mchonga
JF-Expert Member
- Dec 3, 2006
- 1,233
- 248
Sijui ni mimi tu, naona kama attachment hazijakaa sawia! Aliyeziona vizuri naomba azipost tena jamani.
Haya hii hapa.
UKWELI WA KILICHOTOKEA TAREEHE 17-12-2010 KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ARUSHA
Hakika, damu za waliopoteza maisha katika kutafuta haki Arusha tarehe 5-01-2011 zitawalilia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa - - Aruasha, na wasimamizi wa kikao cha tarehe 17/12/2010 kutoka TAMISEMI Dar es Salaam.
􀂾 Baada tu ya Madiwani wa Chadema kupokea taarifa ya Mkutano maalum wa baraza la madiwa la halmashauri ya manispaa wa tarehe 17/12/2010, pamoja na agenda na ratiba, walibaini kuwa agenda haikuwa na kiapo cha madiwani, bali ratiba ilikuwa na agenda hiyo kama shughuli ya 3 ya siku hiyo.
􀂾 Kanuni za kudumu za mikutano na shughuli za halmashauri, Sura ya 6(VI), Kanuni Na 67, inaainisha wazi kuwa kila diwani, kabla ya kushika wadhifa wake kama diwani na kabla ya Mkutano wa kwanza wa halmashauri, atakula kiapo.
􀂾 Ratiba pia ilionyesha kuwa Shughuli na.6 ya siku hiyo, Uchaguzi wa Meya wa halmashauri ilipangwa kusimamiwa na Mkurugenzi wa manispaa, wakati kanuni na. 10 (1) (b), inatamka wazi kuwa, Kama mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawapo, mmoja kati ya wajumbe wa mkutano atateuliwa kuendesha mkutano
􀂾 Mkurugenzi anatakiwa kuwa KATIBU wa vikao VYOTE vya baraza kikiwapo kikao cha kwanza, (Kifungu Na. 24(8) cha sheria za serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji Na.8 ya mwaka 1982, pamoja na marekebisho).
TAREHE 17/12/2010:
􀂾 Madiwani wa Chadema walifika Manispaa saa 3.45 asubuhi na kwa mshangao kukuta askari wengi wakiwa wametanda eneo lote la halmashauri, bila kujua mipango ya mkurugenzi. Waliingia ukumbini na kukuta wenzao wa CCM wameshabana upande mmoja wa ukumbi na kuacha wazi upande mmoja, kaubaguzi ka kiaina fulani.
􀂾 Tarehe 16/12/2010, mkurugenzi alikodi gari la matangazo kupita katika mitaa yote ya manispaa ya Arusha, kuwatangazia wananchi kuja kushuhudia madiwani wakiapa na kumchagua Meya wao tarehe 17/12/2010. Kinyume chake wananchi waliofika, zikiwamo familia za madiwani hawakuruhusiwa kabisa kukaribia eneo la manispaa na hata vyombo vya habari havikuruhusiwa kama kanuni Na. 12 inavyoagiza. Wananchi waliojaribu kukaribia eneo hilo, walipigwa na hata wengine kupelekwa mahabusu na wameshitakiwa mahakamani hadi leo.
􀂾 Mkurugenzi aliingia saa 4.10 asubuhi, akifuatana na viongozi wa TAMISEMI.
􀂾 Aliwasalimia wajumbe na kuwasisitizia kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kikao cha siku hiyo, na wakati huo huo akisisitizia wajumbe kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio ili akidi ya mkutano iweze kutimia na mkutano uanze.
NB: Mkurugenzi aliamini kuwa madiwani wa CHADEMA ni wageni na hawajui lolote kuhusu Kanuni za Kudumu za Mikutano na Shughuli za Halmashauri, lakini kwa mshangao vijana wa Chadema walianza kumtajia na kunukuu kanuni hizo kutoka vichwani kuhusu kuapa kwanza kabla ya kutafuta akidi ya mkutano wa kwanza.
