Waziri Simbachawene: Wakatoliki wekezeni Kwenye Kujenga Viwanda na Siyo ma-JET

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Tatizo kubwa la kushindwa kueleweka kwa Injili imekuwa kwenye kutafakari Maandiko hayo Matakatifu.Tatizo imekuwa namna ya NENO la Mungu linavyoweza kukaa katikati ya yetu.Ugumu imekuwa kwa baadhi ya wapokeaji wa Injili kuyaishi matendo,mawazo,Falsafa na hata Itikadi ya Yesu.

Ni kwamba ili Injili iwe na maana kwa Wakiristu na watu wote "wanaovuta na wanaopumua hewa ya Injili" ni lazima Injli itafsiriwe katika Maisha ya kila siku ya kila mmoja wetu.Lazima watu wawe na furaha na uhuru.Wawe na amani.Hayo mambo matatu ndio Yesu Kristu alikuja kuyasimika duniani.Injili nzima inasisitiza juu ya mambo hayo matatu.

Watu wakiwa na chakula cha kutosha watakuwa na furaha.Watu wakiwa na makazi mazuri watakuwa na furaha.Watu wakipata mavazi na kupata huduma bora za kiafya watakuwa na furaha na Amani.Watu wakiwa huru watajifanyia shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa usajihi na kikamilifu.Huu ndio wito Wa Kiiinjili.

Leo,Waziri George Simbachawene,mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa,TAMISEMI,alimwakilisha Raisi John Pombe Magufuli katika Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 100 ya Upadri/Ukasisi tangu Makasisi Wa Kwanza Wazalendo kupewa daraja hilo Takatifu.Maadhimisho yamefanyika huko Dodoma.

Katika salamu zake kwa niaba ya Raisi Magufuli,Simbachawene amewataka Wakatoliki kupitia taasisi zake au vyama vya Kitume kuangalia uwezekano wa kuanzisha viwanda kadri ya mpango wa Serikali ya Magufuli na kwamba Serikali itatoa kila aina ya Ushirikiano unaohitajika!

Kwa tafsiri sahihi,Simbachawene anayataka mashirika ya Kikatoliki,mintarafu vyama vya kitume kama VIWAWA,WAWATA,CPT, TYCS,KARISTMATIC,UWAKA,Jumuia ndogo ndogo za Kikatoliki na kadhalika sasa nazo zishiriki kazi ya kujenga uchumi.

Wito huu nimeupenda sana! Ni wazo la kisasa sana.Ni wazo linatokana na tafakari ya Injili kadri ya mazingira ya Kiafrika.Afrika inahitaji kujijenga kiuchumi.Tanzania inahitaji kujijenga na kujiimarisha kiuchumi.Huwezi kuwahubiria watu wenye njaa na ombaomba wakakuelewa.Neno la Mungu haliwezi kuwagusa na kumea ndani ya mioyo ya watoto na Vijana wenye utapiamlo.Mbegu ya Neno la Mungu linameaje kwenye mioyo wa watu waliogonjeka kwa sababu ya magonjwa ya kushambuliwa na Vimelea vinavyoishi katika Nyumba za tembe na matope? Neno la Mungu lina maana gani katika jamii ya watu wasiokuwa na usalama wa kimakazi?

Kwa hiyo, ninamsifu sana Simbachawene kwa wito huu kwa jumuia za Kikatoliki.Ni kama amewaalika wakatoliki wajitofautishe na wale wanashindana kuwekeza katika Ma-JET na Helikopta.Injili haitasambaa kwenda angani Bali kwa kutawanyika ardhini,waliko binadamu.Ndio kusema,Jets na Helikopta zetu zitapata umaana ikiwa wanadamu watakuwa kwanza na uhakika wa uchumi na hivi uwezo Wa kujipatia huduma za kijamii.

Nami,kwa njia hii ya mjadala,niwaalike Wakatoliki "tutweke hadi vilindini" ndio kule tujikusanye kupitia vyama vya kitume na Jumuia ndogo ndogo tuanzishe viwanda.Jumuia mbili,tatu au nne zinaweza kujiunga pamoja na kuanzisha kiwanda.Wakatoliki sisi ndio tuliopewa wajibu wa kutafsiri na kupeleka NENO la Mungu hadi miisho ya dunia.Basi tutafisiri wajibu huo na tuuishi kwa matendo.Tuanze na viwanda vidogo hasa vyenye kuzalisha bidhaa muhimu na ya lazima kwa mahitaji yetu ya kila siku.Mfano,Chakula.Chakula kitaendelea kuhitajika hadi Yesu anarudi.Na hivi hii ni investment ya kudumu.

