Unajua kwa nini mawaziri wengi wa JK ni vituko? Hawateuliwi kwa uwezo wao wa kazi isipokuwa wanajipendekeza vipi kwa RA, wanachangia vipi fenda ktk kampeni za JK, ni maswahiba kiasi gani na wakuu wa Mtandao nk. Unakumbuka lile baraza la mawaziri sitini? Wizara ya Usalama wa Raia v. Mambo ya ndani? Basi inasemekana JK alipofika madarakani alidhani RA na EL watamwachia ajitawale akiwapa nafasi lakini haikuwa hivyo. Kwanza RA akasema hataki uwaziri ila akaleta majina ya watu wake kama kumi hivi, Mzee wa Monduli kama umjuavyo akaleta wake kama 33 hivi, bila kusahau wazee wa siasa kama kina King Gunge wa Ngombare asingeweza kuwatupa. Yeye mwenyewe JK akawa na watu wake. Pia usisahau mtazamo wa CC emu kuhusu uwakilishi kimikoa katika Baraza la Mawaziri. Hivyo kufikia mwisho unaajikuta una watu kama mia hivi? Huwezi kuamini kirahisi lakini hao sitini (60) walikuwa ndo kiwango cha chini zaidi kilichowezekana kwa wakati huo maana bado kuna wapambe wengi ambao bado hawakupata nafasi
Kwa hiyo usishangae kumkuta Mama yangu Simba siku zote kuwa mropokaji. Inawezekana yupo hapo kwa sababu alienda kwa RA kuomba uwaziri na RA akampa kimemo ampelekee JK "Apewe nafasi anayopenda. Ni mtu wetu wa karibu!" Kisha JK akainua simu kuripoti kwa bosi wake RA "Tayari Mkuu"
Hujaipata hiyo? Inasemekana tangu wanamtandao waanze kutafuta madaraka (miaka kama 18 hivi imepita) hakuna siku waliwahi kujadili watatatua vipi tatizo lolote kubwa (umeme, maji, barabara, kilimo duni nk.) hapa nchini. Mazungumzo yao mengi ilikuwa wapi watapata fedha na vipi watamwondoa nani katika mlinganyo nk. Inasemekana hata zile kashfa za Sumayi kuwa fisadi na pesa nyingi (Inawezekana ni kweli. Sipingani na hilo maana CCM sijui utamwamini nani wote hayohayo) ziliwekwa wazi ili Mkapa (fisadi mwingine lakini aliyemudu makashkashi) asipate nafasi ya kumwachia urais.