Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya mkutano na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video na kuwaagiza wakague maghala ya mawakala wa saruji na wakiwakuta wamerundika mzigo wa cement wawakamate na kuwafungulia mashtaka.
Mh Majaliwa amezitaka kamati za ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhusika katika operesheni hiyo.
Source EATV
Maendeleo hayana vyama!
Mkuu,
Inasadikika hao wafanyabiashara wana mgomo baridi kushinikiza serikali iruhusu upandaji wa bidhaa ili wavune mara ya mwisho kabla usafiri wa umma kupitia treni haujaanza kusafirisha na gharama kupungua.
Lakini la pili inasadikika waliahidiwa endapo mgombea fulani wa Urais angeshinda basi kila mmoja angekuwa huru kupandisha atakavyo ili kupata faida kubwa kurejeshea kudorora kwa kipato kilichopindukia uhalali.
Kama viwanda wazalisha wanadai hawajapunguza kiwango cha uzalishaji, hawajaongeza bei, serikali haijapandisha kodi, mafuta hayajapanda, miundo mbinu ya usafirishaji ni ile ile na wafanyakazi ni hao hao ambao hawana mikataba na mishahara stahiki iweje mawakala wa usafirishaji wapandishe bei?
Kwa mfano Dar, viwanda vinatengeza aina ya simenti ambayo inatakiwa kuuzwa mikoani hivyo mawakala na wasafirishaji huuziwa kwa bei ya chini kiasi ambacho kwa kulingana na umbali bei elekezi haikutakiwa kupata kwa vyovyote vile lakini cha ajabu hiyo simenti inayotakiwa iende mikoani inaonekana Dar tena kwa bei ya juu zaidi na ile inayotakiwa iuezwe Dar kwa mwongozo wa viwanda inaonekana michache ambapo maana yake ni hujuma kama ilivyotajwa hapo juu.
Swali la kujiuliza kama uzalishaji wa bidhaa ya simenti, bati na nondo ni mwingi kwanini wafanyabiashara hawaendi kununua kiwandani?
Inakuwaje, wasafirishaji wa bidhaa hizi muhimu katika ujenzi wanatumia muda mrefu kusubiria zamu ya upakiaji kiasi cha kuongeza gharama za uendeshaji kwa wafanyabiashara?
Je, ni kweli serikali ndio waliosababisha bidhaa hizi kupanda bei kwa madai kwamba karibu robo tatu ya bidhaa hizo zinapozalishwa zinakuwa kwenye oda kwenda kwenye miradi ya kimkakati?
Serikali isifanye pupa wasije wakaumbuliwa baadae kwa baadhi ya watumishi wanaosimamia taratibu kula njama na wafanyabiashara wachache wasiowaaminifu kuipaka matope serikali mpya baada ya uchaguzi kukamilika.
Tanzania kuna viwanda vingi sana vya simenti
1. Twiga simenti-Dar
2. Nyati simenti-Kimbiji
3. Lucky simenti-Kisarawe
4. Armstrong simenti-Mkuranga
5. Mbeya simenti-Songwe
6. Tanga simenti-Tanga
7. Kilimanjaro simenti
8. Kiluwa Steel iron (NONDO)-Mlandizi Pwani
9. Dangote simenti-Mtwara nk
Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi wa ueledi na kuchukua hatua haraka iwezekavyo kunusuru wananchi masikini kuharibiwa bajeti zao ambazo zinasababisha washindwe kukamilisha ujenzi wa makazi kwa gharama ya vifaa vimepandishwa pasipo na sababu za msingi.
Kwa upande mwingine inathibitisha serikali kupitia baadhi ya watumishi wasimamizi wa taratibu kushawishi upandishaji bei holela, maana wanaposema bei elekezi kwa Dar isizidi 15,000/= wakati mwezi wa Julai hadi Septemba bei ilkuwa 13500/14000 hii sio sawa kabisa. Kwa Morogoro bei elekezi ilkuwa kati 14000 na 15000 kwa miezi tajwa hapo juu imekuwaje ipande kipindi cha uchaguzi hadi sasa wakati serikali imethibitisha haipandisha kodi? Maduka mengi ya vifaa vya ujenzi ikiwa pamoja na simenti, nondo, bati na vifaa vya umeme yamefungwa .
Wananchi wanapolalamikia upandishaji huu usiozingatia hali ya kiuchumi ya qraia wake, wasikilizwe, matatizo sababishi yafuatiliwe haraka na kupewa ufumbuzi ipasavyo.
Haitashangaza mawaziri watakapo tangazwa na kupangiwa jwizara za kuziongoza bidhaa na huduma zilizopanda zikashuka ni suala la muda kujidhihirisha ili mtambue pia wabunge ni wafanyabiashara ambao wanatetea maslahi ya biashara zao kwa hiyo kama hajui atateuliwa ama la ndipo inatokea mianya hii ya kuleta taharuki.
Tutakumbushana baadae