VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ni jambo la wazi kabisa kuwa nchi imepoa. Wananchi hawana furaha. Furaha ya kidemokrasia. Furaha ya kuwasikia na kuwaona wanasiasa majukwaani wakisema na kutenda. Kisiasa na kisasa. Lakini, kwasasa nchi iko kimya na pweke kidemokrasia.
Tangu Waziri Mkuu Majaliwa alipotoa kauli ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa (ile ya kushukuru wananchi), demokrasia imefungiwa kwenye chumba chenye giza nene. Demokrasia inahitaji kutolewa ilikowekwa. Ili iweze kujionesha na kujidhihirisha. Mambo kama ya ubomoaji yangesikika kwenye majukwaa. Mambo ya Zanzibar pia.
Waziri Mkuu Majaliwa, umeiweka wapi funguo ya demokrasia? Tunaiomba. Wapenda demokrasia tunakuomba. Tunataka kuwasikia hata makada wa CCM yetu wanavyojibu bila aibu hata hoja za wapinzani wetu. Makada wana hoja za haja za kuwasambaratisha wapinzani.
Ukimya huu wa kidemokrasia, hakika, unaua vyama vya kisiasa kikiwemo hata CCM. Demokrasia ni mikutano ya kisiasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam