Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Nduli, Iringa kwenye msiba wa Diwani Chonanga

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
WAZIRI mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa jioni ya leo amewasili mkoani Iringa na kufika nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa kata ya marehemu Idd Chonanga na kuungana na waombolezaji katika kuifariji familia ya diwani huyo.

Waziri Pinda ambae aliongoza na mkewe mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Iringa pamoja na viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma walifika nyumbani kwa marehe mu Chonanga eneo la Nduli majira ya saa 10.56 na kutumia muda wa zaidi ya dakika 10 kuifariji familia hiyo.

Akiwa nyumbani kwa marehemu Chonanga waziri Pinda na mkewe wametoa pore kwa familia hiyo ya Chonanga na kuwaomba kuendelea kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na kuwa wao katika chama wapo pamoja na familia hiyo katika maombolezo hayo .

Waziri Pinda amesema kuwa binafsi kama mlezi wa CCM mkoa wa Iringa ameguswa na kifo cha diwani Chonanga na kuwa kutokana na kuwa katika ziara ya kichama mkoa wa Iringa ameona ni vema kabla ya kuanza shughuli za chama kufika kuhani msiba huo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kuwa CCM wilaya ya Iringa mjini na mkoa kwa ujumla wamepata pigo kubwa kwa kifo cha diwani huyo na kusema kuwa CCM itashiriki kwa asilimia 100 mazishi hayo yatakayofanyika mapema kesho katika kijiji hicho cha Nduli.

Kwa upande wake Greyson Chonanga ambae ni mtoto wa marehemu Chonanga ameeleza kufurahishwa na hatua ya waziri mkuu kufika kuhani msiba huo na kuwa wao kama familia hawakutambua kuwa msafara mkubwa kama huo wa kitaifa ungefika kuhani msiba huo.
Huku wakazi wa eneo hilo la Nduli wameelezwa kufurahishwa na umoja wa kweli uliopo ndani ya serikali ya CCM kutokana na viongozi wake kuwajali watu wa chini wanaowaongoza na kuwa utu ambao waziri mkuu ameonyesha ni upendo tosha kwa wana Nduli kwa serikali ya CCM.
Alisema Adam Kalinga mkazi wa kata hiyo ya Nduli ambae alikuwepo msibani hapo kuwa katika kuenzi kazi za marehemu Chonanga wao wataendelea kutambua mchango wake .


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa pili kulia akitoa akiitambulisha familia ya marehemu diwani Idd Chonanga aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli aliyefariki dunia jana



Mtoto mkubwa wa marehemu Idd Chonanga Bw Greyson Chonanga akipewa mkono wa pole na waziri mkuu Mizengo Pinda aliyefika nyumbani kwao eneo la kijiji cha Nduli kuhani msiba huo jioni ya leo. Anayeshuhudia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu


Viongozi mbali mbali wa CCM na serikali mkoa wa Iringa wakiwa na waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana




Mtoto mkubwa wa diwani Chonanga akitoa maelezo kwa waziri mkuu Pinda juu ya kifo cha baba yake

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiomboleza msiba wa diwani Chonanga leo katika kijiji cha Nduli Iringa mjini

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiwaaga waombolezaji leo

Waziri mkuu akiaganga na familia ya marehemu Chonaga leo kijiji cha Nduli Iringa mjini




Mtoto mkubwa wa marehemu Chonanga akimuongoza waziri mkuu na msafara wake kuondoka eneo hilo

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akiwapa pore wafiwa


Ndugu wa diwani Chonanga wakiangana na waziri mkuu Pinda

Waziri Pinda akiagana na famili ya marehemu Chonanga leo

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kushoto akiwa na mke wa waziri mkuu mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mjini Iringa

Mwenyekiti wa CCM mjini Iringa Abed Kiponza akimng'ata sikio mama Tunu Pinda

Familia ya marehemu Chonanga akifurahia baada ya kutembelewa na waziri mkuu








Msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda ukitoka kuhani msiba wa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana na kuzikwa kesho kijijini hapo.
Viongozi mbalia mbali ya serikali ya chama tawala mkoa wa Iringa wakiwa wamejipanga tayari kumpokea waziri mkuu Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa aliyetua Iringa kwa ziara ya kichama mkoani hapa , kutoka kushoto ni mjumbe wa NEC Iringa mjini Bw Madenge, mjumbe wa NEC na mbunge wa Kilolo Prof Peter Msolla ,meya wa Iringa mjini Amani Mwamwindi, mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Bw Kiponza ,mwenyekiti wa CCM Iringa vijiji mama Mtafilalo na madiwani wa Iringa vijiji na kamada wa UVCCM mkoa Salim Asas wa 8 kulia
Wahudumu wa Ndege iliyomleta waziri mkuu wakijiandaa kuagana nae
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akimpokea waziri mkuu Mizengo Pinda
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba akimpokea waziri mkuu
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu akimpokea waziri mkuu
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gerald Guninita akisalimiana na waziri mkuu