Wakaenda mbele zaidi na kumtahadharisha kuhusu ukomo wa uenyekiti wake kuishia kwenye kuapisha madiwani na kumwachia mjumbe mteule kati ya wajumbe waliopo kusimamia uchaguzi wa Meya na kisha Meya atakaye chaguliwa kusimamia uchaguzi wa naibu Meya. Hatua hii ilimshangaza na kuanza kutoka jasho hadi kichwani bila kuelewa lakufanya tena.
Wakati akitafakari aina ya watu walioingia kwenye baraza kipindi hiki, alisimama mjumbe mmoja na kumtahadharisha kuhusu mjumbe HARAMU wa mkutano huo Mary Chatanda kutoka Tanga.
Hapo ndipo hali ya hewa ilipoanza kuchafuka ndani ya ukumbi ule kwa siku hiyo.
Mabishano na kelele zilianza na kuendelea kwa takriban saa nzima hadi kikao kikaahirishwa kwa saa 1, ili watu wakapekue sheria na nyaraka mbalimbali za uthibitisho, na wapate chai katika kipindi hicho.
Vijana wa Chadema waliporudi, walikuwa na nyaraka za kimtandao kuwa Mary Chatanda alichaguliwa na wajumbe kule Tanga, akiwa wa pili kwa kura 490, wa kwanza alikuwa na kura 514 na wa tatu alipata kura 460. Vijana hawa walilithibitishia baraza kuwa, waliomchagua kule Tanga wanamuhitaji akawatumikie, na sio wananchi wa jiji la Arusha.
Meza ilichanganyikiwa baada ya kupata taarifa hizo,na siku iliharibika kabisa.
Walianza kutafuta vielelezo na ushahidi bandia wakumhalalisha mjumbe huyo, bila mafanikio, hadi mkurugenzi alipoamua kuwa basi kama ndivyo. Madiwani waapishwe ili siku isipotee bure.
KIAPO BANDIA:
Baada ya hakimu kufika, Mkurugenzi kwa kofia ya mwenyekiti, alitamka kuwa, kutokana na wingi wa wajumbe wanaotakiwa kuapa, haitawezekana kuapa mmoja mmoja na hivyo kulazimika kuapa kwa pamoja wote. Wajumbe walihoji, kulikoni,wengi wangapi? 30 tu! Licha ya wajumbe kulalamika, Mkurugenzi alisisitiza kuapa kwa pamoja.
Ndipo madiwani wote waliposimama kwa pamoja na kusoma hati za kiapo kwa sauti kama watoto wa shule za awali na kutakiwa kutia saini pale mwisho. Wakati huo, Kitabu cha mahudhurio ya mikutano ya baraza bado hakina sahihi hata moja ya madiwani wa CHADEMA, na hadi leo hakuna sahihi zao.
Je, hati za kiapo za madiwani, ambao wanatakiwa kuapa kabla ya kikao cha kwanza kuitishwa ndizo zinazolazimishwa kutumika kama akidi ya kikao hicho cha kwanza cha tarehe 17/12/2010?!
KULAZIMISHA UCHAGUZI WA MEYA:
Baada ya Mkurugenzi kuona kuwa madiwani wote wameapa na hati husika kusainiwa na kurudishwa kwake, ndipo alipoanza kulazimisha kuendelea na uchaguzi wa meya, hata kufikia kusema wasiotaka kuendelea na uchaguzu watoke nje.
Akaanza kugawa karatasi za uchaguzi. Vijana wa Chadema walimtahadharisha tena kuhusu akidi za mikitano ya uchaguzi, Kanuni Na. 8(2), na kura ya siri, Kanuni Na.9(1), kwamba akidi haikutimia na mazingira ya kura ya siri hayakuwepo.
