Waziri Mwakyembe kulipeleka Gazeti la Dira Mahakamani

Waziri Mwakyembe kulipeleka Gazeti la Dira Mahakamani

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,008
Reaction score
63,999
June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi.

Waziri Mwakyembe amesema ’Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu ‘

‘Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji ‘ –Waziri Mwakyembe

‘Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kiviti kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kulitia doa jeshi letu. Tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru kinatumika kama daladala.‘ –Waziri Mwakyembe

‘Tutafungua kesi hii mahakama kuu ya Tanzania na bado mimi na mawakili wangu tunaangalia impact na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya habari kama ITV na Star Tv kwa kutangaza taarifa ‘- Waziri Mwakyembe

CldytwTWMAA41MR.jpg
 
Hili Dira mmiliki wake ni General Ulimwengu? naauliza matusi sitaki nimefunga tusiharibiane swaumu, kama hujaguswa kunijibu kwa staha basi nyamaza uwaze yako
Umefunga au umebadilisha ratiba ya chakula maana naona kuna usanii mkubwa sana! Kama umefunga kweli unatafuta nini huku kuleta uzushi mtupu ambao ni dhambi! Magazeti ya Jenerali ni Raia Mwema na Raia Tanzania.
 
Maiishie kukanusha tu. chukueni hatua dhidi ya gazeti hili


MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MADAI YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012, limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Familia ya JK yachafuliwa”.
Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.
Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.
Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake. Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.
Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.
Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.
Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.
Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria.
……..Mwisho…..
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

7 Mei, 2012
 
Umefunga au umebadilisha ratiba ya chakula maana naona kuna usanii mkubwa sana! Kama umefunga kweli unatafuta nini huku kuleta uzushi mtupu ambao ni dhambi! Magazeti ya Jenerali ni Raia Mwema na Raia Tanzania.
Nadhani hoja yake ni kumjua mmiliki wa Gazeti la Dira. Hayo ya kubadili ratiba ya kula hayakuhusu. Kama unadhani ni rahisi kubadili ratiba ya kula, fanya hivyo uone. Usicheze na imani za watu
 
Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe akanusha taarifa za gazeti kwamba yeye ni tapeli, aahidi kuwashtaki mahakamani.

Pamoja na kuzungumzia tuhuma zilizoibuliwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania za Utapeli wa Bil 2 wa Power Pool, ambazo amezikana, vilevile amezungumzia Wananchi kuiba kifaru kwenye Kambi ya Jeshi huko kiluvya.

'huku ni kukosa uzalendo na kulitia doa jeshi, tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru kinatumika kama daladala' amesema Waziri Mwakyembe
View attachment 358604
Mkuu Mwakyembe bora ukae kimya tu au umwambie Nape afungie hilo gazeti , lakini nakuhakikisha ukienda mahakamani utashindwa vibaya sana ! Na utashangaaa !!!!
 
Hiyo Habari ya kuiibiwa Kifaru wamesombwa ofisi nzima na wapo jeshini makao makuu kwa mahojiano zaidi na wapi walikopata hizo taarifa.

Kwa wapo kupigishwa ambushi huko? Pole Yao.!
 
Back
Top Bottom