Waziri Mkuu ataja vipaumbele sita

Waziri Mkuu ataja vipaumbele sita

kiraremapojoni

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2018
Posts
391
Reaction score
514
Waziri Mkuu Kassim MAjaliwa jana aliwasilisha bungeni bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 akitaja vipaumbele sita huku akiliomba Bunge limuidhinishie shs 272.9 Billion

Majaliwa alieleza kuwa ofisi yake pamoja na mambo mengine itatekeleza mambo makuu sita ikiwemo kuielekeza mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujenga uhusiano rafiki na walipa kodi

April Mosi, Rais John Magufuli akimwapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi (Sera),Adolph Ndunguru nasafiri Mbibo kuwa naibu kamishna mkuu wa TRA, aliishukia mamlaka hiyo akiitaka kufanya kazi kwa weledi na wafanyabishara huku akisema baadhi yao wamekuwa wakikimbilia upande wa pili wa nchi jirani kufanya biashara

Jana akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake na ofisi ya Bunge, Wasiri Mkuu Majaliwa alisema serikali itaendelea kuonyesha uthubutu tu na dhamira kuhakikisha inatekeleza mambo mbalimbali

"Kuielekeza TRA kujenga mahusiaano rafiki na walipa kodi kwa lengo la kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa walipa kodi kwa taasisi hiyo inatumia nguvu na vitisho kudai na kwa sababu na vitisho kudai kodi na kwa sababu hiyo kuzorotesha ukusanyaji wa mapato" alieleza

Mbali na suala la TRA, aliyataja mambo mengine kuwa ni pamoja na kuendelea kupambana na rushwa, ufisadi na uvivu sambamba na kuimarisha nidhamu kwa viongozi na watendaji wa ngazi zote katika kuwahudumia wananchi.

Alisema wataendelea kusisitiza kwa viongozi, watendaji na wananchi kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, ubunifu na uzalendo katika kujiletea maendeleao" Wafanyabiashara na wajasiriamali kuendesha biashara zao kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo na kujenga tabia ya kuoona fahari ya kulipa kodi kwa maendeleao ya taifa letu" alisema.mengine ni kujenga mazingira mazuri na wezeshi ya kufanya kazi, biashara, kilimo na shuguli nyengine za kiuchumi kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujiongezea kipato.

Alisema watawahimiza wananchi kutumia ipasavyo haki ya kidemokrasia kwakujiandikisha nakushiriki katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa utakaofanyika Octoba mwaka huu, Akizungumza kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019, Majaliwa alisema kuanzishwa kwa mfuko wa pensheni wa Mashirika ya Umma (PSSSF) umewezesha kulipwa kwa madeni yote ya wastaafu wa pspf wa mwaka 2017/2018 na wapatao 9,971 yanayofikia shs 888.39 Billioni

kwa upande wa ajira, alisema hadi kufikia februari. mwaka huu ajira221,807 zimezalishwa nchini. Kati ya ajira hizo, 146,414 na asilimia 66 zimetokana na utekelezaji wa miradi ya umma ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanja vya ndege, reli ya kisasa, miundombinu ya barabara na maji. Alisema ajira75,393 zilitokana na uwekezaji binafsi

SOURCE MWANACHI TAREHE 05.04.2019 PAGE 04

MAONI NA MAWAZO
 
Back
Top Bottom