Waziri Mkuu apokea taarifa ya nyongeza ya mishahara, kuiwasilisha kwa Rais ambaye ataitangaza hivi karibuni

Hii...ni taarifa mbichi kwa wafanyakazi,taarfa ambayo imekaa kisiasa.

Taarfa iliyoiva haiwezi kuwa ya namna hii.hii taarfa haina Tofauti na ile ya utatuzi wa ongezeko la bei ya mafuta.

Hapa ni Siasa, siasa! siasa!!
Lengo ni kuzima mvumo wa mikutano ya Chadema unaondelea. MaCCM yanawaza UBAYA tu.
 
yaani tunazungushanaaaaa mara jambo lenu lipo, ooh hesabu zinaendelea, oooh kikao kinafanyika, mara oooh waziri mkuu kapokea hesabu, tena ooh katelefoni atamkabidhi Sam mapendekezo, ooh Sam atawatangazia yaani kama pasi za NETBALL....... wasi wasi tu mwanzo mwisho
Mwana wanatuonyesha Pasi za Kiman U utafikili kuna kombe tunagombania kumbe mshahara ni haki yetu na madaraja ni haki yetu, na Elimu ilikua gharama ya wazazi wetu..hawa jamaa pasua kichwaa sana.!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA NYONGEZA YA MISHAHARA

*Aahidi kuikabidhi kwa Mheshimiwa Rais Samia wakati wowote

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo leo usiku (Jumanne, Mei 10, 2022) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kiliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Jumapili Mei Mosi 2022 aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA

JUMANNE, MEI 10, 2022.
wananchi wenzangu tulieni mbona siku zitafika tuu kama ukweli utajulikana acheni kupiga ramli
 
WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA NYONGEZA YA MISHAHARA

*Aahidi kuikabidhi kwa Mheshimiwa Rais Samia wakati wowote
Samahani naomba kuuliza,. Waziri Mkuu anatakiwa kisheria kukabidhi hiyo ripoti kwa rais au mpaka waziri mkuu apende
 
Samahani naomba kuuliza,. Waziri Mkuu anatakiwa kisheria kukabidhi hiyo ripoti kwa rais au mpaka waziri mkuu apende
Tangu awamu ya tano ya utawala sheria kuhusu mishahara/maslahi ya mtumishi zilipigwa teke. We elewa kwamba waziri ameahidi kuikabidhi
 
Kazi kweli kweli!
Kumbe hakuna kilichokuwa kimefanyika? Tulitegemea kuwa tayari iko kwenye bajeti ya 2022/2023 kumbe ndiyo kwanza mapendekezo yanapelekwa kwa Rais?
Wabongo kwa kupenda kujifanya mnajua.sasa bajeti ya 22/23 si inaanza Julai 1 sasa mpaka hapa serikali ilichochelewesha ni nini?
 
Back
Top Bottom