Waziri mwingine wa Kikwete katika kashfa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mwingine wa Kikwete katika kashfa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Nov 6, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  *Inahusu zabuni ya kumpata bosi mpya NHC
  *Alipuuza mapendekezo ya Ernst & Young


  NA MWANDISHI WA RAIA MWEMA

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kapteni (mstaafu), John Chiligati, amejitumbukiza katika kashfa mpya ya kupuuza kazi iliyofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernst & Young iliyolipwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuendesha usaili wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), imeelezwa.

  Kutokana na utata katika kupuuza mapendekezo ya kampuni hiyo iliyojijengea heshima nchini kwa kutoa taarifa kuhusu wizi wa Sh bilioni 133 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Waziri Chiligati ameshindwa kuweka bayana sababu za kuipuuza kampuni hiyo.

  Habari za uhakika ambazo Raia Mwema imezipata zinaonyesha kuwa, mara baada ya kustaafu kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Martin Madekwe, miezi kadhaa iliyopita, Serikali kupitia Wizara anayoongoza Chiligati, ilitangaza kuwa wazi kwa nafasi hiyo sambamba na kukaribisha watu mbalimbali kutuma maombi kuwania nafasi husika.

  Watu kadhaa walijitokeza kuitikia wito huo wa Serikali na kwa wakati huo, Kampuni ya Ernst & Young iliteuliwa katika taratibu rasmi za serikali na kupewa jukumu la kuendesha usaili na kupendekeza majina ambayo mojawapo litateuliwa na Waziri.

  Taratibu za upatikaaji wa Mkurugenzi wa NHC zipo mikononi mwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye kwa sasa ni Chiligati, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi. (CCM)

  Hata hivyo, taarifa hizo zinafafanua kuwa baada ya Ernst & Young kulipwa takriban Sh milioni 32 kwa ajili ya kutimiza jukumu hilo , walikabidhi mapendekezo yao kwa Chiligati.

  Taarifa zinaeleza kuwa Chiligati ‘alikalia' mapendekezo hayo ya Ernst & Young na katika hali ya utata kutafuta kampuni nyingine ya Jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kazi hiyo ambayo tayari ilikwishafanywa na Ernst & Young na kuichotea Sh milioni 12 nyingine kama malipo ya kazi hiyo waliyopewa.

  Lakini utata zaidi unatajwa kuibuka pale Chiligati alipopenyeza jina jingine ambalo halikuwamo katika majina yaliyofanyiwa mchujo wa awali na Kampuni ya Ernst & Young, ikidaiwa kuwa msingi wa hatua hiyo ni kuhakikisha mtu huyo (jina linahifadhiwa) ndiye anayeteuliwa na wengine waliopitishwa katika mchujo kihalali na kwa mujibu wa taratibu wanabwagwa.

  Mtu huyo anayedaiwa kulengwa na Chiligati hivi karibuni amejiuzulu kutoka katika kampuni moja ya kitaifa inayodaiwa kukumbwa na utata katika mwenendo wake wa utunzaji wa hesabu, kampuni ambayo iliitisha mkutano wa wanahisa wake hivi karibuni.

  Raia Mwema ilifanya jitihada za kumpata Waziri Chiligati kama ilivyo kwa jitihada za kupata uongozi wa kampuni ya Ernst & Young kuzungumzia kadhia hiyo ambayo dhahiri inazua utata kwenye misingi ya dhana ya utawala bora na wa sheria.

  Inaelezwa kuwa katika kadhia hiyo, licha ya Ernst & Young kulipwa milioni 32 za kazi iliyopewa, takriban Sh milioni 26 nyingine zilitumika katika shughuli iliyohusiana na usaili huo wa awamu ya kwanza ikiwa ni pamoja na kugharimia matangazo ya zoezi husika.

  Juhudi hizo zilizaa matunda kwa kumpata Waziri Chiligati ambaye kwa wiki ya pili sasa yupo mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki vikao vya Bunge katika mkutano wake wa 17, lakini juhudi za kupata uongozi wa kampuni ya Ernst & Young hazikuzaa matunda baada ya uongozi huo kushindwa kutoa majibu ya maswali yaliyotumwa kwao kwa njia ya barua pepe.