Ofisa wa magereza Iringa akimpokea waziri mkuu
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akisalimiana na waziri mkuu Mizengo Pinda ikiwa ni kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa kuongoza mkoa wa Iringa kama kamanda wa polisi baada ya Michael Kamuhanda kupandishwa cheo





kada wa CCM mzee My Studio akisalimia na waziri mkuu

Jembe la manispaa ya Iringa mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa Teresia Mahongo akimpokea waziri mkuu Mizengo Pinda kwa tabasamu kali


Meneja wa Tanroads mkoa wa Iringa ambae anafanya makubwa katika barabara ya Iringa - Dodoma Paul Lwakurwa akipongezwa na waziri mkuu kwa kazi nzuri



Makada wa CCM kutoka vyuo wakimpokea waziri mkuu pichani na Bwana Alcard

Makada wa CCM familia ya My Studio

Wadau wa masuala ya utalii mkoa wa Iringa ambao wanapigania kuitangaza hifadhi ya Ruaha na hifadhi za kusini

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo JOseph Muhumba akisalimiana na waziri Pinda

Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiteta jambo na waziri mkuu Mizengo Pinda katika uwanja wa Ndege Nduli le
 
Naomba viongozi woote ws CCM wafe...shetani endelea kuua haya maccm maana ni mashetani wenzako.hizi ni habari njema kusikia maccm yanakufa!
 
Kifo huwalinganisha wote, CCM na CHADEMA. Kaburi ndo mwisho wa ubabe. Tutende mema tukiwa hai, chama chako hakitakuwepo wakati wa hukumu. Askari wa Tanzania akamuuliza Yesu, na sisi askari tufanye nini? Yesu akamjibu, watendee watanzania wote sawa bila kujali itikadi zao za siasa au dini.

Mungu amsamehe marehemu, nahisi hakujua alipokuwa anatenda. Pole sana Mwanadiwani, bila shaka kwa kuondokewa na baba yako. Mwanadiwani umebaki hai, nakuomba unapotumiwa na CCM hufikirie kesho ya kifo. Diwani sasa anaulizwa kwa nini alimpiga mbunge, CCM hakipo kumtetea. Dunia mapito.
 
watatuua kwa mabomu lakini wajui nao watakufa kwa shinikizo la damu kudadadeki bado pale magogoni akina rama na wapumbavu wenzao...
 
Halafu hao watoto wa huyo diwani wamekaa kimauaji mauaji....Wwnaonesha ni vibaka wazoefu..
 
  • Thanks
Reactions: JGG
watatuua kwa mabomu lakini wajui nao watakufa kwa shinikizo la damu kudadadeki bado pale magogoni akina rama na wapumbavu wenzao...
Huyu jamaa anatuletea habari ya watu walio kufa kwa ulafi ukawa sababishia shinikizo la damu mpaka 2015 wataisha wote
 
Naomba viongozi woote ws ccm wafe...shetani endelea kuua haya maccm maana ni mashetani wenzako.hizi ni habari njema kusikia maccm yanakufa!

Mkuu pamoja na LIKEA niliokupa nakuunga mkono asilimia mia moja
 
100% unajua kungalia picha, maana hapo wamesughuriwa kwamba PM anakuja lakini wapi hawakutakata......ukiangalia sura zao ni majambazi kabisa hao

Halafu hao watoto wa huyo diwani wamekaa kimauaji mauaji....Wwnaonesha ni vibaka wazoefu..
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Naomba viongozi woote ws ccm wafe...shetani endelea kuua haya maccm maana ni mashetani wenzako.hizi ni habari njema kusikia maccm yanakufa!

ama kweli mwisho wa roho mbaya ni aibu! Huyu jamaa na watoto zake ndo walitaka kumuua mbunge msigwa kwa mapanga na mahakama ikawakingia kifua lkn mwnyz mungu mtenda haki kaonyesha kuw wao ndo wanatakiwa wafe kabla ya msigwa. kifupi nngefurahi zaidi wangekufa na hao watoto.
 
Hilo vazi la mwenyekiti wa chama wa mkoa ni kama gwanda la chama fulani wanalolipiga vita bungeni isipokuwa rangi. Angalia rangi ya gwanda la mwenyekiti wa cdm halafu na hilo. Mimi kwa mtazamo wangu cdm sio kwamba wana vazi maalum ila walichagua kutoka mavazi yalipo na kupendwa na vijana. Wangeweza kufanya jeans kuwa uniform sijui wangeacha kuvaa ma-jeans!
 
E84A0574.JPG


Hawa watoto wa Marehemu walio kulia kwa Waziri Mkuu Pinda ndio waliokwenda kuwakata mapanga wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa CHADEMA na ambao kesi yao iko mahakamani?
 
Back
Top Bottom