Waziri mkuu Majaliwa akutana na ufisadi wa kutisha mgodi wa Ngaka, aagiza uchunguzi kufanyika.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,680
22,685
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya uzalishaji wa makaa ya mawe ya TANCOAL ni halali.

Waziri Mkuu akiangalia makaa ya mawe katika mgodi wa NgakaAmetoa kauli hiyo leo mchana mara baada baada ya kupokea taarfa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.


Waziri Mkuu amesema atamwagiza piamdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili apitie mahesabu ya kampuni tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” amesema.



Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kujua ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70) licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawena kuyasafirisha kwenye viwanda hapanchini na nje ya nchi.“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 namkauza zaidi ya hapo.



Mkaguzi wa hesabu anasema kampuni imepata, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Bw. Mlingi Mkucha.


Chanzo : EATV

20170106182436.jpeg
 
Mara rais halafu waziri mkuu, nauliza?, mawaziri na wakurugenzi wao hawaoni lolote baya hadi wakuu waende? Wawajibike ama tuamini haya yote kiinimacho cha wakubwa
 
kwa madudu haya watu bado mnaikumbuka serikali ya hawamu ya 4,,watanzania wajinga sana kwani kwa mtu mzalendo hakuna serikali ya kuichukia km ya hawamu ya 4
 
Sioni umuhimu wa kuwa na mawaziri, maana majukumu yao siyaoni.!
 
CDM ni mafisadi sana! Angalia mgodi huu nao wameufisadi tunahitaji uchunguzi haraka sana!!! Sirikali ya ccm hhaitakuwa na subra kwa hili! Tumechoka
 
Nilichogundua sasa hivi, wananchi hawavutiki tena na wimbo wa ufisadi naona kama wameshauchoka.
Ningekuwa ni mimi ningetafuta kick nyengine
Maana hata kama kutakuwa na hatia utasikia ni kusimamishwa kazi tu
 
kwa madudu haya watu bado mnaikumbuka serikali ya hawamu ya 4,,watanzania wajinga sana kwani kwa mtu mzalendo hakuna serikali ya kuichukia km ya hawamu ya 4
Ili kuichukia sana serikali ya awamu ya nne hatuna budi kuyakumbuka "madudu" haya. Raisi wa sasa alikuwepo madudu haya yakifanyika na mengi tunayaita majipu aliyafahamu. Swali: Kwa nini hakujitenga nayo.

Anayejifanya kupambana na ufisadi sasa alikuwepo bungeni kwa awamu zaidi ya tatu. Wakati upinzani (unaodaiwa "kutetea" ufisadi) ulipokuwa ukipambana sana na ufisadi huyu mpambanaji mkali wa leo alikuwa mpole/mwoga/mnafiki; au sijui alijuwaje. Kama nasema uwongo mdau mmoja atupie hapa hata kaclip ka audio kanakothibitisha kuwa huyu jamaa aliwahi kuwa mpambanaji.

Serikali ya awamu ya 4 ilikuwa na madudu yake yasiyomithilika, na vivyo hivyo serikali ya awamu ya 5.

Tulimvumilia wa awamu ya nne. Tutamvumilia wa awamu ya tano.
 
Huo mgodi wa mbinga- Ruvuma ndo unaitwa mgodi wa Ngaka??… hata hivyo ningefurahi kama mh. angesema neno juu ya barabara na huduma nyingine za kijamii ambazo wananchi wanatakiwa wafaidike kutokana na mgodi huo kwani hali ya barabara tu ni mbaya mno!
 
Awamu hii ufisadi unaibuliwa na CCM wenyewe tofauti na awamu iliyopita ambapo kelele hizi zilihodhiwa na upinzani.

Ni Tanzania pekee kwa Afrika nzima ambapo ufisadi haujazungumza na upinzani kwenye uchaguzi ilhali ufisadi upo.

Funny!!,
 
Waziri mwenye dhamana vipi yuko likizo?

Mwisho wa siku lazima tukubali kuwa nchi yetu bado shamba la bibi na cha msingi ni kuongozwa na katiba imara sio utashi wa watu. What if yeye Majaliwa asingeenda leo? Tungeendelea kuliwa? Magufuli jenga taasisi imara mzee utuachie kitu cha kukumbukwa
 
Back
Top Bottom