Waziri Mwakyembe ashushuliwa.

Mimi nilikuwepo eneo la tukio mpaka saa tatu, ni kukosa la kuandika kudai kashushuliwa wakati alikuwa anathibitisha moja ya kero zinazowakabili waendesha daladala. Kwanza Dr. Mwakyembe alikuwa anakagua nauli kama zinatozwa halali, mbona hilo hauongelei?
Sasa naanza kuelewa akili za baadhi ya watu wanaotaka ionekane mazuri yanafanywa upinzani tu, na sio CCM. Na hii ni dalili ya uroho wa madaraka na si nia ya dhati kutatua kero za wananchi
 
Mi naona ni vizur ameenda direct tena kwa kustukiza mana magamba ni hodari sana wa kuandaa mamluki. kama kweli kiongoz ana nia ya dhati ya kutatua tatizo nisahihi kustukiza ili akutane na hali halisi iwe inafurahisha au isiyofurahisha. ukiwataarifu watendaji wa serikali ya magamba wanaandaa mamluki km wale machinga fake wa mwanza.
well done Mwakay
 
Naona sasa katiba mpya itamke wazi vyma vya siasa vipewe usajili kipndi cha uchaguz tu baada ya hapo vifutwe,hz democrasia nyngne znatuongezea umasikin tu.
 
Amefanya vizuri kwenda kujionea hali halisi. Kwa nchi ilipofikia kila mbinu inatakiwa kutumika. Sio kuweka strategy tu na kukaa ofisini, utapewa taarifa feki. Kila linalowezekana kulifanya kwa stahili yoyote lifanyike hali mradi lina maslahi kwa nchi yetu. Kwani kwenda pale Mwenge amepoteza nini? Wangapi wamepita kwenye wizara hii hawajawahi hata kunusa hiyo kero ya mwenge kwa pua yao? Kushitukiza kunasaidia kupata hali halisi. Tumpongeze kwa alichokifanya badala ya kumponda. Hebu tuwe wakweli na halisi. Wangapi wame-apply management za vitabuni na zimefeli? Tusilete management za vitabuni kwenye nchi kama hii ambayo imeoza kwa ufisadi. Hata Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alitumia approach tofauti ktk uongozi wake na alikuwa anafanikiwa sana. HEKO DR MWAKYEMBE, MUNGU AKUPE NGUVU ZAIDI ZA KUTUMIKIA WATANZANIA KADIRI ATAKAVYOKUWEZESHA>
 
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harison Mwakyembe amejikuta katika wakati mgumu katika ziara yake ya kushtukiza alyoifanya katika kituo cha mabasi Mwenge.

Waziri huyo alifika maeneo hayo na kuanza kuamrisha madereva wa mabasi yanayofanya safari za Makumbusho-Bagamoyo waondoe mabus hayo kwa sababu sio mahali stahili.


Aliwaamrisha wayapeleke mcus hayo katika kituo cha Makumbusho kama ambavyo imeandkwa kwenye magari yao.

Ndipo madereva, makondakta pamoja na wapga debe walipomjia juu na kumwambia kuwa serikali imefanya ufisadi wa kuuza eneo la makumbusho ambako hvi sasa panajengwa Ghorofa.

Madereva hao waliskika wakisema kuwa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na serikali ya CCM.

Madereva hao walisema kuwa hawaondoki eneo hlo hadi hapo watakapopatiwa eneo jngne ambalo linatakiwa.

"Haiwezekani kila siku tunalipia ushuru hapa halafu leo unakuja kusema kuwa si sahii. Hakikisheni kuwa kituo cha makumbusho kinarekebishwa ndipo sisi tuende huko" Aliskika mmojawapo wa madereva hao.

Palitokea mzozo mkali wa maneno baina ya Waziri Mwakyembe na vijana hao wanaofanya kazi katika daladala hzo.

Mwishoni kabisa waziri Mwakyembe alisikika akisema "Suala la eneo la Makumbusho nimelisikia na nitalifanyia kazi"
mwishoni ikabidi awpe number za simu ili awasiliane nao ndpo akaamua kuondoka kwa aibu bila kuacha maagzo yoyote

My Take: Napenda viongozi wasipende kufanya ziara ya kushtukiza bila kufanya uchunguzi kwanza kupitia wawakilishi.

Chanzo Cha Habari ni Mimi mwenyewe nilikuwepo eneo la tukio..


