Mimi nimeshajiamulia kuwa Watanzania tunasumbuliwa na uswahili. Utanashati kwetu ni mwiko, ubabaishaji daima.
Kwenye hili la Kagame cup, dalili za uswahili zilianza kujionesha mapema kabisa pale kombe lilipopokelewa airport. Kwa kawaida, ile ni shughuli rasmi ambayo ingetakiwa iwe na staha. Nchi zingine wangepamba rasmi na kutumia watoto waliovalia nguo safi za mchezo wa mpira kulipokea lile kombe. Maofisa wa TFF wangetakiwa wawepo na suti zao, glovu nyeupe za sufi, kuwepo carpet lekundu, mabaunsa watanashati na coverage nzuri ya TV. Kungekuwa na msafara mpaka mjini, na bendera za TFF, FIFA na Kagame Cup zingepamba barabara yote mpaka litapohifadhiwa kombe.
Badala yake?....Picha kwenye gazeti zilimunoesha jibaba limoja limevaa ndala, kitambi hicho, mkono mmoja kashika sijui takataka gani, na mkono mwingine eti kashika kikomba kama vile ni kopo la kutawazia.
Na ubaya zaidi, Super Sport ilikuwepo kuturekodi tulivyo wababaishaji