Waziri mkuu Majaliwa akutana na ufisadi wa kutisha mgodi wa Ngaka, aagiza uchunguzi kufanyika.

Awamu hii ufisadi unaibuliwa na CCM wenyewe tofauti na awamu iliyopita ambapo kelele hizi zilihodhiwa na upinzani.

Ni Tanzania pekee kwa Afrika nzima ambapo ufisadi haujazungumza na upinzani kwenye uchaguzi ilhali ufisadi upo.

Funny!!,
Sasa watazungumzia wapi wakati hata mikutano ya ndani hairuhusiwi? Na hawa wako madarakani mwaka mzima walikuwa hawajashtuka tu na vyombo walivyonavyo? Bila taasisi imara tunajisumbua
 
Sasa watazungumzia wapi wakati hata mikutano ya ndani hairuhusiwi? Na hawa wako madarakani mwaka mzima walikuwa hawajashtuka tu na vyombo walivyonavyo? Bila taasisi imara tunajisumbua

Wakati wa kampeni hapakuwepo sehemu ya kusemea?

Mbona hata sasa kuna tamko la Mbowe juu ya hotuba ya rais Kagera,Mbowe kazungumzia wapi?

Suala la Saanane Lisu alizumgumzia wapi?
 
Wewe
Waziri mtaasisi. hamana vipi yuko likizo?

Mwisho wa siku lazima tukubali kuwa nchi yetu bado shamba la bibi na cha msingi ni kuongozwa na katiba imara sio utashi wa watu. What if yeye Majaliwa asingeenda leo? Tungeendelea kuliwa? Magufuli jenga taasisi imara mzee utuachie kitu cha kukumbukwa
Wewe unaelewa maana ya taasisi au umekalilishwa tu. Rais mwenyewe ni taasisi. Akiwa corrupt na mvivu wa kufuatilia ndo nchi inaharibika. Lowasa ni fisadi unafikili taasisi ya urais ingekuwaje zaidi ya system nzima kuanzia huu mpaka chini kuharibika. Rais akiwa imara hata chini watafuta tu whether siquencially or simultaneously
 
Ili kuichukia sana serikali ya awamu ya nne hatuna budi kuyakumbuka "madudu" haya. Raisi wa sasa alikuwepo madudu haya yakifanyika na mengi tunayaita majipu aliyafahamu. Swali: Kwa nini hakujitenga nayo.

Anayejifanya kupambana na ufisadi sasa alikuwepo bungeni kwa awamu zaidi ya tatu. Wakati upinzani (unaodaiwa "kutetea" ufisadi) ulipokuwa ukipambana sana na ufisadi huyu mpambanaji mkali wa leo alikuwa mpole/mwoga/mnafiki; au sijui alijuwaje. Kama nasema uwongo mdau mmoja atupie hapa hata kaclip ka audio kanakothibitisha kuwa huyu jamaa aliwahi kuwa mpambanaji.

Serikali ya awamu ya 4 ilikuwa na madudu yake yasiyomithilika, na vivyo hivyo serikali ya awamu ya 5.

Tulimvumilia wa awamu ya nne. Tutamvumilia wa awamu ya tano.

Salute mkuu,

Siku zote mkweli na mtu asiyependa unafiki honekana mapema.

Huyu wanayemuita mtetezi wa wanyonge( ingawa mpaka sasa hajaonyesha kama kweli anaguswa na wanyonge) alikuwepo wakati wa yale madudu hakufunua mdomo kukemea achilia mbali kujiuzulu na kujitenga nao.

Turejee mfano wa deo filikunjombe alivyokuwa anapambana na serikali yake kulinda maslahi ya nchi.

Deo alikuwa hana hata chembe ya unafiki kama hawa wengine mnaowasifu kila siku wakati hao hao wanakashfa kibao walizoshiriki serikali iliyopita.

Viongozi hawa waliopo hawachukii ufisadi na kama wangekuwa wanachuchukia ile mahakama ya mafisadi isinge pumu.

