Waziri Nape; Msiwaachie Watoto wenu walelewe na mitandao

Aug 29, 2022
69
133
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka Wazazi kutowaacha Watoto wao kutumia zaidi mitandao ambapo si salama inapelekea kuharibu kizazi hiki.

Amezungumza hayo wakati akijibu hoja za Wabunge zilizotolewa katika uchangiaji wa Bajeti ya Wizara hiyo ,ambayo imewasilishwa leo Bungeni Jijini Dodoma.

Aidha amesema katika mwaka huu wa Fedha 2024/2025 watakwenda kufanya mapitio ya sheria ya usalama mtandaoni na kufanya marekebisho katika mambo mawili makubwa,mojawapo ni kuwalinda watoto na mitandao .
 
Back
Top Bottom