  Baada ya maelezo ya utangulizi kati ya mwandishi wa gazeti hili na Waziri Chiligati, mazungumzo yalikuwa hivi:

  RAIA MWEMA: "Mheshimiwa Waziri, tueleze ni sababu gani zilikushawishi kupuuza mapendekezo ya Ernst & Young kampuni inayoheshimika, na kisha kuteua kampuni nyingine kufanya kazi hiyo iliyokwishafanywa?

  CHILIGATI: "Nani kakueleza mambo hayo?

  RAIA MWEMA: Tumepata taarifa za uhakika kupitia njia zetu za utendaji kazi wa kawaida.

  CHILIGATI: "Sasa nenda kaandike kuwa mchakato wa kumpata mkurugenzi (wa NHC) unaendelea."

  RAIA MWEMA: "Bado swali la msingi linalohusu matumizi ya fedha za wananchi pamoja na mapendekezo ya kampuni ya awali kupuuzwa na kuteuliwa kampuni mpya kwa kazi hiyo hiyo, hujajibu Mheshimiwa Waziri…naomba majibu ili wananchi waelewe kinachoendelea kwenye shirika lao la taifa."

  CHILIGATI: "Nakwambia…sikiliza bwana…watu hawana shida ya kujua hayo yote, wewe nenda kaandike kwamba mchakato unaendelea na hivi karibuni na hasa mwanzoni mwa mwezi Novemba, mkurugenzi mkuu atatangazwa…nitamtangaza mkurugenzi mkuu…sawa?"

  Mazungumzo na Waziri yaliishia hapo, na hasa baada ya Waziri kuingia katika kikao kingine kilichohusu kutolewa kwa muhtasari wa shughuli za Bunge kwa wabunge wote kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma.

  Shirika la Nyumba la Taifa lipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na kwa kawaida, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo licha ya kuteuliwa na Waziri, huwajibika kwa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo.

  Jukumu kubwa la NHC nchini ni kuwezesha upatikanaji wa makazi bora pamoja na majengo ya biashara, huku lengo kuu la msingi la shirika hilo ni kuwa shirika kiongozi katika sekta ya ujenzi wa makazi.
   
 2. s

  shabanimzungu Senior Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The tz jails will be full of the
   
 3. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Lakini si ndio maana ni waziri? Unataka kila ushauri unaotolewa aukubali?

  Maamuzi yote na lawama zote zinaangukia kwake waziri; kama uteuzi waliofanya haukubaliki tunataka tu kwa sababu ni Ernst & Young aukubali.

  Tumlaumu waziri kama amechukua mtu ambaye hafai na kupuuza ushauri lakini kama hakuna mtu aliyechaguliwa naona tunamuonea tu.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  tunakaribia kuchoka kusikia mambo haya
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkulima,

  Hapo hakuna ushauri, ni kazi ya kitaalam iliyofanywa na kampuni na kuikamilisha. Alichotakiwa kufanya ni kuchagua jina moja kati ya matatu yaliyopendekezwa na hiyo kampuni.

  Hoja nyingine ni matumizi mabaya ya fedha. E&Y ilikomba shilingi milioni 32 kwa kazi hiyo, plus shilingi milioni 26 za matangazo na usaili. Ukijumlisha na shilingi milioni 12 ambazo zimelipwa kwa kampuni ambayo inaendelea na mchakato sasa hivi. Jumla ya zote ni shilingi milioni 70. Si ajabu hiyo kampuni mpya ikaja na majina mawili yaliyopendekezwa na E&Y na then wakapachika jina la huyo mteule.

  Kosa la pili la Waziri ni kwamba je kuipata hiyo kampuni ya nchini alifuata utaratibu? Hiyo ni kazi inayotakiwa kufuata taratibu na sheria za manunuzi. Tunarudi kule kule kwenye mambo ya tender za vitambulisho na Richmond. Aliwapataje hiyo kampuni ya nchini? Kuna tender ilitangazwa?

