Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
Katika hali isiyo ya kwaida jioni hii, waziri muhongo amepetwa na kadhia ya aina yake hapa Dodoma alipokuwa akitoka kwenye duka la madawa. Vijana ambao wanasadikiwa kuwa madereva wa Bodaboda na wachuuzi, yaani wamachinga, walianza kumzomea kumuita "chura! Chura! Chura! Chura!" hali iliyompelekea Bw. Muhongo kutembea kwa haraka kuelekea kwenye gari iliyokuwa ikumsubiria pembezoni mwa barabara. Baada ya kufika kwenye gari, waliondoka kwa kasi ya ajabu kuelekea ofisi za bunge huku vijana wakiendele akumzomea !
My Take:
Huu ni mwanzo mbaya kwa hawa viongozi wenye dharau na wakorofi wa CCM. Watazomewa sasa hivi mpaka watakoma. Huyu muhongo angejaribu kujifunza ustaarabu kutoka kwa Mawaziri wasaidizi wizara ya Nishati na madini waliomsaidia kujibu maswali
My Take:
Huu ni mwanzo mbaya kwa hawa viongozi wenye dharau na wakorofi wa CCM. Watazomewa sasa hivi mpaka watakoma. Huyu muhongo angejaribu kujifunza ustaarabu kutoka kwa Mawaziri wasaidizi wizara ya Nishati na madini waliomsaidia kujibu maswali
![]()
Souece;TZ Daima
BAADHI ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora jana walipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Tukio hilo lilitokea kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika viwanja vya stendi ya mabasi zamani ambako walihudhuria viongozi mbalimbai akiwemo mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage.
CCM ilifanya mkutano huo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiongozwa na Naibu Katibu mkuu wake, Zitto Kabwe, kufanya mkutano katika eneo hilo na kuwachongea wabunge wa CCM Tabora kuwa hawatetei wapigakura wao.
Dalili za zomeazomea zilianza mapema kwani baadhi ya wananchi walianza kuibua vicheko na kejeli kwa viongozi wa CCM huku wengine wakisikika wakisema hawataki majigambo, matusi bali barabara za lami
kutoka Tabora-Nzega, Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora na wengine wakisema 'Peoples Power'.
Wakati Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Idd Ame, akizungumza kwenye mkutano huo, wananchi wachache waliokusanyika walianza kuzomea kila kiongozi huyo alipokuwa akijaribu kuikejeli CHADEMA.
"Ndugu zangu wananchi hebu angalieni mnavyodanganywa, hivi hawa CHADEMA wanajigamba kujenga barabara wakati wao siyo watoaji wa fedha…fedha zinatolewa na serikali ya CCM, hao CHADEMA ni wanafiki na waongo," alisema Ame.
Alisema inashangaza kuona mtu anaacha jimbo lake Kigoma kwenda Tabora kuwafundisha siasa na kudai kuwa huo upumbavu.
Baada ya kauli hiyo, wananchi walipoanza kuzomea kwa nguvu na kudai wanataka sera na si matusi.
"Hapa tuko kamili endeleeni kuzomea tu…tutaumizana kwelikweli hapa msifikiri hatuwezi na tutawashitaki viongozi wa CHADEMA Tabora kwa kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu," alisikika akisema Katibu huyo wa CCM.
Wakati katibu huyo akitamka hayo, Mjumbe wa NEC John Mchele alikwenda jukwaani na kumnong`oneza katibu huyo, ndipo ilizuka fujo kubwa huku Green Guard wa CCM wakitembeza mkong`oto kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakionesha ishara ya vema.
Tafrani hiyo ilidumu kwa dakika 20 na ndipo askari polisi walipoongezwa na mkutano kuendelea.
Baada ya vurugu kutulia huku wananchi wengine wakiondoka, mbunge Tabora mjini, Rage alipanda jukwaani na kutoa sh milioni 68 kwa kata 10 za manispaa hiyo na kila kata ilikabidhiwa hundi yake kwa ajili ya miradi ikiwemo ujenzi wa vyoo, umaliziaji nyumba za walimu na madarasa.
Aidha mbunge huyo alikabidhi chama cha waendesha bodaboda pikipiki mbili na kutoa ahadi ya kuendelea kusaidia.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM Tabora mjini Moshi, Abdurahaman Nkonkota alilaani Jeshi la Polisi kutolinda mikutano ya CCM hadi wanafanyiwa vurugu.