Waziri Mwakyembe ashushuliwa.

Waziri Mwakyembe ashushuliwa.

Nimependa mtazamo huu ijapokuwa humo mwenye bold sikubaliani na wewe. Ni kweli kabisa kituo cha Mwenge kinatisha na kielelezo cha ubovu au uduni wa mipango miji. Lakini tatizo la pale si la viongozi peke yake. Watanzania pia tuna matatizo makubwa. Hatuna discipline au nidhamu ya maisha. Watanzania ni wavivu na watovu wa nidhamu wakubwa. Tunataka kufanyiwa kila kitu. Ni waharibifu wa miundo mbinu tunayoitengeneza wenyewe. Fikiria wale wanaoondoa mifuniko ya maji taka barabarani au wale wanaoondoa vyuma kwenye madaraja. Fikiria yule anayeoona kibao kinachoonyesha bado kilomita 250 kuingia Moshi anaongeza ziro na kibao hicho kusomeka bado kilomita 2500. Watanzania ni walalamishi huku wakiwa wapenda sifa. Ni taifa la ajabu linalohitaji Dikteta kuliongoza.

Madaktari wamegoma wanaua lakini wako wanaoshabikia eti waendeleze mgomo. Madaktari ndio wanaovunja haki za binadamu kwa kuwaacha wagonjwa wafe bila msaada wa matibabu. Lakini wako wanaowaona madaktari eti ni mashujaa. Dk. Ulimboka amepigwa. Pole ulimboka, kwa kufanyiwa ushenzi. Lakini wenye vichwa vya boga wanaodhani kuwa serikali inahusika. Hawataki hata kufikiri kuwa hivi ni nani anaweza kufanya unyama dhidi ya Dk. Ulimboka. Wanakuja na majibu rahisi kwa maswali magumu eti aliyefanya unyama huo ni serikali. Stupid thinking. Wanasahau kuwa madaktari wamejitengenezea maadui wengi ambao wanaweza kuwa ndio wanaohusika.


Now back to the point. Dk. Mwakyembe is doing a fine job. Anafanya staili ya Kim il Sung. On spot guidance. Ila wako wanaochukia wakiwemo mahasimu wake ndani ya CCM na pia kutoka Chadema chama ambacho kina-capitalize matatizo ya watanzania sawa na NAZI party ilivyocapitalize matatizo ya wajerumani na kuteka nchi au kutwaa madaraka kwa kura. Kwa CHADEMA hakina kizuri ambacho CCM na viongozi wake wanaweza kufanya. Kila siku ni shutuma tu.

Nchi hii inaelekea kubaya. Wengi wetu tuna mawazo ya ajabu na yasiyo na tija. Maneno mengi bila tija. Kazi yetu kunywa kahawa tu kuanzia asubuhi mpaka jioni. Hatufanyi kazi isipokuwa kupiga soga na kuzungumzia masuala yasiyo na tija. Waandishi wa habari ndio hasa usiseme. Mawazo yao sawa na ya watanzania wenzao. Wanaandika ujinga usio na maana. Dk. Ulimboka amepigwa sawa. Sasa hiyo imekuwa ndio stori ya kuuzia magazeti. Wanaandika alivyopigwa ulimboka. Lakini hatuoni kwenye magazeti yao idadi ya watanzania waliokufa kwa unyama wa madktari na mgomo wao wa kishenzi wenye mwelekeo wa kisiasa. Stupid nation. Maneno mengi bila vitendo

M.B.W.A. ni strategy mbovu ya kiutawala. Kuhusu watu kutofanya kazi, serikali ilipaswa kuhamasisha au kutumia nguvu. CCM kwa hili lazima tuwalaumu. Kuhusu CHADEMA kutafuta umaarufu kupitia matatizo, mi nawapongeza! CCM wanapaswa kutafuta umaarufu kwa kuchapa kazi! Hii ndo dhana ya MULTIPARTISM. Tafakari mkuu!
 
hivi alishaishughulikia kweli kama alivyoahidi?
 
Mwakyembe mbona anakuwa km mfa maji?Shirika la ndege la Taifa mbona hakikusumbui au umeshindwa?
 
Back
Top Bottom