Waziri Ummy akutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dania. Swali ni kwani mradi Wa Kfw umeachwa ikiwa ulikiwa unasaidia wanyonge.??

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,637
1,863

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Bella Bird ambaye aliongozana na mtaalam kutoka ofisi ya Benki ya Dunia hapa nchini Ndg. Inaam Al Huq na Mariam Ally.

Katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara Dkt. Leonard Subi, masuala mbalimbali yameongelewa ikiwemo Mradi unaoendelea kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia uitwao "Uimarishaji wa Afya ya Msingi na hususani katika kuzuia vifo vya mama na mtoto".

Vile vile, wameongelea miradi mipya miwili yenye lengo la kuboresha na kuimarisha Huduma za Lishe wenye lengo la kupunguza udumavu pamoja na mradi wa kupunguza vifo vya akina Mama Wajawazito nchini.

Miradi hiyo itatekelezwa kwa namna mbalimbali ikiwemo kuhakikisha Watoto wote wanaotakiwa kusoma wapelekwe shuleni na kuwepo na programu za kuwawezesha wanapata vyakula wakiwa shuleni.

Pia, katika mradi wa kuokoa vifo vya Mama na Mtoto, utalenga kwenye uimarishaji wa Miundombinu wa Vituo vya Afya pamoja na upatikananaji wa Huduma Bora kwenye Vituo vyote.
Ummy akutana na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia
Muungwana Blog 3 · 10 hours ago

Kuna mradi Wa KFW ulikuwa unasaidia sana kupunguza vifo vya kina mama na watoto katika mikoa ya Mbeya, tanga Kama nakumbuaka vizuri Mtwara na songea. Kwanzia januari mwaka huu mradi huu umesimamishwa kwa wajawazito wapya. Mradi huu ulisimamiwa kwa weledi mKubwa na bima ya NHIF. Kwa njia moja au nyengine mradi huu uliisaidia hata serikali yenyewe.

Kwa nini mradi huu umesimamishwa jamani. Kama hakukuwepo nia mbaya basi ni vyema mradi huu ukaendelea
 
Umesahau kuwa hao World Bank wamezuia msaada wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 300 kutokana na Jiwe kutamka kuwa hatasomesha watoto wanaopata mimba??

Hii ndizo athari wanazozipata serikali ya awamu ya 5 ambapo viongozi wa serikali wanaendelea "kujiropokea" tu bila kujali athari zake!
 
sasa hao World bank si waanzishe mradi wa kusomesha hao wanaopata mimba za utotoni? Tunafahamu kuwa mimba za utotoni Zina madhara mengi ikiwemo fistula, maternal deaths, umaskini kwa familia inayolea mjukuu. Je katika hiyo misaada kulikiwepo kitita cha kusadia hao watakaopata Fistula, kusadia kulea Mjukuu,nk?kama kweli wana nia njema ya kutusaidia wasitulazimishe vitu vingine vya hovyo kama kuwashangila watoto wanapopata Mimba za utotoni mara sijui tukubari ushoga. Tuna cultures zetu bana.!!!
 
Hamna namna nyinyi ni masikini tu lazima mkubali matakwa ya MABEBERU na bado issue ya Lissu

In God we Trust
 
KFW NI BANK YA MAENDELEO IKO UJERUMANI NA HAO.NDIO WALIKUWA WANAFADHILI HUO.MRADI KWA MAMA MJAMZITO NA MTOTO NADHANI MKATABA UMEISHA ILA WANAO PATA HUDUMA NI WALIO KUWA TEYAR registered.Wapya kwa sasa hawapat hyo huduma hapo nadhani labda anaomba niaje ili kuendeleza
 
Ni kweli sisi ni maskini maana ukiona wasomomi Kama Mdee,Lissu Fatuma wanawasuppoti mashoga unafikiri ni mchezo? Umaskini hata kiroho na kichwani upooo
 
Miradi hiyo itatekelezwa kwa namna mbalimbali ikiwemo kuhakikisha Watoto wote wanaotakiwa kusoma wapelekwe shuleni na kuwepo na programu za kuwawezesha wanapata vyakula wakiwa shuleni.
So... watoto wote hata wale waliopata mimba eeeh??? mbele ya beberu goti la mnyonge litapigwa :)
 
Ni kweli sisi ni maskini maana ukiona wasomomi Kama Mdee,Lissu Fatuma wanawasuppoti mashoga unafikiri ni mchezo? Umaskini hata kiroho na kichwani upooo

Hapo Ummu mwalimu anaongea na hao jamaa kukubali ushoga.
 
KFW NI BANK YA MAENDELEO IKO UJERUMANI NA HAO.NDIO WALIKUWA WANAFADHILI HUO.MRADI KWA MAMA MJAMZITO NA MTOTO NADHANI MKATABA UMEISHA ILA WANAO PATA HUDUMA NI WALIO KUWA TEYAR registered.Wapya kwa sasa hawapat hyo huduma hapo nadhani labda anaomba niaje ili kuendeleza
kama atakuwa anaomba mradi uendelee basi abarikiwe
 
sasa hao World bank si waanzishe mradi wa kusomesha hao wanaopata mimba za utotoni? Tunafahamu kuwa mimba za utotoni Zina madhara mengi ikiwemo fistula, maternal deaths, umaskini kwa familia inayolea mjukuu. Je katika hiyo misaada kulikiwepo kitita cha kusadia hao watakaopata Fistula, kusadia kulea Mjukuu,nk?kama kweli wana nia njema ya kutusaidia wasitulazimishe vitu vingine vya hovyo kama kuwashangila watoto wanapopata Mimba za utotoni mara sijui tukubari ushoga. Tuna cultures zetu bana.!!!

Mimba za utotoni hazishangiliwi na nafikiri serikali na upinzani wote wanazilaani. Kutokuwapa elimu watoto wetu waliopata haya maafa hakupunguzi umaskini wala hakutazuia fistula. Tujifunze kutoka nchi za ulaya, nafikiri kwao tatizo si kubwa na sidhani kama wanawanyima elimu watoto wao waliopata hili tatizo.
 
benki ya Dania ndo benki gani hiyoo naombeni mnisaidie jamani mimi vitu hivi huwa hata sivielewi mleta post na wachangiaji ??

nisaidie mimi mwezenu benki ya daniaa mimi siiifahamu vizuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa hao World bank si waanzishe mradi wa kusomesha hao wanaopata mimba za utotoni? Tunafahamu kuwa mimba za utotoni Zina madhara mengi ikiwemo fistula, maternal deaths, umaskini kwa familia inayolea mjukuu. Je katika hiyo misaada kulikiwepo kitita cha kusadia hao watakaopata Fistula, kusadia kulea Mjukuu,nk?kama kweli wana nia njema ya kutusaidia wasitulazimishe vitu vingine vya hovyo kama kuwashangila watoto wanapopata Mimba za utotoni mara sijui tukubari ushoga. Tuna cultures zetu bana.!!!
Culture za kutowasomesha wasichana mnaowabaka na kisha wakapata mimba? Kama akishapata mimba, asiposomeshwa ndiyo mimba itapotea ili msilee wajukuu?
 
Mbakaji namba moja atakuwA wewe!unaposema mnaowabaki unamanishA nini?
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom