Midas Touch
Senior Member
- Jan 23, 2008
- 188
- 200
Raia wema wa nchi yoyote duniani wanahitaji na ni haki yao kujua nini kinachofanywa na serikali yao kwa ajili yao lini na ni wakati gani jambo gani linatarajwa kufanyika.Hivi karibuni, Waziri wa Ujenzi Mh. Mbarawa alitoa hotuba yake ya bajeti kwa mwaka 2017/18 bungeni na ikapitishwa na bunge tukufu.
Katika hiyo bajeti kwa mwaka 2017/18, ibara ya 66 inahusu ujenzi wa barabara ya KIMARA hadi KIBAHA kwamba umesitishwa kwa sasa na utafanyika katika awamu ya pili ya Mradi Dar es salaam Maritime Gateaway. Hii inamaanisha kuwa ujenzi wa barabara ya KIMARA KIBAHA haupo kwa sasa hadi hapo baadaye.
CHAKUSHANGAZA: Baada ya hotuba ya waziri kupita bungezi pamoja na kuwekwa kwenye mtandao wa zizara {http://www.mwtc.go.tz/uploads/publications/en1493281737-HOTUBA WUUM 2017-2018.pdf} kesho yake TANROAD walipita katika maeneo ya KIMARA na kuweka alama za BOMOA pamoja na kutoa notice ya mwezi mmoja kwa kubomoa maeneo ya makazi na biashara. SOMA HAPA CHINI:
Posted On: Thursday 27, April 2017
HOTUBA YA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO KWA MWAKA WA FEDHA 2017-2018 YAWASILISHWA BUNGENI
http://www.mwtc.go.tz/uploads/publications/en1493281737-HOTUBA WUUM 2017-2018.pdf
HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MHESHIMIWA PROF. MAKAME M. MBARAWA (MB),
AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA
WA FEDHA 2017/2018 A.
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuweka mezani Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
66. MHESHIMIWA SPIKA, MRADI WA BARABARA YA KIMARA – KIBAHA (KM 25.7) UNAHUSISHA UPANUZI WA BARABARA HII KUWA NJIA SITA IKIJUMUISHA UPANUZI WA MADARAJA YA KIBAMBA, KILUVYA NA MPIJI. HADI MACHI, 2017 TARATIBU ZA KUMPATA MHANDISI MSHAURI KWA AJILI YA KUFANYA UPEMBUZI YAKINIFU NA USANIFU WA KINA WA MRADI HUU ZIMESITISHWA KWA KUWA UTAJUMUISHWA KWENYE AWAMU YA PILI YA MRADI WA DAR ES SALAAM MARITIME GATEWAY CHINI YA UFADHILI WA BENKI YA DUNIA.
NOTISI YA TANROADS
MY TAKE:
1. Je, WAZIRI na TANROADS ni vitu viwili tofauti?
2. Raia wanabomolewa nyumaba zao ili kupisha nini? Barabara hiyo kwa mujibu wa bajeti ya wizara HAIPO kwa sasa. LABDA BAADA YA MIAKA 3+
3. Raia aliyeishi kwenye makazi yake kwa zaidi ya miaka 70 ukampa notisi ya kuhama kwa muda wa mwezi mmoja itakuwa haki?
4. Hiyo demolition order wanasema imetoka JUU KWA MZEE MAGUFULI, je ni kweli na kwa lengo gani la kuwakandamiza wananchi?
5. Raia hawapingi ujenzi wa barabara na wala hawapingi kubomolewa majengo yao ila muda uliotolewa hautoshi. Hata hivyo barabara haijengwi leo wala kesho.
6. TUNAOMBA VIONGOZI WETU WATOE DIRA KAMILI JUU YA BARABARA HII.
7. KWA VILE SERIKALI YA AWAMU YA TANO NI SIKIVU, TUNAOMBA IWAELEZE RAIA WA KIMARA HATIMA YAO KWA SASA NI IPI.
8. SHOWDOWN: Inasemekana kuna showdown ya makusudi kabisa kati ya baadhi ya viongozi wa TANROADS na baadhi ya raia wa Kimara. Sasa je, serikali inaongoza kwa "Showdown"
NAWASILISHA