chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,400
- 24,980
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya uzalishaji wa makaa ya mawe ya TANCOAL ni halali.
Waziri Mkuu akiangalia makaa ya mawe katika mgodi wa NgakaAmetoa kauli hiyo leo mchana mara baada baada ya kupokea taarfa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.
Waziri Mkuu amesema atamwagiza piamdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili apitie mahesabu ya kampuni tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” amesema.
Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kujua ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70) licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawena kuyasafirisha kwenye viwanda hapanchini na nje ya nchi.“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 namkauza zaidi ya hapo.
Mkaguzi wa hesabu anasema kampuni imepata, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Bw. Mlingi Mkucha.
Chanzo : EATV