Waziri Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa lafikia Tsh Trilion 69.44

Bikirajohola

JF-Expert Member
Jun 11, 2022
356
632
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.4.

Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh47.07 trilioni na deni la ndani lilikuwa Sh22.37 trilioni

Dk Nchemba amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema ongezeko la deni la Serikali lilitokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Aidha, ongezeko la deni lilitokana na kutolewa kwa hatifungani maalumu yenye thamani ya Sh2.18 trilioni kwa ajili ya deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) lililotokana na michango ya watumishi wa kabla ya mwaka 1999.

Amesema taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa.
 
Huo uhimilivu ambao Huwa unasemwa na wataalam wetu Huwa siuelewi kabisa,

Makusanyo kwa mwezi 1.3t, kuhudumia deni la taifa ni zaidi ya 700b, MISHAHARA ni 600b na zaidi, Bado fedha ya maendeleo, na matumizi mengineyo. Hivi hatuoni kwamba Kuna kipindi makusanyo yote yataenda kuhudumia deni la taifa na kutuacha bila hata ya vitumbua na ya kula kwa urefu wa kamba hizi tulizofungwa...........!
 
Huo uhimilivu ambao Huwa unasemwa na wataalam wetu Huwa siuelewi kabisa,

Makusanyo kwa mwezi 1.3t, kuhudumiwa deni la taifa ni zaidi ya 700b, MISHAHARA ni 600b na zaidi, Bado fedha ya maendeleo, na matumizi mengineyo. Hivi hatuoni kwamba Kuna kipindi makusanyo yote yatemaenda kuhudumia deni la taifa na kutuacha bila hata ya vitumbua na ya kula kwa urefu wa kamba hizi tulizofungwa...........!
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.4.

Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh47.07 trilioni na deni la ndani lilikuwa Sh22.37 trilioni

Dk Nchemba amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema ongezeko la deni la Serikali lilitokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Aidha, ongezeko la deni lilitokana na kutolewa kwa hatifungani maalumu yenye thamani ya Sh2.18 trilioni kwa ajili ya deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) lililotokana na michango ya watumishi wa kabla ya mwaka 1999.

Amesema taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa.
Mmmh....Duuh. Lakini sasa tunaelewa zinaenda wapi, mwanzoni zilikuwa zinanulia chai, sambusa, chapati na samani za maofisi ya serikali. Ndiyo maana deni lilipaa sana kipindi hicho na utegemezi wa bajeti kutoka kwa wahisani imekuwa kubwa.
 
Kopeni ila pelekeni pesa zaidi kwenye miradi yenye tija Ili kupata pesa za kulipia deni..

Ni vyema Serikali iwe na malengo maalumu ya Kukopa specifically kwa ajili ya miradi ya kiuchumi tuu na sio huduma za jamii,huko tutumie pesa za ndani unless kuwe na mazingira ya udharura..

Ila Tanzania ni wavivu Sana Kukopa yaani kadeni hako tuu Sasa tutaendeleaje kwa kujichangisha tuu?
 
Mmmh....Duuh. Lakini sasa tunaelewa zinaenda wapi, mwanzoni zilikuwa zinanulia chai, sambusa, chapati na samani za maofisi ya serikali. Ndiyo maana deni lilipaa sana kipindi hicho na utegemezi wa bajeti kutoka kwa wahisani imekuwa kubwa.
Nimependa hiyo idea ya serikali kunfliat bond Ili kupata pesa za kulipia madeni ya mifuko ya jamii vinginevyo ingekolapse na kushindwa kulipa mafao..

Jiwe alitufanya vibaya sana hapa Tanzania.
 
Huo uhimilivu ambao Huwa unasemwa na wataalam wetu Huwa siuelewi kabisa,

Makusanyo kwa mwezi 1.3t, kuhudumiwa deni la taifa ni zaidi ya 700b, MISHAHARA ni 600b na zaidi, Bado fedha ya maendeleo, na matumizi mengineyo. Hivi hatuoni kwamba Kuna kipindi makusanyo yote yatemaenda kuhudumia deni la taifa na kutuacha bila hata ya vitumbua na ya kula kwa urefu wa kamba hizi tulizofungwa...........!
Ndugu Rais Samia sio kilaza kama waliopita,hayo makusanyo ya 1.3 kwa mwezi ni ya Jiwe..

Mama Kwa mwezi ni 1.8Til..
 
Back
Top Bottom