Waziri mkuu Pinda kuzindua chopper ya Gwajima

Waziri mkuu Pinda kuzindua chopper ya Gwajima

Njia nyepesi kutambua hilo 0+9+1+1+2+0+1+4=18 (18÷3=6) 6+6+6=18 kwa jumla ya namba hizo kwa jicho la Tatu ni 666 je ni kweli Mungu huyu wa mbinguni anaabudiwa.......??? Tafakari
 
Sijui kwanini hakualikwa yule mzee VP mtaalamu wa kukata utepe shughuli kama hizo ndo zake hasa
 
Yale yaliyokuwa yakisubiliwa kwa hamu kubwa na watu wengi juu ya ukweli kuhusu kummmiliki kwa helicopter mchungaji Josephat Gwajima hatimaye yanatimia.ikiwa zimebakia siku na masaa machache kwa tukio hili kuchukua nafasi pale maeneo ya KAWE katika VIWANJA VYA WAZI VYA TANGANYIKA PAKERS ambapo litafanyika tukio hilo kubwa na la kihistoria.Katika ufunguzi au uzinduzi wa chombo hicho cha usafiri ambacho kitazinduliwa au kufunguliwa na Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda katika maeneo hayo ambayo kanisa hilo huabudia,mbali na waziri mkuu na viongozi wengine wa kisiasa pia amesema ya kwamba kutakuwa na viongozi wengi wa madhehebu mbalimbali na dini mbalimbali huku akisikika akiwakaribisha kila mmoja kufika katika kushuhudia tukio hilo.Nikiwa kama mmoja kati ya watu ambao tulikuwa tukifuatilia na kutaka kujua ukweli halisi kamwe sintotamani kukosa kufika eneo hilo ili kushuhudia tukio hilo.
 
OK, OK, OK, OK, helicopter inazinduliwa, itasaidia kupeleka watu mbinguni!!!!!????, au itasaidia kuongeza kipato cha nabii!!!!??
 
Eti Nabii.?!!!!.. Dah yani shetani akikupiga upofu bora hata mlemavu wa macho. Kazindueni bwana ndo wakati wa utawala wa yule mnyama.
 
SASA NI RASMI: Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania; Mhe Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuzindua helicopter ya kanisa la Ufufuo na Uzima, jumapili hii. Helicopter hiyo aina ya Robbinson 44 itakayotumika kuhubiri injili na kutoa misaada ya kijamii pale itakapohusika itazinduliwa jumapili hii ya tarehe 09.11.2014 katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe - Dar es Salaam.

Pamoja na uwepo wa Waziri Mkuu, pia kutakuwa na viongozi mbalimbali wa dini na kiserikali watakaoudhuria; kutakuwepo pia na maaskofu kutoka makanisa ya katoliki, maaskofu kutoka CCT, maaskofu wa makanisa ya kiroho pamoja na maaskofu wa makanisa yote ya Ufufuo na Uzima Tanzania. Pia, pamoja na wageni waalikwa wengine, shehe mkuu wa baraza la kiislamu Dar es Salaam (BAKWATA -Dar es Salaam).

Kanisa la Ufufuo na Uzima ambalo liko chini ya Mch. Josephat Gwajima, sambamba na Helicopter hiyo pia mwakani lina mpango wa kuleta ndege nyingine mbili za abiria. Wakati huo huo taratibu za kujenga uwanja wake wa ndege, utakao milikiwa na kanisa hilo zimekwisha kamilika ikiwemo swala la kibari n.k.

Kanisa hilo ambalo pia linasomesha wanafunzi wengi ndani na nje ya nchi na kusapoti shughuli mbalimbali za kijamii mwezi uliopita liliendesha changizo la kusapoti madawati katika shule za msingi za Kawe. Pamoja na hayo tayari ramani ya Hospitali kubwa inayotarajiwa kujengwa kwa udhamini wa kanisa hilo; ipo tayari ikisubiri taratibu za kiserikali na kiafya kuanza kujengwa.

Akiongea jumapili hii Mchungaji Gwajima alisema sherehe hizo zitaanza mapema asubuhi ya siku hiyo. Na tayari jeshi la polisi litakuwepo kuhakikisha usalama.

View attachment 198886
Mkutano wa Mchungaji Gwajima mkoani Tanga

Naamini anaizindua Lowassa???siyo?
 
Back
Top Bottom