Licha ya tahadhari hizo, alingangania kuendelea na ndipo vijana wote wa Chadema waliposima na kujaa katikati ya ukumbi kupinga hatua hiyo Polisi, wakiongozwa na OCD waliingia ndani ya ukumbi wakitaka kuingilia kati kabla yakutahadharishwa na mjumbe mmoja na kutakiwa watoke nje.
KUAHIRISHA KIKAO
Baada ya hali ya sintofahamu kuendelea kwa muda, mjumbe mmoja alimkumbusha Mkurugenzi kurejea kwenye Kanuni Na. 17(2), ili kuahirisha kikao hicho na akafanya hivyo.
RATIBA YA TAREHE 18/12/2010:
Kutokana na Kikao cha tarehe 17/12/2010 kuisha katika hali ya kutoelewana, madiwani wa chadema walijua kikao hicho kingeendelea siku nyingine na kwa taarifa mpya.
Ratiba ya awali ilionyesha kuwa Jumamosi tarehe 18/12/2010 na Jumatatu tarehe 20/12/2010, madiwani walikuwa wawe kwenye semina elekezi kule Olasiti Garden, na ndiko walikoelekea siku iliyofuata.
Kumbe wenzao wa CCM, baada ya kikao cha tar.17/12/2010 kuahirishwa, walikutana na kusubiri taarifa mpya za kikao cha Jumamosi tarehe 18/12/2010, wakati barua 14 za taarifa za kikao hicho za vijana wa CHADEMA, zilipelekwa na kuachwa kwenye baa moja huko suye na kuachiwa mhudumu kwa maelekezo kuwa akitokea yeyote kati yao akabidhiwe. Barua hizo zilipatikana Jumatatu tarehe 20/12/2010 saa 8 mchana.
Chakushangaza, tarehe 18/12/2010, wakati madiwani wa Chadema wakiwa kule Olasiti Garden, wenzao wa CCM, kwa taarifa walizosambaziana usiku wa tarehe 17/12/2010, waliingia manispaa na kuanza na agenda ya kwanza kwa haraka haraka ya uchaguzi wa Meya, kana kwamba kulikuwa na dharura. Hadi madiwani wa Chadema wanapata taarifa kuwa, wenzao wako Manispaa, Meya na Naibu Meya walishachaguliwa.
Walipokimbia kutoka Olasiti Garden hadi Manispaa wakakuta mambo yamefanyika ndivyo sivyo, ndipo walipoanza kuhoji taratibu zilizotumika na hapo vurugu zikaanza hadi Mbunge wetu kupigwa na kuwekwa mahabusu.
Siku hiyo polisi walikuwa wengi kuliko jana yake, na walitawanyika eneo lote la mita 200 kutoka lango kuu la halmashauri, na walikuwa katika mazingira ya UTAYARI kwa mapambano yoyote. Mazingira kwa vyovyote vile, yaliashiria kufanyika uhalifu fulani kwa nguvu.
TUNASISITIZA KUWA:
􀂙 Muda wa taarifa ya mkutano wa tarehe 18/12/2010 haukufuata kanuni (Na. 7).
􀂙 Baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa tareh 17/12/2010, mkutano wa tareh 18/12/2010 ulikuwa unajitegemea na ulihitaji maandalizi mapya kama zilivyofanyika kwenye halmashauri nyingine nchini.
􀂙 Akidi kwenye mkutano wa tarehe 18/12/2010 haikutimia na hivyo kuufanya mkutano huo kuwa batili.
􀂙 Mary Chatanda alikuwa mjumbe batili wa mkutano huo wa uchaguzi na anaendelea kuwa batili.
VIAMBATANISHO:
Pamoja na barua hii, tunaambatanisha:
Nakala za barua, agenda na ratiba za shughuli za tarehe 17/12/2010 hadi 20/12/2010,
Nakala ya taarifa ya mkutano wa tarehe 18/12/2010 zilizokuwa zimeachwa baa huko Suye na kupatikana tarehe 20/12/2010