Waziri Simba: Tunataka Rais mwanamke

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
na Andrew Chale

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema angependa kuona mwanamke anakuwa Rais katika moja ya nchi za Afrika Mashariki.

Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabunge wanawake wawakilishi wa Jumuiya ya Madola (Commonweath Women Parliamentarians-Africa Region) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Aliwataka wanawake kupigana kwa hali na mali katika nyanja za siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ili kuleta mabadiliko ikiwemo kumpata Rais mwanamke Afrika Mashariki.

Waziri Simba alisema kwa mtazamo wake umefika wakati wa kupata Rais mwanamke katika nchi za Afrika na ingefaa kuanzia na nchi zilizoko katika ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

"Jamani wanawake sasa tumepata fursa nyingi ikiwemo usawa katika vyombo vya maamuzi na uongozi wa juu katika serikali. Hadi sasa tuna maspika wa Bunge la Tanzania, Rwanda na Uganda wanawake," alisema Simba na kuongeza: "Sasa ni zamu ya urais!"

Aliwataka wabunge hao wanaporudi majimboni kwao kuhamasisha wanawake katika maendeleo kwani fursa zilizokua zikimkandamiza mwanamke sasa hazipo tena. Alisema ni suala la kujituma tu ili kujikomboa katika ujinga, utegemezi na uonevu huku akipoongeza serikali kwa kufanikisha kumuinua mwanamke ikiwemo kumpa usawa bungeni na kitendo cha Rais kuchagua wabunge wengi wanawake sambamba na wale waliochaguliwa na wananchi majimboni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake hao ambaye ni Spika wa Bunge la Uganda, Rebeca Kadaga, aliwataka wawakilishi hao kuhakikisha wanatumia fursa ya mkutano huo kuleta maendeleo katika bara la Afrika. "Tutahakikisha wanawake tunapiga hatua kuliongoza bara la Afrika na kuondoa tofauti zote ikiwemo uonevu kwa wanawake," alisema Kadaga.

Naye mwakilishi mkuu wa kanda wa wabunge hao kwenye jumuiya hiyo, Beatrice Shelukindo, alisema mkutano huo ulioanza Septemba 16, utakuwa chachu kwa wabunge wanawake kwani utaleta changamoto kwenye jumuiya hiyo na matataizo yote yatakayokusanywa watayajadili na kuyafanyia kazi. Mkutano huo unatarajiwa kufungwa leo na mke wa Rais, Salma Kikwete.


Source: Tanzania Daima.

Mtazamo:

Huyu waziri wetu mh! Nashangazwa kwanini bado wanamteua tu kuwa waziri. Tukirejee katika tamko lake nimetokea kuuliza maswali yafuatayo sipati majibu. Je unapendelea tuchague mtu kwa gender yake au yule ambaye ana sifa za kuwa kiongozi wa nchi? Hivyo vyeo akina mama walivyopewa hadi kwenye uspika ni kwa kiwango gani vimeweza kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii?

Je urais siku hizi gender ni kigezo kikuu au ni kampeni tayari zimeanza? Are we familiar with gender discrimination and racial discrimination je hii sio sexism discrimination maana na wanaume nao wakisema wanataka rais mwanaume itakuwaje??? Huyu waziri wetu sijui huwa anafikiriaga matamko au la sijui
 

CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,423
1,903
Ameanza.........tunataka rais mwenye uwezo wa kuwa rais.....sio mabao ya jinsia uspika umetuionyesha mengi
 

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,897
1,287
kilaza wa aina ya kipekee katika historia ya Tanzania.
Mbona Anna Senkoro akiwa PPT Maendeleo aligombea Urais mwaka 2005 na hatukuona mwanamke yoyote wa ccm akimuunga mkono, kama kweli alidhamiria hiko anachosema leo , alipaswa kuonesha mfano.
images
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Kwenye kongamano/Mkutano huwa alikuwa anatumua lugha gani ? Maana shule yake ndogo na kugha ya kuunganisha watu kimataifa haijui na ndiyo maana hata bungeni aliepushwa kujieleza .Huko alitumia lugha gani ?
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Huyu nae katokea wapi....

