Waziri Mpina: Wasingechoma moto vifaranga ningewafukuza wote

Hivi hivyo vifaranga walivipima kujiridhisha kuwa vina ugonjwa au walivichoma tu kwa kuvihisi? Mbona walikataa visirudishwe vilikotoka?
 
Sheria ndiyo inaelekeza hivyo! Kwa ndege wakikamatwa kama ambavyo wanafanya kwenye bidhaa wanavyovichoma moto! Tuwe watafiti wa mambo kabla ya kupinga kila kitu! Mbona bidhaa nyingi tu huwa zinachomwa moto na huwa hamsemi zirudishwe ziliko toka?

Kama wangekuwa wamepimwa na waakakutwa na Maradhi ni hadi kuwachoma.Serikali ingekuwa hata fine tu na si kuchoma mtaji wa mtanzania mwenzetu
 
Kama wangekuwa wamepimwa na waakakutwa na Maradhi ni hadi kuwachoma.Serikali ingekuwa hata fine tu na si kuchoma mtaji wa mtanzania mwenzetu
Una hurumia huyo mfanyabiashara wa vifaranga na vifaa vya madukani na pharmacy ambao bidhaa zao huwa zinachomwa moto?? Kwa kuwa sheria imetamka hivyo then you need to comply with the country laws mkuu!
 
Reasoning and argumentation ni somo zuri na lilifaa sana kwa hawa viongozi wetu. Kutoa message kwa public na ikuelewe si kitu cha mchezo.
 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma moto vifaranga 6000 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege na kuteketeza mtaji wa aliyevileta ili kama kuna njia nyingine alizokuwa anatumia kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi hawezi kurudia tena

Na amesema askari waliohusika kamawasingechoma moto vifaranga vile, basi angewafukuza wote

Ukiwakuta mawaziri wanavyojinasibu kwamba kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara. Matendo yao sasa ni kama makamanda wa Polisi n wanashindwa ku assume executive role labda mkuu wao amewateua kuwa makamanda hasa wa awamu hii ni ngumu kujua nani amehitimu katika executive role. Wasichojua wanapata vip treatment sio kwa sababu ya kuwa watoa amri zaidi plse wastueni hawa jamaa.
 
Mnavyoijua Kenya jinsi walivyokuwa serious kwenye kilimo ni kweli hatchery ina vifaranga 6000 tu vingine viko wapi na havikuleta ugonjwa Uko Kenya.
 
Nadhani anatakiwa kuelimishwa juu ya ukatili kwa wanyama.

Kuratibu disputes na wafanya biashara kwasababu unachoma moto vifaranga ili iweje?!

Kwann wasingekabidhi hiyo gari kwa askari na wamshike huyo dada warudi nae mpakani kenya na kumwambia awarudishe aliponunua kwa gharama zake ili iwe fundisho na si kuwachoma moto kwa ukatili ule. Mbona utu siku hizi unakuwa ni bidhaa adimu najama pumbavu sana
 
Hii ni zaidi ya roho mbaya, yaani Serikali imekuwa kama mtu binafsi duuh..

Kwa upande mmoja watu wanaitazama dunia hivyo...ila kwa upande mwingine, tuanze kufuata sheria. Zipo ili tuepuke hizi hasara. Tunataka super profit na mara nyingine tunazipata...sasa ngoma ikikataa ndio hayo.
 
Waziri wa Ufugaji na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali ilichoma moto vifaranga 6000 kutoka Kenya ili kuzuia magonjwa ya ndege na kuteketeza mtaji wa aliyevileta ili kama kuna njia nyingine alizokuwa anatumia kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi hawezi kurudia tena

Na amesema askari waliohusika kamawasingechoma moto vifaranga vile, basi angewafukuza wote

Wamelewa sifa ili waonekane ni watendaji wazuri kwa aliyewateua...sifa zenu zina ukomo!
 
Back
Top Bottom