na Andrew Chale
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema angependa kuona mwanamke anakuwa Rais katika moja ya nchi za Afrika Mashariki.
Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabunge wanawake wawakilishi wa Jumuiya ya Madola (Commonweath Women Parliamentarians-Africa Region) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Aliwataka wanawake kupigana kwa hali na mali katika nyanja za siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ili kuleta mabadiliko ikiwemo kumpata Rais mwanamke Afrika Mashariki.
Waziri Simba alisema kwa mtazamo wake umefika wakati wa kupata Rais mwanamke katika nchi za Afrika na ingefaa kuanzia na nchi zilizoko katika ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
"Jamani wanawake sasa tumepata fursa nyingi ikiwemo usawa katika vyombo vya maamuzi na uongozi wa juu katika serikali. Hadi sasa tuna maspika wa Bunge la Tanzania, Rwanda na Uganda wanawake," alisema Simba na kuongeza: "Sasa ni zamu ya urais!"
Aliwataka wabunge hao wanaporudi majimboni kwao kuhamasisha wanawake katika maendeleo kwani fursa zilizokua zikimkandamiza mwanamke sasa hazipo tena. Alisema ni suala la kujituma tu ili kujikomboa katika ujinga, utegemezi na uonevu huku akipoongeza serikali kwa kufanikisha kumuinua mwanamke ikiwemo kumpa usawa bungeni na kitendo cha Rais kuchagua wabunge wengi wanawake sambamba na wale waliochaguliwa na wananchi majimboni.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake hao ambaye ni Spika wa Bunge la Uganda, Rebeca Kadaga, aliwataka wawakilishi hao kuhakikisha wanatumia fursa ya mkutano huo kuleta maendeleo katika bara la Afrika. "Tutahakikisha wanawake tunapiga hatua kuliongoza bara la Afrika na kuondoa tofauti zote ikiwemo uonevu kwa wanawake," alisema Kadaga.
Naye mwakilishi mkuu wa kanda wa wabunge hao kwenye jumuiya hiyo, Beatrice Shelukindo, alisema mkutano huo ulioanza Septemba 16, utakuwa chachu kwa wabunge wanawake kwani utaleta changamoto kwenye jumuiya hiyo na matataizo yote yatakayokusanywa watayajadili na kuyafanyia kazi. Mkutano huo unatarajiwa kufungwa leo na mke wa Rais, Salma Kikwete.
Source: Tanzania Daima.
Mtazamo:
Huyu waziri wetu mh! Nashangazwa kwanini bado wanamteua tu kuwa waziri. Tukirejee katika tamko lake nimetokea kuuliza maswali yafuatayo sipati majibu. Je unapendelea tuchague mtu kwa gender yake au yule ambaye ana sifa za kuwa kiongozi wa nchi? Hivyo vyeo akina mama walivyopewa hadi kwenye uspika ni kwa kiwango gani vimeweza kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii?
Je urais siku hizi gender ni kigezo kikuu au ni kampeni tayari zimeanza? Are we familiar with gender discrimination and racial discrimination je hii sio sexism discrimination maana na wanaume nao wakisema wanataka rais mwanaume itakuwaje??? Huyu waziri wetu sijui huwa anafikiriaga matamko au la sijui