Waziri Mkuu Majaliwa: Wakuu wa Mikoa kagueni Mawakala wa Saruji, mkiwakuta wamerundika mzigo wakamateni mkawashitaki!

Safi sana waziri mkuu, tena ikiwezekana wafunguliwe kesi za ujujumu uchumi, hii itasaidia sana kupunguza bei ya saruji si unaona jinsi mlivyofanikiwa kushasha bei ya sukari, sukari sasa mtaani imeshuka kilo ni sh 800 kutoka 1800 aliyoiacha kikwete!
 
PM sijui kama anatambua kuwa ktk kufanya biashara kuna suala la "warehousing" ambalo lipo halali kabisa kisheria. Kuhifadhi bidhaa kwa muda kwa matarajio ya kupata faida baadaye kutokana na "seasonal availability of goods at the market" ni mojawapo ya "speculative motive" ya mfanyabiashara kutengeneza faida ya uhakika....
Jiandae kupigwa uhujumu uchumi na money laundering
 
Mwambieni aitishe kikao kingine, dumu la mafuta ya kula liter 20 bei ya leo ni shilling 80,000/=

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Aisee! Mwaka huu mwanzoni huku kwetu tulikuwa tunanunua dumu 56k, ikapanda taratibu hadi 75k kufikia mwezi wa 6. Nikaona isiwe tabu, nikaachana na biashara hiyo
 
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya mkutano na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video na kuwaagiza wakague maghala ya mawakala wa saruji na wakiwakuta wamerundika mzigo wa cement wawakamate na kuwafungulia mashtaka.

Mh Majaliwa amezitaka kamati za ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhusika katika operesheni hiyo.

Source EATV

Maendeleo hayana vyama!
Wakishawashtaki ndio tutapata saruji?
 
Unapoficha cement Ina maana mzunguko unapungua.
Mimi Nina miezi 2 Sasa sijaona cement.
Kila siku nampigia wakala simu anasema bado wazo kuna foleni.nampigia wa nyati anasema kiwandani Kuna foleni ,nampigia wa camel anasema sio Leo Wala kesho.
Sasa cement umeenda wapi?
Kama viwanda vimezidiwa na mahitaji.
Mbona ishu ndogo waruhusu cement ya nje
Hivi mtu kama karundika cement yake unaanzaje kumkamata? Why not flood the market with lots of cement ili “aliyeficha” kama yupo ajione mjinga?

Hizi efforts zinapaswa kupelekwa huko cement inakozalishwa. Tunazima moto sana sisi
 
Baada ya vita mwaka 1979 serikali ya wakati huo ilijaribu mbinu hizi za kijinga kutaka kudhibiti bidhaa zisitoweke sokoni lkn waligonga mwamba vibaya.

Bidhaa ikiadimika ina maana iko kwenye short supply na moja kwa moja bei lazima ipande na ukilazimisha isipande ni sawa na kumlazimisha mama aliyefika kujifungua asijifungue wakati muda umefika. Majaliwa ni sharti afahamu kuwa hamna uchawi hapo.
 
Kila siku nampigia wakala simu anasema bado wazo kuna foleni.Sasa cement umeenda wapi?
Kama viwanda vimezidiwa na mahitaji.
That is it. Shida ipo huko cement inapozalishwa. Huwezi kutatua shida hii kwa kudeal na mtu mmojamoja. Hakuna mtu anaweza “kuficha” cement kama soko lipo saturated na mzigo wa kutosha
 
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya mkutano na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video na kuwaagiza wakague maghala ya mawakala wa saruji na wakiwakuta wamerundika mzigo wa cement wawakamate na kuwafungulia mashtaka.

Mh Majaliwa amezitaka kamati za ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhusika katika operesheni hiyo.

Source EATV

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu,

Inasadikika hao wafanyabiashara wana mgomo baridi kushinikiza serikali iruhusu upandaji wa bidhaa ili wavune mara ya mwisho kabla usafiri wa umma kupitia treni haujaanza kusafirisha na gharama kupungua.

