Waziri Mkuu Azindua Kiwanda Cha Kuchakata Muhogo

Mwaume

Senior Member
Sep 10, 2014
114
52
Wakuu habari za jioni.
Leo tarehe 22 Machi 2019 kwenye taarifa ya habari ya saa kumi jioni nimemuona Waziri Mkuu akizindua kiwanda cha kuchakata muhogo.

Nafikiri hii ni fursa nzuri kwa wakulima wa zao hili kwa Mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani.

Nami sitaki fursa hii inipite hivyo naomba mwenye taarifa nzuri kuhusu kiwanda hiki anijuze pamoja nawengine wanao zihitaji, hasa taarifa za bei ya muhungo kwa ekari, upatikanaji wa mashamba, pembejeo, mbegu nk.

Natanguliza shukurani zangu za dhati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuelekea Tanzania Ya Viwanda chini ya Rais Magufuli hatimaye Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amefungua Kiwanda cha kuchakata Muhogo cha CASSAVA STARCH OF TANZANIA COMPANY LIMITED kilichopo katika kijiji cha Mbalala, jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Ujenzi wa kiwanda hicho umetokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa.

Juhudi hizi zitaongeza wigo wa Soko la Mihogo na pia Kuongeza thamani ya zao hilo ili liweze kuingia katika Soko la Dunia.

1553287749576.png
 
Bora tutaepukana na madalali wa Buguruni.

Vp na yale mahindi tulioingia mkataba na shirika la chakula mauzo yake yanaendeleaje jamani mwenye taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Crisps za mihogo balaa
Yaani sio wabunifu tu ila kila kitu kipo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kichwa cha habari kiwe Wakulima wa Muhogo Lindi, wapata Soko la Uhakika, halafu ndio ungeendelea na mengine.

Wakulima wa Muhogo Tanzania tulitangaziwa soko kubwa sana China 2018, jitihada za balozi wetu kule,Mchina kaja ananunua mhogo mbichi kilo moja shs 150. Baadae msimu huo huo wakabadilika wakasema hawataki mbichi, wananunua mkavu (makopa) kwa Tsh 280 mpaka 300/=. Matokeo yake mihogo iliyolimwa Nov 2017 bado iko shambani, sababu baadhi ya mbegu ambazo wakulima walilenga soko la mchina kutokana na kuhamasishwa na viongozi na watalaam, haziuziki masokoni. Na hao viongozi wako kimya na pia Tantrade.

Yaani bei ya kuchimba kuukatakata kama slesi ndogo ndogo kwa mikono ( kuchakata) na kukausha kwa kutumia jua. Na bado wanataka umpelekee kwenye godauni lake kwa gharama zako mwenyewe. Bei hiyo imeshindikana haina maslahi Hata eka 2 tu ni vigumu sana.

Labda mfaransa atakuja na gia nyingineSent using Jamii Forums mobile app
 
uhudi hizi zitaongeza wigo wa Soko la Mihogo na pia Kuongeza thamani ya zao hilo ili liweze kuingia katika Soko la Dunia.

Ungefafanua. Sentensi yako hii inayoonekana kuwa na mambo mawili:

Mosi, mhogo utachakatwa katika kiwanda hicho na kutengeneza 'starch'.

Pili, Hapo hapo unazungumzia "---- soko la mhogo na pia kuongeza thamani ya zao ili liweze kuingia katika soko la Dunia."

Hili linachanganya. Zao la mhogo litaingia katika soko la Dunia, au ni bidhaa inayotokana na mhogo (iliyoongezwa thamani) ndio itaingia katika soko la Dunia?

Kwa ufupi swali langu ni hili: je, China tutawauzia mhogo, au tutawauzia bidhaa (starch), inayotokana na mhogo; au yote mawili?
 
Kichwa cha habari kiwe Wakulima wa Muhogo Lindi, wapata Soko la Uhakika, halafu ndio ungeendelea na mengine.

