Waziri Mwijage: Mimi ni 'propagandist' niliyesomea China. Aagiza tani 20,000 ya sukari bandarini itolewe

Hivi hapa Tanzania kuna mtaalam/Wataalam wa Logistics au ndio wanapuuzwa na waliowakuta Ofisini?
 
Ya kutoka zanzibar ya sh 65000 kwa mfuko unakataza,ya india brazil sh 110000 mfuko unaikubali.Aliyetuloga afufuke
 
Kumbe ni propagandist ndo maana anadai ni mcha Mungu. Wako wacha Mungu na bado wana damu za wanadamu wenzao mikononi mwao
 
Sasa nimeelewa ni kwanini blenda ni kiwanda! Magu sahau tz ya viwanda kwani uliempa wizara ni mzee wa porojo na mtengeneza uongo! Hatifiki hata kidogo kwani hana weledi na biashara! Isitoshe huyo propagandist alifaa kuwa kwenye ofisi ya polepole akisaka wanachama na kukisemea chama na sio wizara nyeti hiyo! Na kwanini mawaziri wa zama hizi ni wale watu weak na wasio na vision?
 
Upungufu sukari mafuta ni tatizo la kutokuwa na dhamira.Serikali ifanye kusudi kutoa ruzuku,utafiti,mifumo umwagikiaji,mashamba kwa wakulima.Ni msimu mmoja wa kilimo tutauza nje sukari na mafuta.
 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema nchi ina sukari ya kutosha na kilichojitokeza ni propaganda ya watu wasioitakia mema.

Akihitimisha hoja ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 leo Mei 11, 2018 bungeni, Mwijage amesema tayari ameagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula la Dawa Tanzania (TFDA) kuiondoa sukari yote iliyopo bandarini.

Amesema yeye ni mcha Mungu na asingependa kuona Waislamu wanaotarajia kuingia katika mfungo wa Ramadhani wanapata shida ya kupata sukari.

Waziri Mwijage amesema hakuna tatizo la sukari kwani kuna akiba ya sukari tani 43,000 iliyopo katika stoo.

“Lakini Tanzania tunatumia tani 40,000 kwa mwezi,” amesema.
Amesema amewaagiza mameneja wa TBS na TFDA kuhakikisha tani 20,000 ya sukari iliyopo bandarini inaondolewa.

“Viwanda vya sukari vyote bado kama wiki tatu vinaanza kuzalisha. Suala la sukari lilikuwa ni propaganga na mimi ni ‘propagandist’ niliyesomea China,” amesema.

Kuhusu mazingira ya uwekezaji, Mwijage amesema amekuwa akipigania kuyafanya kuwa rafiki na kuwaomba wabunge wanapobaini kuwapo kwa changamoto zozote waziwasilishe kwake na hatua zitachukuliwa.

Pia, amesema amepokea maoni na ushauri wote uliotolewa na wabunge na kuahidi kuufanyia kazi.
Kweli huyu ni propogandist aliyetokea China!
 
Back
Top Bottom