Waziri Mkuu umeteleza kwa hili la walimu kuishi karibu na shule

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
WALIMU KUKAA KARIBU NA SHULE:

1. Utawalipia kodi ya nyumba?

2. Wengine wameshajenga mbali na shule, je watapewa hasara ya kwenda kupanga?

3. Wengine wameolewa na waume zao wako mbali kidogo na mji, je ndoa ikivunjika watapewa waume wengine?

4. Maeneo mengine karibu na shule NYUMBA zina bei ghali sana kulingana na mazingira na hivyo walimu hutafuta unafuu mtaani. Je wataongezewa mshahara kidogo ili wakidhi kodi?

5. Je, kuna NYUMBA za kutosha kwa walimu karibu na shule? Kama hakuna kuna walimu wanafamilia hawawezi kuishi maisha kama yupo geto,kisa tu kuwa karibu na shule.

Deogratius Kisandu.
 
Asingefanya kama amri. Angetoa ushauri tu. Kwani kama wafanyakazi wengine hawaamrishwi sehemu ya kuishi si vema kuamrisha waalimu.
Kama ni shule za boarding huwa zina nyumba nzuri za walimu karibu. Hapo waalimu huwa wanakaa bila hata kuambiwa.
Ila hizi za kata sijui.
 
WALIMU KUKAA KARIBU NA SHULE:

1.Utawalipia kodi ya nyumba?

2. Wengine wameshajenga mbali na shule, je watapewa hasara ya kwenda kupanga?

3.Wengine wameolewa na waume zao wako mbali kidogo na mji, je ndoa ikivunjika watapewa waume wengine?

4.Maeneo mengine karibu na shule NYUMBA zina bei ghali sana kulingana na mazingira na hivyo walimu hutafuta unafuu mtaani. Je wataongezewa mshahara kidogo ili wakidhi kodi?

5.Je, kuna NYUMBA za kutosha kwa walimu karibu na shule? Kama hakuna kuna walimu wanafamilia hawawezi kuishi maisha kama yupo geto,kisa tu kuwa karibu na shule.

Deogratius Kisandu.
Deo kwa kweli umeuanza mwaka vizuri. Post hii imetulia na umeandika kwa umakini sana. Basi kama ni maradhi yalikuwa yanakusumbua tumuombe Mungu mwaka huu akuponye ili urudi kuwa wa kawaida
 
Tatizo lililopo viongozi wetu tuliowapa mamlaka makubwa upeowao wakufikiri mbali ni Mdogo sana.1 maisha wanayoishi wao wanathani kila mtu wanaishi kama wao,2 hawapimi uzito wa matamshi wanayotoa kama kiongozi, 3 viongozi tuliowachagua hawafanyi tafiti nakama wanafanya wanazipuuza katika kutatua kero za wananchi matokeo yake mtu anaongea tu ili mradi tu katoa maagizo
 
Back
Top Bottom