  Haina maana yoyote Kampuni mbili zifanyie kazi same list of applicants. Kilichoongezeka ni hilo jina moja la mteule wa Waziri ambalo lilipachikwa. Hiyo kampuni mpya haijaanza zoezi upya, bali imechukua barua zile zile na ita/inawasaili watu wale wale. Upuuzi mtupu!

  Atakuwa yuko sahihi iwapo zoezi hilo lilifutwa na kuanza upya, lakini lazima aeleze kwanini aliyaweka kapuni matokeo ya E&Y, hawaamini ama yeye ni mtaalam zaidi yao na hivyo aliona kazi iko substandard? If so kwanini walipewa kazi? Na je walioiteua hiyo kampuni ya E&Y walitumia vigezo gani kiasi kwamba E&Y wakashinda tender lakini wakashindwa ku-deliver?

  Inasikitisha sana maana tunaweza kuingia hasara mara mbili, gharama za kumpata huyo mteule na pia akaenda kushindwa ku-deliver kwa kuwa inaonekana hana qualifications na ndiyo maana alikwepa kule kwa E&Y.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Chiligati sio mtalaam ni mwanasiasa.lazima awasikilize E&Y.
  KIBURI HICHO ANAKIPATA WAPI CHA KUSEMA MKURUGENZI ATATANGAZWA TU.
  HUYU CHILIGATI HANA AKILI NA AMEKOSA BUSARA NDIO MAANA HATA MAKUNDI NDANI YA CHAMA KAYAKUZA KWA KAULI ZAKE ZISIZO NA BUSARA.
  AWAJIBIKE.
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  inatia kizunguzungu hii ni nephotism
   
 8. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamani hizi habari za ni kweli particularly MALIPO? Pesa yote for interviews? Jamani madawa hakuna mahospitalini leo unaniambia kuwa milioni hizo zote zimetumika just for interviews??????? CAG uko wapi????? Hasira za watanzania ziko wapi?
   
 9. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ama watanzania tulio wengi ni mazezeta au tumerogwa. Hakuna mantiki usaili kutumika mapesa hayo nasi tunaendelea na maisha kama hakuna kilichotokea. Hivi mpaka litokee jambo gani ndio tuamke na kusema sasa basi? Hivi NHC shirika ambalo hata usimamizi wa nyumba zake unasuasua, utaratibu wa kumpata mkurugenzi mkuu nao unahitaji mihela mingi kiasi hicho? Hivi hawa jamaa nchi wanaipeleka wapi? Hata majibu yao ni ya kijeuri jeuri tu! Inaelekea tumeamua kusalimu amri na kukubali kuwa sasa tunatawaliwa na "ufalme" au "usultani" manake hawataki kuulizwa jambo lolote utadhani hii nchi ni mali yao! Itafika mahali tutalazimika kuwafyeka...Mungu apishie mbali.
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ndio maana anasema vita ya ufisadi ni Comedy kwa kuwa inamchekesha, na ndio maana anamchukia Sitta!!!???
   
 11. m

  msabato masalia Senior Member

  #11
  Nov 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wa-tz bwana.............ifungwe Taifa stars,full kulalamika,ITV,Channel 10 fukuza Maximo,..........wakiibiwa...........Mungu yupo!!!!!!!!Aaaaaaaaaaaaaaaaaagh,nendeni tena kwenye Tv mseme tumeibiwa. Mbona pesa ya Yanga na Simba pesa inapoliwa mnakuwa wakali kwenda hadi mahakamani kupinga????? Hivi kwa nini? Nimekata tamaaa. Home sweet Home???????????
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Regardless of the nitty gritties of the nomination process, Minister Chiligti, judging from the telephone excerpts, has displayed a high degree of highhanded bureaucracy and lack of respect for the public's right to information.He seems to still be living in the days of "Chama chashika hatamu" and cannot cope in a modern society with a free press and an educated population that is literate enough to demand information for the assesment of public officials.
   
