Waziri Simba: Tunataka Rais mwanamke

Kwenye kongamano/Mkutano huwa alikuwa anatumua lugha gani ? Maana shule yake ndogo na kugha ya kuunganisha watu kimataifa haijui na ndiyo maana hata bungeni aliepushwa kujieleza .Huko alitumia lugha gani ?

Contact UsBrowse by TopicBrowse by Country
Name Sophia Simba
Surname Simba
First Names Sophia
Alternate Name Sofia Simba
Title
Country of Birth Tanzania
Positions
From To Organisation Position
2008 President's Office Minister of State in the President's Office - Good Governance
2007 SADC National Gender Machineries SADC National Gender Machinery - Tanzania
2006 2008 Ministry of Community Development, Gender & Children Minister of Community Development, Gender & Children
2005 Presidentially Appointed MPs Member
1996 1996 University of Zimbabwe Postgraduate Student - Postgraduate Diploma in Women's Law
1994 1996 Dar es Salaam City Councillor
1993 1996 Chama cha Mapinduzi CCM Councillor
1987 1991 University of Dar es Salaam Undergraduate Student - LLB Law
1983 1997 Legal (from 1992) & Administrative Officer - Metal Engineering Industries Developmnet Organisation (MEIDA)
1982 1983 University of Dar es Salaam Undregraduate Student - Certificant in Law
1974 1979 UWT - NDC Branch Chairman
1971 1978 National Development Corporation NDC Personal Secretary
Date of Birth 27 Jul 1950
Political Affiliation CCM
eMail
Telephone
Address Ministry of Community Development, Gender and Children, P O Box 3448, Dar-es-Salaam
Notes POLITICAL EXPERIENCE
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 1995 Todate
Union of Women Tanzania - UWT Chairman(Upanga West branch)) 1994
Chama Cha Mapinduzi - CCM Councilor 1993 1996
Union of Women Tanzania - UWT Secretary (UWT-NDC branch) 1973
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of the board(NDC Branch-CCM) 1973
[ Retrieved on 5/7/2006 ]

AMESOMA BANA ILA KIHIYO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
na Andrew Chale

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema angependa kuona mwanamke anakuwa Rais katika moja ya nchi za Afrika Mashariki.

Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabunge wanawake wawakilishi wa Jumuiya ya Madola (Commonweath Women Parliamentarians-Africa Region) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Aliwataka wanawake kupigana kwa hali na mali katika nyanja za siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ili kuleta mabadiliko ikiwemo kumpata Rais mwanamke Afrika Mashariki.

Waziri Simba alisema kwa mtazamo wake umefika wakati wa kupata Rais mwanamke katika nchi za Afrika na ingefaa kuanzia na nchi zilizoko katika ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

“Jamani wanawake sasa tumepata fursa nyingi ikiwemo usawa katika vyombo vya maamuzi na uongozi wa juu katika serikali. Hadi sasa tuna maspika wa Bunge la Tanzania, Rwanda na Uganda wanawake,” alisema Simba na kuongeza: “Sasa ni zamu ya urais!”

Aliwataka wabunge hao wanaporudi majimboni kwao kuhamasisha wanawake katika maendeleo kwani fursa zilizokua zikimkandamiza mwanamke sasa hazipo tena. Alisema ni suala la kujituma tu ili kujikomboa katika ujinga, utegemezi na uonevu huku akipoongeza serikali kwa kufanikisha kumuinua mwanamke ikiwemo kumpa usawa bungeni na kitendo cha Rais kuchagua wabunge wengi wanawake sambamba na wale waliochaguliwa na wananchi majimboni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake hao ambaye ni Spika wa Bunge la Uganda, Rebeca Kadaga, aliwataka wawakilishi hao kuhakikisha wanatumia fursa ya mkutano huo kuleta maendeleo katika bara la Afrika. “Tutahakikisha wanawake tunapiga hatua kuliongoza bara la Afrika na kuondoa tofauti zote ikiwemo uonevu kwa wanawake,” alisema Kadaga.

