NasDaz,
..mimi nadhani Prof a-stick to his job description.
..People Power is just a party slogan/greeting sawa na CCM wanaposalimiana kauli ya kidumu chama cha mapinduzi.
..kama Prof alikuwa na ushauri kwa CDM alitakiwa kwenda kwenye sera zao. Sasa na matatizo yote tuliyonayo ktk sekta za nishati na madini, do we really want our minister to be occupied with advising CDM on their outreach programs??
..Inawezekana ushauri wa Prof.Muhongo kwa CDM ukawa ni mzuri--sina uhakika. Lakini kwa mtizamo wangu sidhani kama Raisi alimteua kufanya kazi ya kuwa mshauri wa CDM. Pia nadhani wa-Tanzania walio wengi--CDM included, wangependelea atumie muda wake, akili zake, na nguvu zake, kuondoa uozo ulioko ktk sekta za madini na nishati.
NB:
..Kuhusu mawaziri kutokuwa wabunge nakubaliana na wewe 100%.
..Dhana hiyo malengo yake ni kuondoa uwezekano wa mawaziri kupendelea majimbo walikotoka, na tabia na mienendo ya mawaziri kuwa wakereketwa wa vyama vyao.
..Lakini pia tujifunze toka kwa wenzetu ambao mawaziri wao hawato bungeni. Labda nitoe mfano wa Mama Hillary Clinton. Huyu mama ni mkereketwa haswaa wa Democratic Party, lakini tangu ateuliwe kuwa Secretary of State huwezi kumsikia akizungumzia mambo ya Republican vs Democrats.
..Sasa nakuomba urudi hapa Tanzania uangalie mawaziri wetu wanavyo-behave. In particular mtupie jicho John Magufuli ambaye ktk kila hotuba yake hawezi kutamka sentensi mbili bila kurusha vijembe kwa CDM, au kutamka maneno "ilani ya CCM ukurasa wa XX mpaka XX."