Waziri Nape aagiza Jeshi la Polisi kuchunguza ajali zinazosababishwa na magari ya Serikali. Kamanda Mutafungwa asema wataanzia Simiyu na Mtwara!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,940
141,915
Waziri wa Tehama na Habari mh Nape Nnauye ameliagiza jeshi la polisi kuchunguza ajali zinazosababishwa na madereva wa magari ya serikali hususani ajali ikiyouwa waandishi 6 mkoani Simiyu.

Naye mkuu wa kikosi cha Usalama barabaranu kamanda Mutafungwa ameahidi kuanza uchunguzi mara moja akianza na ajali za Simiyu na Mtwara.

Source: ITV habari
 
Barabarani Sasa hivi kumekuwa na vurugu kubwa za magari ya Serikali na mabasi makubwa ya mikoani.

Yaani ukiwa unaendesha gari yako hasa highway ukafika salama unamshukuru Mungu. Barabarani unaweza kuwa mstaarabu na makini Ila mzembe mmoja akakusababishia ajali.

Asilimia kubwa ya Traffic wamekuwa ni chanzo Cha ajali kuendelea kutokea kwani hata dereva akivunja Sheria barabarani anamhonga elfu mbili kisha anaendelea na safari.

Kamanda Mtafungwa angejaribu kutoka na Gari binafsi toka Dar Hadi Dodoma aone uozo uliopo barabarani.
 
Siku moja nilikuwa highway, safari ya mbali. Basi nikawa napelekana na gari moja hivi. Wao walikuwa na mwendo mkali sana. Basi wakawa wananiacha mbali.

Lakini kila nikiendesha, nawakuta mbele wamesimamishwa na polisi, wanaongea. Mara wanaachiwa na kuendelea na safari. Wananipita. Mara nawakuta tena wamesimamishwa na askari wengine pembeni wanaongea, mara hao wameachiwa, wananipita tena.

Hivyo hivyo hadi mwisho wa safari. Jamaa alikuwa nawatupia polisi elfu tano tano, halafu anaruhusiwa kama kawaida!

hata dereva akivunja Sheria barabarani anamhonga elfu mbili kisha anaendelea na safari.
 
Waziri wa Tehama na Habari mh Nape Nnauye ameliagiza jeshi la polisi kuchunguza ajali zinazosababishwa na madereva wa magari ya serikali hususani ajali ikiyouwa waandishi 6 mkoani Simiyu...
Huyu inafaa atumbuliwe tena hajui mpaka wa cheo chake. Sasa yeye amekua saa ngapi waziri wa mambo ya ndani? Ngojeni tu mtashuhudia tambo na kauli zake ndio mtaelewa magu hakukosea kumtema.
 
Kwa nini askari wa barabarani wanayaogopa magari ya serikali? Aisee wanavuruga sana hawa jamaa!
 
Waziri wa Tehama na Habari mh Nape Nnauye ameliagiza jeshi la polisi kuchunguza ajali zinazosababishwa na madereva wa magari ya serikali hususani ajali ikiyouwa waandishi 6 mkoani Simiyu...
Waziri wa TEHAMA?. Ile wizara aliyopewa ndugulile kipindi kile imefutwa!.
 
Mh Nape yule bwa mdogo aliyekutisha mguu wa kuku yupo...sasa tunaanzia wapi mweshimiwa ?

Afu na yule bwa mdogo aliyevamia kituo cha utangazaji usiku wa manane na mabunduki eti kisa shilawadu waligoma kurusha ka clip kaka ka udaku...na yeye yupo..ila siku hizi anaishi kama digidili msituni, huyo na yeye nakukumbusha tu mweshimwa kama itakupendeza
 
Mh Nape yule bwa mdogo aliyekutisha mguu wa kuku yupo...sasa tunaanzia wapi mweshimiwa ?

Afu na yule bwa mdogo aliyevamia kituo cha utangazaji usiku wa manane na mabunduki eti kisa shilawadu waligoma kurusha ka clip kaka ka udaku...na yeye yupo..ila siku hizi anaishi kama digidili msituni...huyo na yeye nakukumbusha tu mweshimwa kama itakupendeza
Na waziri wa Mambo ya ndani yupo,nape aache kuingilia majukumu yasiyomuhusu
 
Rudisheni madereva wa zamani mliowafukuza mtakwisha na hao madereva vyeti.
Udereva ni ujuzi na sio vyeti
 
Huyu inafaa atumbuliwe tena hajui mpaka wa cheo chake. Sasa yeye amekua saa ngapi waziri wa mambo ya ndani? Ngojeni tu mtashuhudia tambo na kauli zake ndio mtaelewa magu hakukosea kumtema.


Umewaza kama Mimi , hajui mipaka ya kazi yake nime soma sehemu katoa maelekezo marehemu wanaodai waajili wao walipwe ndani ya siku saba

Kama yeye ni Kidume apigane vita nzito za nssf
 
Hivi Ile ajali ya Bus Saba Za Police Mwaka Jana Ndiyo Wamembambikia Dereva Wa HOWO Huku Wao Wakisema Wapo Sahihi
 
Back
Top Bottom