Wakulima wa Muhogo Tanzania tulitangaziwa soko kubwa sana China 2018, jitihada za balozi wetu kule,Mchina kaja ananunua mhogo mbichi kilo moja shs 150. Baadae msimu huo huo wakabadilika wakasema hawataki mbichi, wananunua mkavu (makopa) kwa Tsh 280 mpaka 300/=. Matokeo yake mihogo iliyolimwa Nov 2017 bado iko shambani, sababu baadhi ya mbegu ambazo wakulima walilenga soko la mchina kutokana na kuhamasishwa na viongozi na watalaam, haziuziki masokoni. Na hao viongozi wako kimya na pia Tantrade.

Yaani bei ya kuchimba kuukatakata kama slesi ndogo ndogo kwa mikono ( kuchakata) na kukausha kwa kutumia jua. Na bado wanataka umpelekee kwenye godauni lake kwa gharama zako mwenyewe. Bei hiyo imeshindikana haina maslahi Hata eka 2 tu ni vigumu sana.

Labda mfaransa atakuja na gia nyingineSent using Jamii Forums mobile app

Hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa akili zetu zinafanya kazi namna gani.

Mchina anataka tulime mhogo, halafu tumuuzie mhogo huo yeye akatengeneze vitu vya thamani kwao. Kwani hawezi kujenga kiwanda hapa, nasi tukapata ajila za watu wetu, na akasafirisha mali iliyotengenezwa ikauzwe huko China?

Kwa nini iwe hivi kila mara? Wao watuuzie vya thamani kubwa, sisi tuwauzie vya thamani ndogo! Tukihitaji 'starch ya mhogo', tukaagize China, 'starch' ileile iliyotokana na mhogo wetu?

Hivyo viwanda vya kutengeneza wanga vina ugumu gani wa kuvijenga na kuviendesha hapa kwetu?

Na tunajigamba tunaandaa uchumi wa viwanda!
 
Wakati huo korosho zinaoza kwa kukosa wanunuzi
Kuelekea Tanzania Ya Viwanda chini ya Rais Magufuli hatimaye Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amefungua Kiwanda cha kuchakata Muhogo cha CASSAVA STARCH OF TANZANIA COMPANY LIMITED kilichopo katika kijiji cha Mbalala, jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Ujenzi wa kiwanda hicho umetokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa.

Juhudi hizi zitaongeza wigo wa Soko la Mihogo na pia Kuongeza thamani ya zao hilo ili liweze kuingia katika Soko la Dunia.

View attachment 1051625
FB_IMG_1550766064153.jpeg

In God we trust
 
Akikujibu nitag, nakula chips dume (muhogo wa kukaanga) hapa nishushie na maji siku iende...
Ungefafanua. Sentensi yako hii inayoonekana kuwa na mambo mawili:

Mosi, mhogo utachakatwa katika kiwanda hicho na kutengeneza 'starch'.

Pili, Hapo hapo unazungumzia "---- soko la mhogo na pia kuongeza thamani ya zao ili liweze kuingia katika soko la Dunia."

Hili linachanganya. Zao la mhogo litaingia katika soko la Dunia, au ni bidhaa inayotokana na mhogo (iliyoongezwa thamani) ndio itaingia katika soko la Dunia?

Kwa ufupi swali langu ni hili: je, China tutawauzia mhogo, au tutawauzia bidhaa (starch), inayotokana na mhogo; au yote mawili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaamini kuwa Serikali ina habari kuwa katika miaka 1980 Serikali ilijenga kiwanda cha kutengeneza wanga inayotokana na mihogo eneo la Katunguru Mkoa wa Mwanza. Majengo yapo, ofisi zipo na mashine zipo japo labda sasa hivi zimepitwa na technologia. Ni ushauri kwa Serikali kufufua kiwanda hiki ambacho hakitakuwa na gharama kubwa na kuwezesha wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuhamasishwa kulima muhogo na kujiatia kipato.
 
Back
Top Bottom