Waziri Mkuu ananishangaza sana

salisalum

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
418
136
Waziri wa Ujenzi Dr. Magufuli katia X nyumba zote zilizoko kwenye hifadhi ya barabara na kaagiza Tanroads wavunje bila kuangalia makunyanzi kupisha ujenzi wa barabara.

Waziri mkuu akiwa kwenye jimbo la Magufuli tena baadaye akamtembelea mama yake, alimwagiza asitishe bomoa bomoa mpaka bunge lijadili. Sielewi maana yake nini. Je, bunge litabadili hiyo sheria ya barabara? Magufuli ndiye aliyemwomba Pinda apindue maamuzi yake? Hii ni dharau au waliteta kwanza wakakubaliana atangue tena kwenye hadhara? Kama Magufuli hata react tumweleweje? Asiporeact haitaonyesha kwamba ni kiongozi dhaifu ambaye hutafuta kila nafasi kutafuta umaarufu uchwara? Hii maana yake nini?

Serikali ambayo kila waziri ana lake. Hakuna harmony hata kidogo.
 
Prime haaminiki tena, sheria ziko wazi sasa yeye anapinga waziri wake asitimize sheria?! tuna shida kubwa ya WAZIRI MKUU hapa...
 
Pinda amepinda, nafikiri hajaenda kwa babu kunywa dawa sasa wadudu wameshachanganya ndiyo maana anaropoka.Haikutegemewa kwa WM kumponda waziri wake nakumtaka aache kusimamia sheria tena mbele ya wapiga kura wake, huu ni wenda wazimu kabisa.
 
mmh! Huyu mh. Atakuwa ana ajenda binafsi, mh magufuli alikuwa sahihi na anafata taratibu za kazi, mh yeye anafata siasa. Mimi sina iman na utendaji wa PM, yupo kisiasa zaidi.
 
CCM imechoka ipumzisheni otherwise mtaona mengi sana ambayo hamkutaraji. Mimi i am sick and tired with two people in this country:
1. JK
2. Pinda
They are root causes of all these problems.
harafu sasa hata siku mia hazijapita wameanza kujiandaa na 2015, kweli kuna kutekeleza ahadi hapo? mpaka leo ni bajaj tu ambazo kwanza ni wazo finyu kumpakia mama mjamzito kwenye bajaj, si utaishia kumdondosha na kusababusha maafa makubwa.
 
Amepinda kabisa huyu mzee, wakati tunalalamikia foleni yeye anazuia nyumba zilizojengwa holela zisibomolewe duh heri Lowassa
 
CCM ni pure wasanii. Wakati wa kampeni JK alijinadi kwa slogani ya:-
"NGUVU ZAIDI, ARI ZAIDI NA KASI ZAIDI" Magufuli kwa Ari zaidi anatekeleza majukumu yake kwa Kasi zaidi na kusimamia Sheria kwa Nguvu zaidi, lakini Pinda anasema kasi ya Magufuli ni kubwa zaidi hivyo anamfunga speed gavana ili waende mwendo wa kobe!

Huu usanii wa Pinda na bosi wake unaharibu nchi! Magufuli toka huko hapakufai, wanakudhalilisha bure! Jiunge na CHADEAMA ili kasi yako ijenge nchi. Pinda HAFAI kuwa kiongozi wanchi sembuse WAZIRI MKUU, aende akalime.
 
siasa ni headache jamani ndio maana watu wanauwana kwa sababu ya siasa,siasa ni kama jinamizi fulani hivi likikukaba halikuwachi,umaarufu wa magufuli ulimfunika hata Mkapa sembuse Mkwere na Pindapindua????? wote wamepinda kabisa wanaona kasi ya mwenzao ni kubwa lakini wananchi ndio tunaelewa nani mtendaji na ni nani msanii...dhambi ya watanzania wa CCM ya kuwaingiza ikulu inawatafuna wenyewe.
 
Back
Top Bottom