Mnafiki mkubwa huyu! Giza likiingia anamlamba miguu Lowassa huku mbele ya wanawake wenzie anajifanya kupigania rais mwanamke. Toka lini Lowassa akawa mwanamke. Si ni huyu huyu alisema Lowassa ni mwanaume wa kweli? Au anawachuuza wale wa nchi nyingine?
 
Sep 16, 2011
14
1
huyu anaota ndoto za mchana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yeye sio mtu wa kusema hayo wapo akina mama tunaowaamini na vichwa sio huyu mama hata kidog kama akina Getrude Mongela, Asha Migiro, Anna Tibaijuka, Ananilea Nkya na Ussu Mallya
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
172
Huyu mama anafikiriaga masaburi, chama chake kinafikiria masaburi, na kufikiria kwake kwa masaburi ndio kuliko pelekea akapendekeza tuwe na speaker Mwanamke na wote tunajua huyu mama speaker anachokifanya bungeni....... Anyway, tym will tell.........
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,786
Hivi tukisema leo tumchague mwanamke kuwa rais.CDM mtaleta mtu gani? Teh teh teh ! Hapo ndo utaona kuwa vyama vingine vya msimu.Mnakimbilia kufagilia makada wa CCM ati wanawake tunaowaamini ni Tibaijuka na Migoro sio Sofia Simba.Vyama vingine bwana vichekesho vimejaa makamanda tu.
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,959
10,288
Sofia Simba uwezo kichwani hafifu. Hotuba zake ni kichefuchefu kwa mwenye akili.
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Hivi tukisema leo tumchague mwanamke kuwa rais.CDM mtaleta mtu gani? Teh teh teh ! Hapo ndo utaona kuwa vyama vingine vya msimu.Mnakimbilia kufagilia makada wa CCM ati wanawake tunaowaamini ni Tibaijuka na Migoro sio Sofia Simba.Vyama vingine bwana vichekesho vimejaa makamanda tu.

Hujatukanwa siku nyingi nini?
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
172
Namkumbuka aliwahi kusema kwenye campaign aliwaambia wanawake wenzie - wanaofikiria kwa masaburi kwamba wasiotaka ipigia CCM kura wawanyime unyumba............ JK naye sijui anatumiaga vigezo gani kutoa hz political posts....
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
172
Hivi tukisema leo tumchague mwanamke kuwa rais.CDM mtaleta mtu gani? Teh teh teh ! Hapo ndo utaona kuwa vyama vingine vya msimu.Mnakimbilia kufagilia makada wa CCM ati wanawake tunaowaamini ni Tibaijuka na Migoro sio Sofia Simba.Vyama vingine bwana vichekesho vimejaa makamanda tu.

Hao uliowataja kwa mfano wanamfikia Halima Mdee ktk utekelezaji? Humbleness an meekness isiwe kipimo cha uongozi bora uliotukuka au kupewa madaraka.....
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,292
37,521
Hiyo mbona simple, JK akimaliza muda wake anamuachia Salma Kikwete. Si mnakumbuka ile BABA MAMA WATOTO,akimaliza Salma aanakuja RIZ 1.
 

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,899
Kweli uzoefu ni dawa.Hii ni kampeni ya Asha Rose Migiro. ccm Wanajua hawana hoja yo yote ya kumnadi mtu yo yote toka chama hicho awe na gamba ama asiwe na gamba. Wanajua kuwa wakimpata mwanamke watapata kura za wanawake ambao ni wapiga kura wengi nchini. Hii ni hesabu nzuri. Tatizo ni kwamba imepitwa na wakati, wanawake na watanzania hawadanganyiki tena.Pili, ni nani anayewaletea watanzania maendeleo wakati CCM wameshaanza mikakati ya uchaguzi wa 2015 kuanzia 2011? Ndo maana nasema nchi hii, kazi tunayo chini ya ccm hii ya Magamba.
 

wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
800
270
Nakumbuka raia mwema waliongelea mkakati wa ndani wa kumuwezesha mwanamama mmoja kukamata urais baada ya mheshimiwa aliyepo sasa kumaliza muda. Hii ilikuwa ni baada ya ile fumua fumua ya kamati kuu kama sikosei. Nadhani ndo haya tunaanza kuyasikia kidogo kidogo. Kuna mtu ameuliza hapo juu kwamba kwa nini Senkoro hakupata support kama suala ni rais mwanamke tu? Ndiyo maana huwa nalipenda raia mwema!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom