Waziri Mkuu anapotoa majibu mapesi kwa maswali mazito!: Ni uwezo or just saving faces?!..

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Nafuatilia Bunge Live kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Nimesikiliza maswali magumu mazito ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe na majibu rahisi na mapesi ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

This leaves much to be desired kuhusu uwezo wa Waziri Mkuu wetu kujibu maswali magumu mazito kwa kutoa majibu rahisi na mapesi.

Maswali yamehusu
1. Sintofahamu ya hali ya usalama
2.Kupotea Kwa Ben Saanane 6 months bila taarifa, tuwaite Scotland Yard Watusaidie?.
3. The right to information ya Bunge Live.

Majibu.
1. Hali ni shwari na vyombo vya ulinzi na usalama viko makini kwenye hili, muhimu ni kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kunapotokea Sintofahamu yoyote.

2. Kuhusu Ben Saanane amesema ametangulia mbele ya haki, kisha akasema uchunguzi unaendelea kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na Uchunguzi hauna time frame. Tanzania inashirikia na vyombo vya nje ikiwemo Scotland Yard ila vyombo vya ndani vina uwezo, tuviaminie. Uchunguzi ukikamilika, taarifa itatolewa. Kama neno ametangulia mbele ya haki lilitangulia, kwa uchunguzi unaoendelea na Scotland Yard hawahitajiki, then isn't this a known thing?!. Kwa vile tayari TISS imeisha tuhumiwa tena Bungeni na wabunge wa CCM kuhusika na utekaji, hivi kweli kuna chombo cha ndani kinaweza kuchuichunguza TISS kwa kuzingatia mada kuu ya Ben iliyompotezesha?!. Nilidhani kuepuka chombo kuwa hakimu wa kesi yake yenyewe (Nemo judex in causa sua), na miezi 6 for doing nothing, hapa tulihitaji usaidizi!.

3. Bunge Live: Bunge liliisha amua namna ya kutoa habari zake kwa umma.

Waziri Mkuu anapotoa majibu mapesi kwa maswali magumu na majibu rahisi kwa maswali mazito kuhusu hali ya usalama wa raia: Jee ni uwezo mdogo wa kujibu maswali magumu kwa majibu rahisi au ni majibu ya makusudi tuu just for saving faces ya kuilinda serikali pale ambapo serikali haina majibu ya maswali hayo?. Mfano kwenye issue ya Bunge Live, up to now is there any justified reasons ever given why Bunge is not live throughout kama zamani?. Japo sababu ziliwahi kutolewa kule nyuma kuwa it's too costly, is this a justified reasons?, kwa kuzingatia kuna mtu baki who has nothing to do with Bunge alisikika akisema "ndio maana nilizuia Bunge Live"!.
RASMI: BUNGE SASA NI IDARA YA IKULU
Amewathibithibitishia mbele ya Spika Ndugai kuwa yeye ndiye aliyezuia BUNGE LIVE kwa kuwa anakerwa na jinsi wapinzani walivyokuwa wakipata umaarufu kupitia Bunge live.
Je, hapo tuna BUNGE au IDARA YA IKULU?
Japo sijafanikiwa kuiona video clip akiyasema haya asije kuwa kasingiziwa tuu maana media zetu kwa kuwalisha watu maneno, hazijambo!.

Kama ni kweli aliyasema hayo na ni kweli ni yeye ndie aliyezuia Bunge Live na sababu ndizo hizo, then this is not right! . Huku ni Mkuu wa Executive kuingilia mamlaka ya The Legislature hivyo kukiuka kanuni ya "The Independent of the Parliament" ndani ya "The Separation of Powers"!.

Mhe. Mbowe alishindwa kuliframe vizuri hili swali la Bunge Live ili kuthibitisha the independence of Legislature imeingiliwa na the Executive!.

Kitu kizuri kuhusu majibu ya Waziri Mkuu kilichonifurahisha ni jinsi alivyo humble, simple na down to earth kwa kujibu kwa unyenyekevu mkubwa na kuonyesha heshima kwa KUB.

My Take.

1. Kwanza Wabunge wetu wapewe semina ya jinsi ya kuuliza maswali na sio kutoa hutuba. Beating around the bush for too long kunapunguza strength ya swali.

2. Kwa vile sessions zote za Maswali ya Papo kwa Papo huanza na swali toka kwa KUB, then kabla ya session hii KUB afanye tete a tete meeting na some few good questions formulators kwenye kambi yao watamsaidia ku frame hard straight questions with facts, yasiyokubali majibu rahisi rahisi.
3. Viongozi wafunze kutoa majibu sahihi ya maswali with straight answers packed with facts sio nao kutoa maelezo marefu na wao pia kuhutubia bila concise answers!.

4. Kwa vile hii ya maswali ya papo kwa papo tumeiga Bunge la Westminster, then wabunge wetu haswa wa upinzani wawe facilitated kuhudhuria hizi sessions za mabunge kama yale, kipindi hiki ni grilling kwa PM anakuwa grilled kweli kweli sio huku anaulizwa kama anabembelezwa au anaombwa kujibu!.
,
5. Na mwisho ni pongezi pia kwa Spika Ndugai kwa uvumilivu wa kuvumilia maelezo mareefu ya wabunge, enzi za Speed and Standards (RIP), there was no room ya hii dilly darling kama hii, wengine maswali waliyaandika na kuuliza ili tuu kuonyesha uwepo wao bungeni. This is very healthy kwa Spika Ndugai is changing for the better,
Ndugai huyu tuliyemzungumza hapa, sio Ndugai huyu wa leo!.
Vurugu za Jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.

Naibu Spika Mhe. Dr.Tulia Akson has to learn from this man, kwa sababu ile last session ya maswali ya papo kwa papo Dr.Tulia aliyoiendesha, was disastrous hadi tukapendekeza
Napendekeza Bunge Lianzishe Maswali Kwa Spika, Ili Maswali Kwa Waziri Mkuu Yabaki
Kwa mwendo huu, kiukweli kazi bado tunayo na safari bado ni ndefu. Jee tutafika? .

Wasalaam
Alhamisi Njema.
Paskali
 
Mayalla Paskali, uliuliza swali zuri sana JPM, that was a very technical question worthy of your respect, knowledge, credibility! Leo nimekujibu ile ya TISS, umeniumiza sana na options za benefit of doubts!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mbona inaeleweka kuwa Waziri Mkuu maswali ya papo kwa hapo hayawezi hana tofauti na Mwijage waziri wa viwanda kwenye kujibu maswali sifa wanayoitaka ni kuitwa kiongozi Makini tu..
 
Shemeji,ukiona kitumbua chako kunamtu anataka kukidondosha kwenye mchanga lazima ukifunge vizuri.Maswali aliyoulizwa ni sawa na kupiga sahani yenye kitumbua,lazima aikamate vilivyo!

Majibu yote hamna kitu
 
Hata Kasimu anaumizwa sana na uWaziri Mkuu wa Bashite,kwa hiyo maswali mengi yanajibiwa katika hali ya msongo wa mawazo. Hakuna namna tusubiri mpaka 2020 au kuchore mstari
Think tank ya CDM, jaribu kuwa critical na fikiri kabla ya kuandika OKW BOBAN SUNZU. Ndio maana threads zako za zamani zina sintofahamu nyingi, unakosa credibility. Bashite ameingiaje hapo kwenye maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu?
 
Wanabodi,

Nafuatilia Bunge Live kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Nimesikiliza maswali magumu mazito ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe na majibu rahisi na mapesi ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

This leaves much to be desired kuhusu uwezo wa Waziri Mkuu wetu kujibu maswali magumu mazito kwa kutoa majibu rahisi na mapesi.

Maswali yamehusu
1. Sintofahamu ya hali ya usalama
2.Kupotea Kwa Ben Saanane 6 months bila taarifa, tuwaite Scotland Yard Watusaidie?.
3. The right to information ya Bunge Live.

Majibu.
1. Hali ni shwari na vyombo vya ulinzi na usalama viko makini kwenye hili, muhimu ni kwa wananchi wote kutoa ushirikiano kunapotokea Sintofahamu yoyote.

2. Uchunguzi unaendelea kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na Uchunguzi hauna time frame. Tanzania inashirikia na vyombo vya nje ikiwemo Scotland Yard ila vyombo vya ndani vina uwezo, tuviaminie. Uchunguzi ukikamilika, taarifa itatolewa.

3. Bunge Live: Bunge liliisha amua namna ya kutoa habari zake kwa umma.

Waziri Mkuu anapotoa majibu mapesi kwa maswali magumu na majibu rahisi kwa maswali mazito kuhusu hali ya usalama wa raia: Jee ni uwezo mdogo wa kujibu maswali magumu kwa majibu rahisi au ni majibu ya makusudi tuu just for saving faces ya kuilinda serikali pale ambapo serikali haina majibu yards maswali hayo?.

Kitu kizuri kuhusu majibu ya Waziri Mkuu kilichonifurahisha ni jinsi alivyo humble, simple na down to earth kwa kujibu kwa unyenyekevu mkubwa na kuonyesha heshima kwa KUB.

My Take.

1. Kwanza Wabunge wetu wapewe semina ya jinsi ya kuuliza maswali na sio kutoa hutuba. Beating around the bush for too long kunapunguza strength ya swali.
2. Viongozi wafunze kutoe majibu sahihi ya maswali na sio nao kutoa maelezo marefu na wao pia kuhutubia bila concise answers!.
,
Pongezi pia kwa Spika Ndugai kwa uvumilivu wa kuvumilia maelezo mareefu ya wabunge, enzi za Speed and Standards (RIP), there was no room ya hii dilly darling kama hii, wengine maswali waliyaandika na kuuliza ili tuu kuonyesha uwepo wao bungeni.

Kwa mwendo huu, kiukweli kazi bado tunayo na safari bado ni ndefu. Jee tutafika? .

Wasalaam
Alhamisi Njema.
Paskali
Paskali, maswali yaliyoulizwa mbona yanalegalega kwenye mizani. Mfano swali la Ben Saanane siyo swali la kumuuliza Waziri Mkuu. Ni kweli Ben saanane, kama raia wengine anahaki ya kutafutwa iwapo atapotea ila si wa kuitafutwa kwa Scotland yard. Hii ni kwa sababu Chadema wenyewe walishatangazia umma kuwa Ben kaamua kujificha ili atafute umaarufu. Kwa hiyo mjadala wa Ben ni kama waliufunga wao wenyewe. Hata hilo swali la Bunge live si jipya, ni jambo ambalo lilishatolewa majibu mara kwa mara. Hivyo halikustahili kuwa miongoni mwa maswali yanayopaswa kuulizwa waziri mkuu. Binafsi naona aidha spika amestahi Mbowe au spika hakuwa makini kusikiliza maswali yaliyoulizwa.
 
Mayalla jifunze kuwa grea thinker. Jiondoe kwenye kikundi cha kulalamika sasa tujielekeze kwny ujenzi wa hoja
 
Angetokea mtu aulize kwa waziri mkuu kwa nini KUB anaendelea kushika wadhifa wake despite tuhuma nzito za kukwepa kodi na kujihusisha na ngada basi ningeona bunge liko serious
 
Paskali, maswali yaliyoulizwa mbona yanalegalega kwenye mizani. Mfano swali la Ben Saanane siyo swali la kumuuliza Waziri Mkuu. Ni kweli Ben saanane, kama raia wengine anahaki ya kutafutwa iwapo atapotea ila si wa kuitafutwa kwa Scotland yard. Hii ni kwa sababu Chadema wenyewe walishatangazia umma kuwa Ben kaamua kujificha ili atafute umaarufu. Kwa hiyo mjadala wa Ben ni kama waliufunga wao wenyewe. Hata hilo swali la Bunge live si jipya, ni jambo ambalo lilishatolewa majibu mara kwa mara. Hivyo halikustahili kuwa miongoni mwa maswali yanayopaswa kuulizwa waziri mkuu. Binafsi naona aidha spika amestahi Mbowe au spika hakuwa makini kusikiliza maswali yaliyoulizwa.
Kupotea kwa Ben Saanane hakuwezi kumalizwa na tamko la cdm. Ni jukumu la serikali kuchunguza. Hivi wewe mtoto wako akipotea na ukasema amejificha, serikali iridhike? Hapana.
 
Mawaziri wengi ndiyo hovyo sana afadhari ya PM, hata kama majibu yake hayajitoshelezi lakini anaonesha kujali napenda sana mtu akiwa humble.
Sasa wale wengine sijui mawaziri wako very rude sijui kiburi na majivuno!
Wanawajibu wabunge wanaouliza maswali muhimu na ya msingi hovyo hovyo sana ukiwaskia hadi hasira yani ndiyo maana kuna mabunge huko watu wanachapana makonde humo ndani sababu tu ya upuuzi usovumilika.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu Paskalli inaonekana una taarifa za kutosha juu ya majibu yaliyotakiwa kutokana na maswali yale.
Ebu tupe majibu mazito aliyotakiwa kutoa Mh. Waziri Mkuu (maana wewe umeandika ametoa mepesi) ili ukate mzizi wa fitina kama upo!
 
Bunge kwa sasa linaendeshwa kwa maelekezo kutoka Ikulu.Hili swala la Waziri Mkuu kutoa majibu mepesi mepesi kwenye hoja nzito kama hizo zimetolewa ni dalili tosha kwamba kuna jambo halipo sawa.
 
Back
Top Bottom