 13. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  yeye mwenyewe sura yake ni full comedian.
   
 14. PoliteMsemakweli

  PoliteMsemakweli Member

  #14
  Nov 7, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nami siwezi kuamini!! Yaani usaili wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa shirika kama la National Housing which is not a techinical Shirika linahitaji ushauri wa Ernest & Young na mahela yote hayo? Hii ni kazi ya techinical Ministries kuteua wataalam ambao wangefanya usaili wa wale waliomba kazi....Kweli wajinga ndio waliwao.....Baada ya kazi kufanyika na mahela yetu kuliwa bado tena wanatafutwa wataalam wengine... kwa misingi gani? kwa utaratibu upi? Jamani we have had enough of this..
   
 15. s

  susu Member

  #15
  Nov 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Have never come acrross in with such things in my life,paying 32 mil for interview somebody,how much are they going to pay the hired one?these is absolutely nosense.we are poor country even the welth one doesnt pay that much.These should be investigate by PCB .someone has to explain theses.It is rsponsiblity of minister to appoint the chief excutive of NHC but dont think he has to use that much amount for just interview.the minster should go as well.
   
 16. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,401
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  kanda2,mbavu sina!
   
 17. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kwanini huna mbavu? ujinga huu wa kuwatafuta Enerst and Young akawalipa.halafu analeta kampuni yake ya mtaani na jina la mtu wake analichomeka ni UCOMEDY tosha.yaani sisi tuko serious yeye anafanya maigizo.waandishi wanamfuata hadi Dodoma anajibu Pumba.
  mambo yake ni Comedy SURA yake ni Full COMEDIAN.
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Acha jazba "waandishi" walimpigia simu na si kumfuata Dodoma.

  Back to the mada, waziri sio rubber stamp awe anaidhinisha kila kitu tu, kama hajaji ridhisha anaweza kuachana na huo ushauri wa "kitaalam" vilevile, so tuliza ball kijana bongo tambarare!
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Keil,

  Hao E&Y wanalipwa mahela yote hayo kwa kazi tu ya kumpata mkurugenzi wa NHS?

  Sijui lini Watanzania tutaacha kuwa wajinga na kuanza kuthamini vilivyo vyetu na kutumia vizuri pesa za wananchi kwa mambo ya maana kama elimu na afya.

  Watanzania wengi inaelekea bado hatuyajui matatizo yetu na ndio maana nchi itaendelea kuwa maskini. Ubabaishaji kila sehemu.

  Eti wataalamu? Give me a break, mbona hawakutoa ushauri kuokoa mabank na mashirika yao huku nje?

  Huyo waziri na hao E&Y wote ni walaji tu wa fuko la watu maskini. NHS ya mwalimu ilikuwa more effective kuliko haya mashirika yenye wakurugenzi waliopatikana kwa mamilioni ya pesa.
   
 20. K

  Keil JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Mtanzania,

  Tanzania ni shamba la bibi, kila mtu akipata nafasi anavuna apendavyo. Swala la hizo gharama nilikuwa nime-reserve comments zangu na ndio maana nikasema tutaingia hasara mara 2.

  Kama NHC ingekuwa inatengeneza faida ya mabilioni, ningeweza kuona kwamba it is worthy it, lakini wako choka mbaya. Hela za kujenga nyumba mpya hawana. Hela za kukarabati nyumba alizojenga Nyerere na zile tulizowadhulumu wahindi, hakuna. Leo Wizara inakwenda ku-spend shilingi milioni 70 kwa ajili ya kumpata MD/DG wa NHC!

  Mimi ninafikiri kwamba Idara Kuu ya Utumishi wangeanzisha kitengo ambacho kingekuwa kina deal na kufanya recruitment ya watu kama hao badala ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa kampuni binafsi. Tanesco nao wamefanya hivyo, lakini sijui wametumia fedha kiasi gani. Ni system nzuri inayosaidia kupata mtu mwenye sifa zinazotakiwa, but gharama zake zinakuwa inflated sana.
   
Loading...