono kabisa, iweje CAG ndio akagundue Wizi na Ubadhirifu wakati huku wilayani katika halmashauri pia kuna wakaguzi na wanamahesabu wenye CPA / ACCA?

Hawafanyi chochote wanafanya kazi kwa mazoea tu, bora hizo nafasi zichukuliwe na vijana wengine wasio na ajira.
 
Haya ndio madhara ya kumpa mtu cheo ambacho hana taaluma nacho.

Kazi ya mkaguz wa ndan ama mkaguzi wa nje, yaani akishakuwa tu ni mkaguzi, ieleweke kuwa hana authority au mamlaka yoyote juu ya jambo flani, yeye ni mkaguzi tu.

Kama vile unavyoona CAG hawez kumfukuza kaz mfanyakaz yoyote yule wa umma, ama kama vile ambavyo hawezi kulazimisha shirika flan ama taasisi flani ifanye matumiz flani, ndivyo ambavyo mkaguz wa ndani alivyo.

Ukaguzi sio cheo chenye mamlaka ndan ya Ofisi, yaani kusema kwamba mkaguzi ataniwajibisha au kitu flan hakiwezi kwenda pasipo mkaguzi.

Naona Waziri ameongea kihuni tu, wakurugenz ama bodi inachukua hatua ya kumpa mzabun tenda flan pasipo ushindani, mhasibu anaruhusu fungu litoke kwa amri ya bod au mkurugenzi. Sasa mkaguzi hapo anahusika na nini? Akija mkaguz wa nje yeye ataandika tu tenda flan yalifanyika makosa flani.

Labda shirika flani linaenda kununua madawa ya milion 200, wameenda huko hawajapewa risit au wamekiuka utaratibu, sasa mkaguzi atakagua nini? Mkaguzi kama jinsi anavyoitwa ndivyo anavyotenda, yeye ni mkaguzi tu.

Mfano mmenunua computer 100, je atahakiki 100 zipo? Na documents ni halali? Kabla ya kununua ilifanyika quotation sehemu tofauti? Aliyeauthorize hayo malipo ni mhusika n.k

Sasa mkaguz yeye ni wa kuletewa documents tu ofisin, hana mambo mengi kama tunavyowafkiria.

Tatizo ni mifumo iliyopo katika mashirika na sio mkaguzi.

Ngoja niishie apa
Kwa mara ya kwanza Ummy anaibuka kuwa kilaza kwenye uwaziri.
Kaona wasio na nguvu kisiasa ni wahasibu kwahiyo anataka kuwaonea, hajaona DED wala wakuu wa Idara?
Siasa za kiafrika hovyo sana, mtu anajua ukweli lakini hataki kuufata
 
Namuunga Mkono kabisa, iweje CAG ndio akagundue Wizi na Ubadhirifu wakati huku wilayani katika halmashauri pia kuna wakaguzi na wanamahesabu wenye CPA / ACCA?

Hawafanyi chochote wanafanya kazi kwa mazoea tu, bora hizo nafasi zichukuliwe na vijana wengine wasio na ajira.
Seniors wengi kwenye ofisi za serikali wanafanya kazi kwa mazoea sana na kwa kujuana....
 
Back
Top Bottom