Waziri Mkuu Majaliwa: Viroba marufuku kuzalishwa wala kutumiwa kuanzia Machi 01, 2017

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059

Amesema wameshakaa na wenye viwanda vya kutengeneza pombe hizo na kuwaambia viroba kuwa kuanzia tarehe 1/3/2017 ni marafuku kutengeneza viroba.

Amewataka watengeneze pombe zenye ukubwa unaokubalika kwani viroba vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi.

Amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la kupiga vita dawa za kulevya
 
Utafiti wangu bubu unaonesha bei ya kiroba na gongo vinawiana, na sioni kinywaji kingine cha kuziba pengo la kiroba zaidi ya gongo... Hakuna na hakutakuwepo.

Tujiandae na biashara haramu ya viroba kutoka nje ya nchi (Zambia, Malawi nk) na gongo kurudi katika utukufu wake wa miaka iliyopita.

[HASHTAG]#YaLeoKali[/HASHTAG]
 
Sometimes common sense is not common, hii ni kwa faida ya vijana wetu, yaani utakuta vijana wamekaa tu kwenye viduka wananyonya viroba, nchii hii inaenda wapi jamani nguvu kazi ya taifa inapotea,kwanza pombe inawekwa kwa namna ambayo inaondoa hadhi ya pombe yenyewe na mmwaji wake, nakupongeza sana waziri mkuu kwa hilo, ila inabidi iwekwe rasmi kabisa, kiutaratibu yaani kisheria.
 
kabla ya viroba miaka ya 1992 vijana walikuwa na akili sana eeh?
 
Sometimes common sense is not common, hii ni kwa faida ya vijana wetu, yaani utakuta vijana wamekaa tu kwenye viduka wananyonya viroba, nchii hii inaenda wapi jamani nguvu kazi ya taifa inapotea,kwanza pombe inawekwa kwa namna ambayo inaondoa hadhi ya pombe yenyewe na mmwaji wake, nakupongeza sana waziri mkuu kwa hilo, ila inabidi iwekwe rasmi kabisa, kiutaratibu yaani kisheria.
kukiwa na ajira hayo ya kukaa tu yataisha..
 
Back
Top Bottom