Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Bella Bird ambaye aliongozana na mtaalam kutoka ofisi ya Benki ya Dunia hapa nchini Ndg. Inaam Al Huq na Mariam Ally.
Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara Dkt. Leonard Subi, masuala mbalimbali yameongelewa ikiwemo Mradi unaoendelea kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia uitwao "Uimarishaji wa Afya ya Msingi na hususani katika kuzuia vifo vya mama na mtoto".
Vile vile, wameongelea miradi mipya miwili yenye lengo la kuboresha na kuimarisha Huduma za Lishe wenye lengo la kupunguza udumavu pamoja na mradi wa kupunguza vifo vya akina Mama Wajawazito nchini.
Miradi hiyo itatekelezwa kwa namna mbalimbali ikiwemo kuhakikisha Watoto wote wanaotakiwa kusoma wapelekwe shuleni na kuwepo na programu za kuwawezesha wanapata vyakula wakiwa shuleni.
Pia, katika mradi wa kuokoa vifo vya Mama na Mtoto, utalenga kwenye uimarishaji wa Miundombinu wa Vituo vya Afya pamoja na upatikananaji wa Huduma Bora kwenye Vituo vyote.
Ummy akutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia
Muungwana Blog 3 · 10 hours ago

Kuna mradi Wa KFW ulikuwa unasaidia sana kupunguza vifo vya kina mama na watoto katika mikoa ya Mbeya, tanga Kama nakumbuaka vizuri Mtwara na songea. Kwanzia januari mwaka huu mradi huu umesimamishwa kwa wajawazito wapya. Mradi huu ulisimamiwa kwa weledi mKubwa na bima ya NHIF. Kwa njia moja au nyengine mradi huu uliisaidia hata serikali yenyewe.
Kwa nini mradi huu umesimamishwa jamani. Kama hakukuwepo nia mbaya basi ni vyema mradi huu ukaendelea