Ni jambo zuri kwa Waziri kufanya kazi mtaani na kukutana na watu kama hivi.Ni jambo jema. Ila ukienda ndani zaidi unaona kwamba hayo ni matokeo ya mfumo ambao haufanyi kazi. Umekufa kabisa.God help us!
 
Hao madereva wamemuonea mwakyembe mchapa kazi makosa ni watendaji wa magufuli
mbona pale mwenge pembeni ukielekea ubungo daladala zimepafanya stand, mbele kidogo magari ya
mbao yanshusha mizigo na kupunguza ukubwa wa Barabara

yeye na watendaji wake hawaoni ila wanaona magari ya vifusi na mchanga na kuyakamata kuyapeleka ofisi
za tonroads mkoa dsm tu wapime uzito hivi wanashindwa nini kwenda kule mwanzo wa lami yaani bunju yapoanzia kukanyaga lami ili mzigo ukizidi wapunguze hawa watendaji wako kimaslahi zadi Magufuli mwambie huyo meneja wako afanye kazi na sio kuchagua kazi zenye rushwa wajue ya kwamba matumizi ya parking ndani ya barabara ni uharibifu mkubwa wa barabara
lakini wao wanawaza kukamata
 
Kaka mwakyembe ni jembe wala huyko kimaslahi kama watendaji wa Tonroads mkoa

Wanutumia mzani ule wa Mobile kwa manufaa yao na sio manufaa ya taifa

kwa akili ya kawada mzani ni mobile kwa nini usiende kuzuia kwenye source unasubiri magari yaharibu kwanza ndipo uyazuie hiyo akili matope hakuna kingine zaidi ya Rushwa ndiyon maana hawataki kwenda unakotokea mzigo hawatapata

rushwa huku barabara zinaharibika Magufuli ondoa mamenaja ambao sio wabunifu wapeleke huko kwenye mizani ya kudumu
 
Kwa jinsi source ilivyo, unaweza kusema Mwakyembe hakujiandaa.
Lakini ni vigumu kujua utashi wa visit yake maana kuna mtu kasema alikuwa anaongelea
mpaka kuhusu nauli sasa ni vigumu kujua ukweli je alienda kuwafukuza kweli ama
kuna vitu alitaka kujua!
 
Tuache kuwa wanafiki jamani. Wakati Mrema waziri wa mambo ya ndani alikuwa anasifiwa kwa tabia yake yakushtukiza na kuwapa watu siku 7. sijui kwa sababu anaongea lugha moja na CDM . Leo Mwakyembe anafanya kama Mrema anakosolewa.

Hivi kwa akili zenu CDM mnaweza kweli kuongoza nchi? mimi bado sijaona mbadala wa CCM bali nachoona watu wameichoka CCM tu na hii ni hatari maana CDM ni janga la Taifa.

Mwakyembe piga kazi
 
Sijaona sehemu aliyoshushuliwa ..
Zaidi ya mazungunzo ya kawaida. Tu
 
Wewe ndo mnafki. Hivi ukweli huo alpashwa kuupata moja kwa moja toka kwa watu wa chn yake au wapga debe?

Utendaji kazi wa style hii ndiyo uliobaki, wengine wamegoma, mfumo umefail unafanyaje? inabidi uweke juhudi binafsi ujitoe kimasomaso - haya ndiyo yaliyojitokeza kwa bajeti ya Magufuli wiki hii -siyo mafanikio ya serikali wala chama ni ya binafsi
 
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harison Mwakyembe amejikuta katika wakati mgumu katika ziara yake ya kushtukiza ......
Chanzo Cha Habari ni Mimi mwenyewe nilikuwepo eneo la tukio..

Weka picha ili tujue kuwa ulikuwepo eneo hilo.!
 
Mbona sijaona sehemu aliyoshushuliwa hapa. Zaidi wamempatia ukweli kwa ajili ya kuufanyia kazi. Ili kama kuna mtu aliuziwa kituo chao pale Makumbusho then Mwakyembe anatakiwa afuatilie na kuwapatia ufumbuzi...tuache ushabiki wa kijinga.

Mbona huangalii vitu kwa jicho la uchunguzi? Hivi Waziri mzima kuchoma mafuta na kuacha Bunge na kuja kuamrisha jambo ambalo serekali na Manispaa ya chama chake wameshaua si kuumbuka? Hivi asingeweza kujipanga akafuatana na meya na mkurugenzi wa kinondoni ili ziara yake ikawa endelevu! Mwakyembe anacholenga ni kujitofautisha na wenzie kisanii tu. Tusipowashtukia makada w a aina hii ubabaishaji hautaondoka.
 
Back
Top Bottom