Amesema wameshakaa na wenye viwanda vya kutengeneza pombe hizo na kuwaambia viroba kuwa kuanzia tarehe 1/3/2017 ni marafuku kutengeneza viroba.
Amewataka watengeneze pombe zenye ukubwa unaokubalika kwani viroba vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi.
Amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la kupiga vita dawa za kulevya
Wengine pombe kwetu ni mila na ibada utazuiajeMimi nilidhani wanazuia pombe kama pombe, kumbe wanazuia viroba tu.
Wengine pombe kwetu ni mila na ibada utazuiaje
Sijui itakuwaje sasa MALOKI hamna tena!Tumekwisha wakuu...
Kaka kwa kweli bado sijajuwa hasa maana yao, ni kupiga marufuku vile viplastiki sababu ya mazingira, au sababu vijana wanaharibika?! Na kama vijana walio chin ya 18yrs wanatumia loki wakushtakiwa na wauzaji na sio kutuumiza sie mkuu, mbona majuu tumeona kuna vinywaji vikali vya ujazo mdogo kama viroba kaka?!Sijui itakuwaje sasa MALOKI hamna tena!
Tafadhali! Tafadhali! Tafadhali.... futa kauli yakofuta hadi beer.
Hahaha wanafuta vifungashio?Mbona nilisikia wanafuta vifungashio na sio ggongo iliyomo kwenye kiroba
Juhudi yoyote inayosaidia hata mtanzania mmoja au mwanafunzi asiyejitambua na kuokoa uchafuzi wa mazingira inapaswa kupongezwa na kuungwa mkono. Ila Viwanda muda wa kutosha ili wabuni kinywaji mbadala ambacho hakina athari lalamikiwa sio flexible kama kiloba
Mkuu hiki kina double disadvantages ukiacha uchafuzi wa mazingira maana mifuko yake inamills kubwa kikubwa zaidi vinachochea unywaji wa kilevi kwa kificho watu wa makundi mbalimbali wakiwemo watoto na wanafunzi. Kuhusu mifuko ya plastic serikali iliyopita ilishatoa maelezo ni mifuko na vifungashio vyenye sifa zipi na Mills ngapi vyafaa kutengenezwa ambavyo ni environmental friendly otherwise viwe reusable.Namna gani mifuko ya plastic maarufu kama RAMBO ambayo ni mikubwa na inatumika kama vifungashio kila sehemu, madukani, sokoni, mikaa, buchani hadi hotelini!.? Au nayo ni sehemu ya viroba?
Mkuu hiki kina double disadvantages ukiacha uchafuzi wa mazingira maana mifuko yake inamills kubwa kikubwa zaidi vinachochea unywaji wa kilevi kwa kificho watu wa makundi mbalimbali wakiwemo watoto na wanafunzi. Kuhusu mifuko ya plastic serikali iliyopita ilishatoa maelezo ni mifuko na vifungashio vyenye sifa zipi na Mills ngapi vyafaa kutengenezwa ambavyo ni environmental friendly otherwise viwe reusable.
Sidhani kama inaweza kuwa hivyo maana uwepo wa Makampuni pamoja na kupata faida wanaangalia wellbeing ya society. Ila kwa maoni ya kina zaidi huwezi kuzuia ulevi kwa watoto au muda wa kazi kwa kubadil design ya vifungashio japo inapunguza kwa asilimia kadhaa. Nguvu kubwa zingewekezwa kwenye maadili ya familia maana mabadiliko ya technology yatatusogeza karibu na vitu vingi visivyofaa tena kwa spidi ambavyo wenda vingine visizuilike. Nimewahi kupanda bodaboda Bila kujua jamaa alikuwa na viroba mfukoni vingi tu na alikuwa amelewa. Itasaidia lkn kama ulevi ni addictive inabidi kama nchi tufikiri zaidi suluhisho la kudumu.Itakuwaje kama mawakala wa ulevi wataondoa viroba, badala yake watengeneze vichupa vidogo vidogo vya plastic au vya vioo lakini vikawa na uwezo wa kufichika na kubebeka kirahisi?