Waziri mkuu Majaliwa tuokoe walimu Bunda

Waziri mkuu Majaliwa tuokoe walimu Bunda

Mm nilidhani una tatizo umenyimwa uhamisho,sasa watoto wakirudia ww unaathirika vipi? Hayo ni maisha kila mtu anajaribu bahati yake basi kama vipi mkifundisha muwaruke wasielewe!!! Kweli walimu sisi tuna roho mbaya sana!!
 
Pole sana...ila huu ni upande mmoja wa habari.
Waandishi wa habari mtusaidie na upande wa pili ili kuweza kutoa ushauri bila upendeleo...
Afisa elimu anatumia taratibu na kanuni katika kutoa uhamisho wa watumishi wa wikaya yake.
 
Mheshimiwa waziri mkuu,afisaelimu wa wilaya Sistaimelda Lubengo anatunyanyasa,anatuonea,anatutisha,ni mkatili ni mbabe,anatumia vibaya madaraka yake.
Mh waziri mkuu walimu tulihojiwa kuhusu kuwepo wanafunzi waliorudia darasa la saba shuleni baada ya kuhitimu shule mbalimbali hapa mkoani,tulikiri mara kadhaa kuwa wapo hata hivyo hatua hii ilimkera afisaelimu kwa kuwa ni ndugu wa mwl mkuu,akidai tukiendelea kukiri atatoa uhamisho wa adhabu usio na malipo.
Wakaguzi wa elimu kanda walikagua shule wakagundua kuwepo wanafunzi hao hata hivyo walitoa taarifa ya uongo,waliungana na afisaelimu,afisa utumishi na mkurugenzi wa wakati huo kukandamiza walimu.
Mh,baada ya kuhamishwa tuliomba kulipwa gharama za uhamisho kwa kuzingatia kanuni za kudumu L.5 (1) na L 13.(1)hata hivyo afusaelimu aligoma kujibu barua mpaka alipolazimishwa na kaimu mkurugenzi wa wakati huo.Hata alipojibu aligoma kulipa,
Walifika wakaguzi wa elimu kanda ya ziwa walikagua shule,tulihojiwa, waligundua kuwa wanafunzi walirudia,na waligundua baadhi nyaraka za uhamisho zilighushiwa ili kuwahalalusha,waliandika taarifa kwa mamlaka zenye dhamana kuta ka zichukue hatua za kinidhamu kwa mkaguzi mkuu wa elimu wilaya na afisa elimu na mwl mkuu ambaye tayari kavuliwa madaraka.
Mh waziri mkuu sakata hili afisaelimu wa mkoa analijua fika,ofisi ya katibu tawala mkoa inalifahamu kwa maandishi na ushahidi upo.
Madai ya gharama za uhamisho yameendelea kuwepo,mazungumzo yamefanywa kati ya mkurugenzi na walimu hata hivyo afisaelimu ameendelea kukaidi kulipa na mkurugenzi wa sasa kwa mara nyingine wameungana kutukandamiza,kuminya haki.
Mkurugenzi ameandikiwa barua mara kadhaa na chama cha walimu wilaya CWT amegooma kuzijibu hadi sasa,licha ya kufuatwa na kuombwa na viongozi wa chama cha walimu,sababu anazijua yeye.
Mheshimiwa waziri mkuu,yapo mengi sana,hivyo tunaomba msaada wa ofisi yako mambo yafuatayo;
1.Kusema ukweli ni jinai?
2.Uhamisho wa adhabu ulianza lini?Kwa kosa lipi?Vituo tulivyohamishiwa ni gereza?Adhabu hiyo inaisha lini?
3.Ni kanuni ipi ya mwongozo wa elimu inayoruhusu waliohitimu f 4,waliofeli f2 na la 7kurudia elimu ya msingi,ili atakayehoji ajue amewakosea waliorudia na hivyo kustahili adhabu?
Tunaomba ofisi yako itusaidie kutusimamia kulipwa stahiki zetu.
Walimu Bunda.
 
Acha unaa ndugu mtoto kurudia wewe kinakukereketa nini?
 
Back
Top Bottom