Naye mwakilishi mkuu wa kanda wa wabunge hao kwenye jumuiya hiyo, Beatrice Shelukindo, alisema mkutano huo ulioanza Septemba 16, utakuwa chachu kwa wabunge wanawake kwani utaleta changamoto kwenye jumuiya hiyo na matataizo yote yatakayokusanywa watayajadili na kuyafanyia kazi. Mkutano huo unatarajiwa kufungwa leo na mke wa Rais, Salma Kikwete.

Source: Tanzania Daima.

Mtazamo:

Huyu waziri wetu mh! Nashangazwa kwanini bado wanamteua tu kuwa waziri. Tukirejee katika tamko lake nimetokea kuuliza maswali yafuatayo sipati majibu. Je unapendelea tuchague mtu kwa gender yake au yule ambaye ana sifa za kuwa kiongozi wa nchi? Hivyo vyeo akina mama walivyopewa hadi kwenye uspika ni kwa kiwango gani vimeweza kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii?

Je urais siku hizi gender ni kigezo kikuu au ni kampeni tayari zimeanza? Are we familiar with gender discrimination and racial discrimination je hii sio sexism discrimination maana na wanaume nao wakisema wanataka rais mwanaume itakuwaje??? Huyu waziri wetu sijui huwa anafikiriaga matamko au la sijui
Huyu si ndo anaongozwa na akili za ngono? Anadhani ikulu ni kama guest house.
 
Yani hawa CCM bana.. washaona watanzania wote majuha nini? Tunataka rais na sio sketi au shati pale magogoni

suala la jinsia linakujaje come 2015!? sheeeeeenzy zao
 
Hilo suala la ngono tuanze kwa kumuuliza yule padre ameishaacha kamchezo kake ka kuchukua wake za watu na kutaliki?
 
na Andrew Chale

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema angependa kuona mwanamke anakuwa Rais katika moja ya nchi za Afrika Mashariki.

Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabunge wanawake wawakilishi wa Jumuiya ya Madola (Commonweath Women Parliamentarians-Africa Region) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Aliwataka wanawake kupigana kwa hali na mali katika nyanja za siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ili kuleta mabadiliko ikiwemo kumpata Rais mwanamke Afrika Mashariki.

Waziri Simba alisema kwa mtazamo wake umefika wakati wa kupata Rais mwanamke katika nchi za Afrika na ingefaa kuanzia na nchi zilizoko katika ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

“Jamani wanawake sasa tumepata fursa nyingi ikiwemo usawa katika vyombo vya maamuzi na uongozi wa juu katika serikali. Hadi sasa tuna maspika wa Bunge la Tanzania, Rwanda na Uganda wanawake,” alisema Simba na kuongeza: “Sasa ni zamu ya urais!”

Aliwataka wabunge hao wanaporudi majimboni kwao kuhamasisha wanawake katika maendeleo kwani fursa zilizokua zikimkandamiza mwanamke sasa hazipo tena. Alisema ni suala la kujituma tu ili kujikomboa katika ujinga, utegemezi na uonevu huku akipoongeza serikali kwa kufanikisha kumuinua mwanamke ikiwemo kumpa usawa bungeni na kitendo cha Rais kuchagua wabunge wengi wanawake sambamba na wale waliochaguliwa na wananchi majimboni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake hao ambaye ni Spika wa Bunge la Uganda, Rebeca Kadaga, aliwataka wawakilishi hao kuhakikisha wanatumia fursa ya mkutano huo kuleta maendeleo katika bara la Afrika. “Tutahakikisha wanawake tunapiga hatua kuliongoza bara la Afrika na kuondoa tofauti zote ikiwemo uonevu kwa wanawake,” alisema Kadaga.

Naye mwakilishi mkuu wa kanda wa wabunge hao kwenye jumuiya hiyo, Beatrice Shelukindo, alisema mkutano huo ulioanza Septemba 16, utakuwa chachu kwa wabunge wanawake kwani utaleta changamoto kwenye jumuiya hiyo na matataizo yote yatakayokusanywa watayajadili na kuyafanyia kazi. Mkutano huo unatarajiwa kufungwa leo na mke wa Rais, Salma Kikwete.