Lakini la pili inasadikika waliahidiwa endapo mgombea fulani wa Urais angeshinda basi kila mmoja angekuwa huru kupandisha atakavyo ili kupata faida kubwa kurejeshea kudorora kwa kipato kilichopindukia uhalali.

Kama viwanda wazalisha wanadai hawajapunguza kiwango cha uzalishaji, hawajaongeza bei, serikali haijapandisha kodi, mafuta hayajapanda, miundo mbinu ya usafirishaji ni ile ile na wafanyakazi ni hao hao ambao hawana mikataba na mishahara stahiki iweje mawakala wa usafirishaji wapandishe bei?

Kwa mfano Dar, viwanda vinatengeza aina ya simenti ambayo inatakiwa kuuzwa mikoani hivyo mawakala na wasafirishaji huuziwa kwa bei ya chini kiasi ambacho kwa kulingana na umbali bei elekezi haikutakiwa kupata kwa vyovyote vile lakini cha ajabu hiyo simenti inayotakiwa iende mikoani inaonekana Dar tena kwa bei ya juu zaidi na ile inayotakiwa iuezwe Dar kwa mwongozo wa viwanda inaonekana michache ambapo maana yake ni hujuma kama ilivyotajwa hapo juu.

Swali la kujiuliza kama uzalishaji wa bidhaa ya simenti, bati na nondo ni mwingi kwanini wafanyabiashara hawaendi kununua kiwandani?

Inakuwaje, wasafirishaji wa bidhaa hizi muhimu katika ujenzi wanatumia muda mrefu kusubiria zamu ya upakiaji kiasi cha kuongeza gharama za uendeshaji kwa wafanyabiashara?

Je, ni kweli serikali ndio waliosababisha bidhaa hizi kupanda bei kwa madai kwamba karibu robo tatu ya bidhaa hizo zinapozalishwa zinakuwa kwenye oda kwenda kwenye miradi ya kimkakati?

Serikali isifanye pupa wasije wakaumbuliwa baadae kwa baadhi ya watumishi wanaosimamia taratibu kula njama na wafanyabiashara wachache wasiowaaminifu kuipaka matope serikali mpya baada ya uchaguzi kukamilika.

Tanzania kuna viwanda vingi sana vya simenti

1. Twiga simenti-Dar
2. Nyati simenti-Kimbiji
3. Lucky simenti-Kisarawe
4. Armstrong simenti-Mkuranga
5. Mbeya simenti-Songwe
6. Tanga simenti-Tanga
7. Kilimanjaro simenti
8. Kiluwa Steel iron (NONDO)-Mlandizi Pwani
9. Dangote simenti-Mtwara nk

Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi wa ueledi na kuchukua hatua haraka iwezekavyo kunusuru wananchi masikini kuharibiwa bajeti zao ambazo zinasababisha washindwe kukamilisha ujenzi wa makazi kwa gharama ya vifaa vimepandishwa pasipo na sababu za msingi.

Kwa upande mwingine inathibitisha serikali kupitia baadhi ya watumishi wasimamizi wa taratibu kushawishi upandishaji bei holela, maana wanaposema bei elekezi kwa Dar isizidi 15,000/= wakati mwezi wa Julai hadi Septemba bei ilkuwa 13500/14000 hii sio sawa kabisa. Kwa Morogoro bei elekezi ilkuwa kati 14000 na 15000 kwa miezi tajwa hapo juu imekuwaje ipande kipindi cha uchaguzi hadi sasa wakati serikali imethibitisha haipandisha kodi? Maduka mengi ya vifaa vya ujenzi ikiwa pamoja na simenti, nondo, bati na vifaa vya umeme yamefungwa .

Wananchi wanapolalamikia upandishaji huu usiozingatia hali ya kiuchumi ya qraia wake, wasikilizwe, matatizo sababishi yafuatiliwe haraka na kupewa ufumbuzi ipasavyo.

