Waziri Mkuu ampa siku 3 Mkurugenzi wa Manispaa Ukerewe aeleze amepeleka wapi milioni 350 za miradi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Februari 18, 2018 wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.

Amesema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.


"Namtaka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 mwezi huu waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.”

Waziri Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo.

Pia Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84 zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa ni sh. milioni 60 tu.

“Kama mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa sababu Serikali haiwezi kuvumilia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si vinginevyo.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie utendaji wa viongozi na watumishi katika wilaya zote za mkoa huo na kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella.
Majaliwa_0.jpg


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi.

Amewataka viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.]


Chanzo: EATV
 
Waziri mkuu nilitegemea ungetoa Dakika waziri WA mambo yandani ajihudhuru, mkurugenzi kinondoni awekwendani, Kamanda wa polis kinondoni shusha cheo
 
Hizi kiki hatuzitaki.

Mwigulu, Igp, na kamanda mambosasa wanatakiwa kuachia ngazi kwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo yaliyofanywa na askari.

Hizi kiki hatuzitaki. Kama amefanya ufisadi si apelekwe mahakamani? Unampa siku 3 ili akafukie ushahidi au?

[what trump said about african governments]
 
Mimi namkubali sana Mh waziri mkuu, Mungu aendelee kumsaidia baada ya Magufuli ningependa yeye awe Rais wa JMT kwa awamu ya 6
 
Hizi kiki sijui zitaendelea mpaka lini,
Tuambieni hela zilizokwapuliwa Escrow,Tangold,meremeta,Richmond, zipo wapi?
Huu ni uzushi tu,Hanna kitu hapo,
Maelezo yatakuja tu,kwamba pesa zilipelekwa kujenga,maabara,zimelipa posho za safari,kwisha,

This is just fucking PR stunt,the PM is praying,
Majizi mangapi yameenda jera,na kufilisiwa,

Jambo kubwa mlilofanya ni kumwachia babu seya,kwanini hamfanyi,jambo lenye uzito huo huo kwa mafisadi,
Fisadi akamatwe,afungwe,hela aliyoiba irudi,iperekwe HESLB,vijana wapige shule,sio kuwatwanga risasi wakati mnaiba kura
 
Huyo mkurugenzi kama ana akili yeye amuambie tu Wazir Mkuu hela imetumika kununulia wapinzani wote Ukerewe, kama akifanya hivyo ataongezewa na nyingine kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom