Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi mradi wa maji wa miji 28 Katavi

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
261
Reaction score
199
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KATAVI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 13, 2026 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 22.8 umefikia asilimia 55 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Julai 2026. Kukamilika kwake kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.

Baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Dkt. Mwigulu amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya maji.

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha takribani lita milioni 12 za maji kwa siku.

 

Attachments

  • IMG-20260313-WA0194.jpg
    395.4 KB · Views: 2
  • IMG-20260313-WA0184.jpg
    270.3 KB · Views: 5
  • IMG-20260313-WA0190.jpg
    421.7 KB · Views: 3
Namuona mzee kimanta mwenyekiti wa CCM mkoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…