Haitashangaza mawaziri watakapo tangazwa na kupangiwa jwizara za kuziongoza bidhaa na huduma zilizopanda zikashuka ni suala la muda kujidhihirisha ili mtambue pia wabunge ni wafanyabiashara ambao wanatetea maslahi ya biashara zao kwa hiyo kama hajui atateuliwa ama la ndipo inatokea mianya hii ya kuleta taharuki.

Tutakumbushana baadae
 
Maajabu haya! Tunatumia nguvu nyingi kwa mambo yanayohitaji akili tu. Ninunue mzigo wangu nitunze halafu iwe kesi?!

Je kama nataka kujenga safina? Je kama bei iliyopo sokoni ni ya hasara nilazimishwe kufilisika?! Sijui nchi zingine wanafanya vipi.

Njooni vijijini huku sass watu wametunza magunia kibao ya mpunga. Wayatoe ili tununue mchele sh.200/- kwa kg
 
Baada ya vita mwaka 1979 serikali ya wakati huo ilijaribu mbinu hizi za kijinga kutaka kudhibiti bidhaa zisitoweke sokoni lkn waligonga mwamba vibaya.

Bidhaa ikiadimika ina maana iko kwenye short supply na moja kwa moja bei lazima ipande na ukilazimisha isipande ni sawa na kumlazimisha mama aliyefika kujifungua asijifungue wakati muda umefika. Majaliwa ni sharti afahamu kuwa hamna uchawi hapo.
Unatuletea mambo ya mwaka 47 mkuu? Cement ipo ya kutosha ila wahuni fulani wanataka wapate faida kubwa kama ambavyo walitaka kufanya kwenye sukari lakini wakanyooshwa na hawa watanyooshwa tu hawa wahuni.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya mkutano na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video na kuwaagiza wakague maghala ya mawakala wa saruji na wakiwakuta wamerundika mzigo wa cement wawakamate na kuwafungulia mashtaka.

Mh Majaliwa amezitaka kamati za ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhusika katika operesheni hiyo.

Source EATV

Maendeleo hayana vyama!
Sasa hapa kazi ipo ,maana wasije kuta nimeweka mifuko yangu elfu moja ambayo ilishalipiwa na mteja lakini bado kufika chukua mzigo wake mkanipa kesi, hapo kwa kweli mkinipa kesi na mh pm anidhamini
 
Maajabu haya! Tunatumia nguvu nyingi kwa mambo yanayohitaji akili tu. Ninunue mzigo wangu nitunze halafu iwe kesi?!

Je kama nataka kujenga safina? Je kama bei iliyopo sokoni ni ya hasara nilazimishwe kufilisika?! Sijui nchi zingine wanafanya vipi.

Njooni vijijini huku sass watu wametunza magunia kibao ya mpunga. Wayatoe ili tununue mchele sh.200/- kwa kg
Mkuu jaribu kutumia akili zako vizuri kwanza. Usilinganishe mkulima wa mazao na mfanyabiasha. Mfanyabiashara ana leseni ya biashara iliyo na masharti wakati mkulima hana leseni hivyo hakuna masharti yanayombana!
 
Hivi mtu kama karundika cement yake unaanzaje kumkamata? Why not flood the market with lots of cement ili “aliyeficha” kama yupo ajione mjinga?

Hizi efforts zinapaswa kupelekwa huko cement inakozalishwa. Tunazima moto sana sisi
Hivi mtu huwa anaficha bidhaa kwenye "ghala" lake? Je awalazimishe wanunuzi kumaliza mzigo alionao?
 
Unatuletea mambo ya mwaka 47 mkuu? Cement ipo ya kutosha ila wahuni fulani wanataka wapate faida kubwa kama ambavyo walitaka kufanya kwenye sukari lakini wakanyooshwa na hawa watanyooshwa tu hawa wahuni.
Sasa wasukari waliponyooshwa vp bei ilishuka??Serikali ikitaka vitu viwe NAFUU si itengeneze na kuuza yenyewe??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom