Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Habari kubwa kwenye magazeti ya Leo ni kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kuwapiga mkwara mzito, wagombea wa vyama vya upinzani kuwa wasitumie majukwaa ya kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni kuwachafua wagombea wenzao.
Ingawa hakuwataja kwa majina wagombea hao, ni dhahiri alikuwa na maana ya wagombea wa Chadema na ACT Wazalendo, ambao kwao CCM ndiyo wanawaona kuwa ni tishio kubwa sana kwao.
Ni jambo la kushangaza kauli hiyo kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu wa CCM, kwa kuwa katika kipindi chote cha miaka 5 iliyopita, chama cha CCM "kilijipendelea" kwa kufanya kampeni peke yao, nchi nzima, wakiwachafua na kiwatukana viongozi wenzao wa upinzani, huku wakivipiga marufuku vyama vya upinzani, kutofanya mikutano yoyote ya kisiasa ya kujibu mashambulizi hayo
Sasa inashangaza mno kwa viongozi hao wa upinzani wanapotumia fursa hii waliyoipata wakati huu kufanya kampeni kujieleza, Waziri mkuu anasema wasiwachafue viongozi wa CCM!
Hivi kwa mfano kauli iliyotolewa na kiongozi wa Chadema, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Urais Tundu Lissu, kuwa Rais Magufuli ametumia nafasi yake ya Urais kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa, huko kijijini kwake Chato na "kulazimisha" kuwa na mbuga yao ya wanyama ya Burigi, kwa Maelezo ya waziri mkuu, ni kumchafua Rais Magufuli?
Ninavyoona Mimi kama raia wa Tanzania, ambaye nina haki ya kutoa maoni yangu, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 18(1) uamuzi wa busara kwa viongozi wa CCM ni kwa Rais Magufuli kujitokeza hadharani na kujibu mapigo hayo ni kwanini yeye ameamua kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kwenye kijiji chake, kinyume cha viongozi waliomtangulia, akina Mwalimu Nyerere, Alli Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, hawajafanya kama yeye, aende kwenye majukwaa ya kisiasa ili atoe maelezo kama maneno aliyoyatoa Tundu Lissu ni ya uwongo. OVA