Ulimsikiliza jana??
Alieleza mengi mazuri, ila komenti ya peoples power inavuruga hata mie sikumwelewa.
Akiwa kama mwalimu inawezekana alikuwa anawafundisha watu juu ya nguvu ya umma kama walimu wengine wanavyofanya mashuleni na vyuoni.
CHADEMA wanasema:
".....CHADEMA inaamini katika falsafa na itikadi ya nguvu na mamlaka ya umma. Sasa tumeamua kuweka bayana falsafa yetu na itikadi yetu. CHADEMA tunaendelea kuwa na falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma. Huu ni msimamo wetu wa asili: Kwamba falsafa ya CHADEMA ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni na kuendeleza mawazo, raslimali, uchumi na siasa za nchi.
Aidha, falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa kwa dola ya nchi na kuwa umma ndio wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatma ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa, kutakrimiwa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni....
...hivyo basi, falsafa ya "nguvu na mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vinavyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na haki. Hii ni falsafa tuliyokuwa nayo ambayo tunaiendeleza." Chanzo:
Marekebisho ya Katiba ya CHADEMA
Mafundisho ya CHADEMA kuhusiana na tasinifu ya nguvu ya umma hayana tofauti yoyote na mafundisho yanayotolewa na walimu wa sekondari na wakufunzi wa vyuo wanapokuwa wanafundisha madarasani. Kwa mfano, tasinifu ya nguvu ya umma imo katika kitabu kiitwacho "Mwongozo wa Somo la Uraia Kwa Ajili ya Walimu wa Sekondari na Wakufunzi wa Vyuo" (2002) kilichoandikwa na Dk. Naomi B. Katunzi.
Katika kitabu hiki, tasinifu ya nguvu ya umma imejadiliwa katika somo la 11 na 12 kuanzia ukurasa wa 45 hadi 51. Kwa namna fulani basi, Taasisi ya Elimu Tanzania, Walimu wa Sekondari na Wakufunzi wa Vyuo wanaofundisha somo la uraia, wanafanya kazi ya kueneza itikadi ya CHADEMA? Kama ni hivyo, inawezekana hii ndiyo sababu iliyoifanya CHADEMA kupata mteremko katika siasa zake za hivi karibuni hasa kwa vijana? Siyo kwamba Muhongo, kama mwalimu, alikuwa anazawazisha mambo tuu hapo juu ya people's power kama wanavyofanya walimu wengine?