Source: Tanzania Daima.

Mtazamo:

Huyu waziri wetu mh! Nashangazwa kwanini bado wanamteua tu kuwa waziri. Tukirejee katika tamko lake nimetokea kuuliza maswali yafuatayo sipati majibu. Je unapendelea tuchague mtu kwa gender yake au yule ambaye ana sifa za kuwa kiongozi wa nchi? Hivyo vyeo akina mama walivyopewa hadi kwenye uspika ni kwa kiwango gani vimeweza kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii?

Je urais siku hizi gender ni kigezo kikuu au ni kampeni tayari zimeanza? Are we familiar with gender discrimination and racial discrimination je hii sio sexism discrimination maana na wanaume nao wakisema wanataka rais mwanaume itakuwaje??? Huyu waziri wetu sijui huwa anafikiriaga matamko au la sijui
Kampeni kwa ASHA ROSE MIGIRO at work kwa maelekezo ya Jk aka Kingwendu.
 
Kwanza ni makosa yasiyosameheka kumtafuta kutoka CCM rais 2015 awe wa jinsia ya kike au kiume. Uzoefu unatuonyesha kwamba CCM yote imeoza bila kujali jinsia.
 
Kuna rais mwanamke nchini Liberia, kwa nini iwe tu Afrika Mashariki? Ni sawa kuwa na rais hata mwenye jinsia mbili lakini aingie kwenye nafasi hiyo kwa uwezo wake na si kwa kupigiwa chapuo kama alivyofanyiwa yeye Sofia Simba kwenye ubunge wa SADC. Kupewa nafasi hiyo bila kufanyiwa interview. Au Anna Makinda kupewa nafasi ya uspika eti kwa sababu ni mwanamke.

Hivyo awe mwanamke, mwanamme or whatever.......lazima aingie kwenye nafasi hiyo kwa uweledi wake na si kwa njia za vichochoroni (shortcuts).
 
naaam mama Sophia kanena alichotumwa!, uzoefu wa Siasa Chafu na za kinazi, Huwa hana ujuzi wa kujenga hoja zaidi ya kutumwa!
naona Asha Ngedere kamtuma mamaa kunena....!

aaaagaah Labda first lady nae anaupenda Urais, ctunamwona akiwa ktk motorcade yake?
mpk unashindwa tofautisha ni ya PM au First Lady!
FL aliweza kupata uzoefu ktk campaign ya 2010. Mama tumesikia nae ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM!

Kama tujuavyo East Africa Viongozi wameanza kulewa madaraka na kuzibeba families zao, mfano Uganda, mama m7 kuwa Minister.

Nakumbuka raia mwema waliongelea mkakati wa ndani wa kumuwezesha mwanamama mmoja kukamata urais baada ya mheshimiwa aliyepo sasa kumaliza muda. Hii ilikuwa ni baada ya ile fumua fumua ya kamati kuu kama sikosei. Nadhani ndo haya tunaanza kuyasikia kidogo kidogo. Kuna mtu ameuliza hapo juu kwamba kwa nini Senkoro hakupata support kama suala ni rais mwanamke tu? Ndiyo maana huwa nalipenda raia mwema!!