Hivi unaanzaje kukosa kesi wakati huohuo wafuatao wapo mtaani

Lowassa

Prof Tibaijuka

Andrew chenge

Mkulu mwenyewe muuza nyumba zile za

Wabunge wa ccm na ccm kwa ujumla kuhusu zile 10m za kupitisha mswaada wa habari according to mbowe press

Nakataa leo nitakataa kesho nitakaa siku zote Viongozi waliopo hawachukii ufisadi huenda wao ndo wanajitengenezea njia ya kupiga zaidi
 
Awamu hii ufisadi unaibuliwa na CCM wenyewe tofauti na awamu iliyopita ambapo kelele hizi zilihodhiwa na upinzani.

Ni Tanzania pekee kwa Afrika nzima ambapo ufisadi haujazungumza na upinzani kwenye uchaguzi ilhali ufisadi upo.

Funny!!,
Mkuu upo sahihi kilichobaki kwa wapinzani ni kuwa watetezi wakuu wa ufisadi na mafisadi mwenyewe

..natamani kuona watu wenye mtazamo chanya wa mustakabali wa nchi yetu na si watetezi wa mafisadi Kama wafanyavyo upinzani kwa sasa.
 
Wakati wa kampeni hapakuwepo sehemu ya kusemea?

Mbona hata sasa kuna tamko la Mbowe juu ya hotuba ya rais Kagera,Mbowe kazungumzia wapi?

Suala la Saanane Lisu alizumgumzia wapi?
Kama nilivyo koment hapo awali sasahivi wapinzani wamegeuka watetezi wakuu ufisadi nchini
 
Muongo si alikuwa huko last month alipoenda na wazalishaji wa saruji. Maana yake hakuyaona haya yote
 
ngoja kwanza faru john kaishia wapi hatutaki mambo nusu nusu tupewe mrejesho wa faru john na nani mhusika hizi story za kuibua ufisadi afu zinaishia hewani mwisho 2016
 
Waziri mwenye dhamana vipi yuko likizo?

Mwisho wa siku lazima tukubali kuwa nchi yetu bado shamba la bibi na cha msingi ni kuongozwa na katiba imara sio utashi wa watu. What if yeye Majaliwa asingeenda leo? Tungeendelea kuliwa? Magufuli jenga taasisi imara mzee utuachie kitu cha kukumbukwa
Ha ha alienda wakati wa mgogoro wa wazalisha saruji walipotiwa ban ya kuingiza makaa ya mawe to nje ya nchi. Nadhani hakuyaona haya. Pili nimejua serikali ina hisa katika mgodi huo 30% ndo maana wali ban importation ili angalau nao wapate gawio la pesa
 
Hii awamu ni two man show. bila wao kufika maeneo ya matukio husikii tuhuma. aidha tatizo lingine ni ufuatiliaji wa wayaagizayo, soko mwanjelwa, faru john, uvaaji vitambulisho, usafi jumamosi nk.
 
kwa madudu haya watu bado mnaikumbuka serikali ya hawamu ya 4,,watanzania wajinga sana kwani kwa mtu mzalendo hakuna serikali ya kuichukia km ya hawamu ya 4
Naungana nawe kwa 109% ,,kwa mtu aliyepevuka akili vzr na ana fikra chanya hawezi kuikumbuka serikali dhaifu dunian kwa wakat huo kama ile ya 4 ,,,ilikua ya hovyo kila sekta , ilikosa maamuzi, watu wanapokufa mafuriko dar Mjomba anacheka , uswahiba kila kona ,,, Nina uhakika kila anayeikumbuka ile gvt ana moja kati ya haya;
1.vyeti feki
2.Fisadi au jizi
3. Mnafiki
4.mkwepa kodi
5. Katumbuliwa kwa uzembe
6.kafilisika kwa kibano cha jpm
7.kakosa cheo.
Naamin kwa mtu ambaye anafanya kazi kwa kutumia taaluma halali hawez kilalamika kwamba serikali iliopo haifai .itakua haifai kwa wenye njia za mkato.
 
hiyo kesi itakufa kama zilivyokufa nyingine zilizopita....hii ni nchi ya matajiri tuuuu walalahoi tutaisoma namba.
 
Back
Top Bottom