Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Nimestaafu tangu mwezi June 2015 na hadi sasa bado sijalipwa mafao yangu.
Mwezi Novemba nilipokwenda makao makuu ya PSPF nikaambiwa mafao yangu yako tayari na jalada langu lilikuwa ofisi ya malipo kuandikiwa hundi lakini serikali ilikuwa haijawasilisha fedha inazodaiwa na mfuko huo.
Nilivuta subira hadi niliposikia tamko la Naibu Waziri wa fedha akiwapa siku saba PSPF kuwalipa wastaafu.
Juzi siku ya Ijumaa tarehe 15.01.2016 nikaenda tena PSPF makao Makuu ofisi ya malipo majira ya saa 4 asubuhi.
Nilijibiwa na mtumishi wa ofisi hiyo kijana wa kiume aliyekuwa zamu kuwa hundi yangu iko tayari isipokuwa hawawezi kunikabidhi hadi aje mwakilishi anayetambuliwa kutoka idara ya Polisi makao makuu ndiye atasaini kuchukua hundi hiyo.
Nilichapa mguu hadi makao makuu ya Polisi kitengo cha wastaafu na kumkuta Sgt David ambaye baada ya kumweleza mara moja akamtuma askari kufuatilia hundi hiyo.
Hata hivyo kabla ya kuchukua jukumu la kwenda makao makuu ya polisi niliomba kuonana na Meneja wa huduma kwa wateja lakini pia nilijibiwa yuko likizo na hakuna mbadala wake.
Kutokana na imani niliyokuwa nayo niliondoka kurejea nyumbani nikiamini mambo yako sawa.
Majira ya saa tisa alasiri nilimpigia simu Sgt David na kwa masikitiko makubwa akanieleza mafao yangu bado na lugha aliyotumia mtumishi wa PSPF ilikuwa ni njia ya kuniondoa tu.
Hayo ndiyo majanga ya mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma.
Nina imani mamlaka husika zitafuatilia utendaji wa taasisi hii ya umma kwani ule msoto wa wastaafu uliokuwepo miaka ya nyuma hadi watu kupiteza maisha bila kulipwa unerudi kwa kishindo.