Nawasilisha na Karibuni kwa mjadala.
 
Maghu pamoja na kelele zote hamna ata kiwanda alichonga zaidi ya vyerehani ! Simbachawene atuambie alikusudia kusemaje kama si kumsema Gwajima ? Tz ya viwonder na siyo firms.

Mkuu fikra mpya na za kujitegemea ni za aina hiyo ya Simbachawene.Fikra kwamba Serikali ndio wenye wajibu wa kujenga viwanda ni fikra ambazo zinatoka katika watu ambao Injili haijaweza kutibu madonda ya Ukoloni vichwani mwao.

Suala la Ujenzi Wa Viwanda ni la Jumuia ya Watanzania wenyewe.Serikali kazi yake ni kutoa dira na miongozo.Serikali kazi yake ni kujenga na kuimarisha miundombinu ya Viwanda:Umeme,maji,Barabara,mawasiliano na "harmozation" ya mifumo ya kodi. Nje ya hapo kutaka Yesu ashuke atuwekee viwanda.
 
Hii serikali yenye mawaziri haijielewi, kwani makanisani yameandikishwa kama taasisi za kibiashara? viwanda ni purely business contrary na registration ya makanisa. kwa nini mu impose Sera yenu kwa wengine? jengeni viwanda ninyi mlio ahidi.

Ndio maana tunasema watu hawajailewa sawa sawa Injili.Wakatoliki wanaielewa Teolojia ya Ukombozi.Ukombozi wa mwanadamu ni Wa kimwili na kiroho.
 
Hii serikali yenye mawaziri haijielewi, kwani makanisani yameandikishwa kama taasisi za kibiashara? viwanda ni purely business contrary na registration ya makanisa. kwa nini mu impose Sera yenu kwa wengine? jengeni viwanda ninyi mlio ahidi.
Huelewi kabisa maana ya NGO nini? Poor you. Ngo maana yake ni kuwa faida yote inayopatikana iwe kwa shughuli za kibiashara hairuhusiwi kugawiwa Kama dividend bali inatakiwa iendelee kutumika kwenye shughuli za NGO tu walizosajiliwa kufanya. NGO zote zinaruhusiwa kufanya biashara wakitaka
 
Hii serikali yenye mawaziri "wapumbavu " haijielewi, kwani makanisani yameandikishwa kama taasisi za kibiashara? viwanda ni purely business contrary na registration ya makanisa. kwa nini mu impose Sera yenu kwa wengine? jengeni viwanda ninyi mlio ahidi.

vatican pia ni wawekezaji wakubwa hata taasisi ya mama theresa nayo inafanya uwekezaji.

sio kwamba hawatalipa kodi watalipa na faida inayopatikana itatumika kuhubiri injili katika mwili na roho ikiwa ni pamoja na kujenga shule na hospitali.

hebu fikiria mvinyo unaoagizwa kwa ajili ya ibada unafikiri wakiwekeza hapa tunaweza kuajili watu wangapi na fedha kiasi gani tukaokoa? zabibu africa mashariki ipo tanzania tu hivyo wakiwekeza wanaweza kuuza kwa kiasi kikubwa kwa makanisa mengine.
 
Makanisa na taasisi mbalimbali za dini na binafsi zimewekeza kwenye elimu, lakini sasa watoto wanaosoma katika shule hizo mmeweka mkakati wa kuwanyima mikopo; yaani mnawapa adhabu wazazi, je kesho wakianzisha viwanda si mtatafuta namna ya kuwapiga kodi kubwa watakaofanya kazi katika viwanda hivyo! Shame on you govt.
 
Hii serikali yenye mawaziri "wapumbavu " haijielewi, kwani makanisani yameandikishwa kama taasisi za kibiashara? viwanda ni purely business contrary na registration ya makanisa. kwa nini mu impose Sera yenu kwa wengine? jengeni viwanda ninyi mlio ahidi.
Mkuu dini zote zinaruhusiwa kufanya biashara za Aina yoyote watakayo duniani kote hata Dini yako inaruhusiwa cha msingi faida mtakayopata hamu rusiwi mgawane inatakiwa itumike kuendeleza kazi za dini tu. Hivyo ruksa anzisheni hata biashara Ya duka boda boda shule vyuo viwanda daladala supermarket au shirika la ndege au shirika la meli ruksa
 
Back
Top Bottom