Nafikiri wanatumia "mwanamke" kama ajenda kuu lakini hawaamaanishi mwanamke yeyote agombee; ukiingia ndani zaidi utaelewa wanataka mwanamke lakini awe na ties na mafisadi au mtu fulani. Kuna wanawake wengi tu wa CCM wameshindwa majimboni si kwasababu ya upinzani wa nje; lakini upinzani wa wanawake wenzao ndani ya chama. Sophia Simba analielewa hili vizuri. CCM wakiteua mgombea mwanamke I guarantee atashindwa vibaya. Sio kwasababu ya uwezo wake, bali kwasababu wanawake wengi viongozi walio CCM hawakuingia kwa nguvu zao wenyewe so, wengi hawajui kufanya kampeni bila majungu (professionalism ni zero). Misuguano within itakuwa mikubwa kuliko kawaida kila mtu akitaka kuuza sura and the like. Halafu kuna kile kamtindo ka tukose wote "kama hutanichagua sehemu fulani sikupi kura" Hili nililiona sana kwenye mpambano wa ubunge Moshi mjini "Betty Minde VS Meghji". Kampeni zao za primaries walichafuana sana lakini finally Betty Minde alipitishwa na chama. However, Meghji side waliumia kiasi kwamba some of the members walikuwa tayari kumkosesha Betty kura zao. Kulikuwa na kampeni chafu (udini etc) kiasi ambacho sidhani kama mpaka leo pande hizo mbili zimeweza ku-repair relationship. Tukumbuke pia mpambano wa "Sophia Simba na Janet". Sasa hili lenyewe litamuogopesha mwananchi wakawaida mwenye nia yaku-support mwanamama mwenye uwezo. Kama chaguzi ndogo ni hivi uraisi si watu watauana. Kuna kazi nyingine ambayo ni ngumu zaidi ni ku-convince kina baba kwamba: a woman can stand alone particularly in CCM and make big decisions bila kuwa influenced na mwanaume (hasa ikizingatiwa vyeo vinatolewa kwa mtindo fulani e.g. viti maalumu). I am one of those people who advocates gender rights, lakini lazima tuwe realistic ili tuweze kufikia malengo. Tena kama front faces zikiwa hizo zakina Sophia Simba I doubt!!! Mgombea anaweza kuwa ni mtu mahiri lakini wanaomzunguka wakiwa "shade" wanapunguza positives za mgombea. Wanawake makini hawatataka kuzungukwa na watu kama Sophia Simba (sijui labda Senkoro was one of them). Ukiwa mtu wa misimamo kunaongeza ugumu wakuweza kupita kutokana na wivu, majungu, hence kutokuwepo na "mtandao wakuaminika" kama ilivyo mazoea kwa CCM.
 
huyu anaota ndoto za mchana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yeye sio mtu wa kusema hayo wapo akina mama tunaowaamini na vichwa sio huyu mama hata kidog kama akina Getrude Mongela, Asha Migiro, Anna Tibaijuka, Ananilea Nkya na Ussu Mallya

Mkuu, Getrude Mongella ameshindwa uspika, amekataliwa na wananchi wake kwenye ubunge; nafikiri history itself inam-disqualify kwenye any other higher post.
 
Rais anachaguliwa na wananchi

Wanawake wanaruhusiwa kuingia kwenye mchakato kisheria

Sasa mama washauri waanza kujitembeza tuwafahamu

wananchi waamue ok..
 
Akiwa Rais mwanamke tofauti itakuwa ni nini? Hata huyu aliyepo sasa, si tuliambiwa ana mvuto wa kike, tabasamu na haiba nzuri?
 
Nilikuwa sitaki kusema neno kwenye hii topic lakini kwa post yako, imenibidi niseme neno.
Akili yako ilivyo ya kichina unafikiri sofia simba akisema mwanamke awe rais basi inakuwa? Unafikiri katiba inaweza kusema hayo unayofikiri? Omba upangiwe kazi nyingine.....unafikiri cdm na vyama vingine ya siasa vitaweka mwanamke kwa vile ccm imefanya hivyo?
anywayz! Kenge ni kenge tu!!
Unajua kuna wanawake wangapi ambao ni vyuma vya pua katika uongozi ambao sio wanachama wa ccm?
Unafahamu tuna vyuo vingapi na wasomi wanawake wangapi katika vyuo hivyo?
Unajua kuna wataalamu wangapi wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya nchi?

Hivi tukisema leo tumchague mwanamke kuwa rais.CDM mtaleta mtu gani? Teh teh teh ! Hapo ndo utaona kuwa vyama vingine vya msimu.Mnakimbilia kufagilia makada wa CCM ati wanawake tunaowaamini ni Tibaijuka na Migoro sio Sofia Simba.Vyama vingine bwana vichekesho vimejaa makamanda tu.
<br />
<br />
 
Back
Top Bottom