Waziri Mkuu amelidanganya bunge na watanzania wote

Tatizo ni moral corruption iliyojengeka ndani yetu kiasi kwamba sasa tunaamini kwamba kusema uongo ni sawa tu, na mtu akisema uongo wala hajisikii kwamba hilo ni tatizo. Viongozi wanasema uongo wa wazi bila hata kigugumizi! Tutaponaje kweli kama uongo ndo umekuwa "norm" ya mawasiliano kwenye jamii ?????
Solution ni kutafuta dawa ya kutibu hiyo moral corruption.
 
Asanteni sana wadau kwa michango yenu! Kuna wengine hatukuwa karibu na kilichojiri bungeni hi leo asubuhi, ili mjadala unoge, ni vizuri aliye na taarifa in bulets, alicho sema PM. Asante Josephine kwa taarifa nzuri ya upande wa pili wa shilingi
 
Nadhani serikali inatakiwa kujua kwamba haiwezekani tena kutoa majibu ya kisanii bungeni wakati unaulizwa maswali yenye maslahi kwa wananchi halafu wananchi wakakaa kimya. Kwamba wananchi wana nafasi ya kutoa maoni yao na kuweka ukweli sawa.

Naomba Godibulesi aweke ushahidi sawa kisha tumtake Pinda ajiuzulu. Tusiendelee kuvumilia uongo wa serikali tafadhali, na hii ianze na waziri mkuu
 
Tatizo si Lema kuleta ushahidi, tatizo ni je haki itatendeka? Inavyoonekana mpaka sasa ni kwamba Lema hana adabu, hata huo ushahidi wake hauwezi kukubalika maana kumuumbua PM si rahisi na jambo ambalo silitegemei kutoka katika Bunge hili. Ajiandae tu kwa adhabu atakayopewa huo ndo ukweli wenyewe
 
Hata malaika akiingia CCM hawezi akatoka msafi atachafuka tu.Pinda ulianza vema sasa UMEPINDA:sick: baba.
Hata shetani anawashangaa dhambi nyingine hakuwatuma,mnamshinda umahiri hata shetani HATARI:roll:
 
Tatizo si Lema kuleta ushahidi, tatizo ni je haki itatendeka? Inavyoonekana mpaka sasa ni kwamba Lema hana adabu, hata huo ushahidi wake hauwezi kukubalika maana kumuumbua PM si rahisi na jambo ambalo silitegemei kutoka katika Bunge hili. Ajiandae tu kwa adhabu atakayopewa huo ndo ukweli wenyewe

Ikiwa atadhibiwa kwa kuzuiwa kuhudhuria vikao vya bunge itasomeka kuvunjwa katiba, haki ya wananchi kuwakilishwa itakuwa imeporwa,
Nashauri ikitokea tufungue kesi ya kikatiba ya kuwanyima wananchi haki yao ya kuwakilishwa,
 
Josephine, you have done better to post this topic: well-well-done.
Kwa kifupi ni kwamba CCM wanamtumia Pinda kama chambo, kwamba kila atakacho kuwa anazungumza mbele ya jamii basi jamii nzima itaamini kuwa ni sahii kwa kuzingatia kwamba ktk Bunge lililopita kila alipokuwa akisimama kuongea alikuwa anajitahidi kutoa maelezo manyoofu na yaliyo jaa busara na hekima na watu wengi walimsifu na kwa vile alikuwa anajiita ni mtoto wa mkulima basi apo aliweza kuiteka jamii, na wengi walizani kuwa atakuwa mkombozi wa nchi kumbe ktk kipindi hicho alikuwa anaipalilia njia CCM kwa ajiri ya awamu nyingine.
Watanzania kwakweli hatupaswi kudanganyika tena,, Pinda inavyoonekana analetewa taarifa zingine ambazo si kamilifu nayeye kwa vile anapendwa walau tofauti na wengine hao mafisadi anazitwanga hivyohivyo akijua kuwa hakuna anayejua ukweli wake: kwa taarifa tu ''wenye machungu na nchi kila siku tunafanya utafiti juu ya taifa letu na DATA za msingi tunazo. Hivyo hili la Arusha kwakweli ata na mimi nimeshangaa nilichokisika leo na tukio zima lilivyokuwa ktk harakati za kumpta Meya wa AR. Watanzania tusichoke kupambana-ukweli utaendelea kuonekana na hatimaye Nchi itaingia mikononi mwa wa kweli.
 
Jamani hebu mwenye habari kamili juu ya alichoongea Pinda atujuze kwa uwazi,na nini alisema Lema hata spika kuingilia.
 
Time will always determine,pinda umepoteza uhalali wa kuwa pm,na hakika hutaepuka kikombe hiki
Msisahau Pinda ni miongoni mwa wabunge wa sisiemi 19 ambao ni wabunge batili!!!!!!!!!! Si jambo la kushangaza kusikia maneno ya namna hiyo kutoka kwa Pinda! Wameamua na wamedhamiria kweli kweli kuendesha nchi hii kwa uwongo mkubwa wa madai ya "UTAWALA WA SHERIA" kwenye mgongo wa utawala wa "UGAIDI" tangu mbinu zilizotumika wakati wa uchaguzi mkuu, tukio la Arusha, na sasa haya matukio ya uporaji hadharani kwa nguvu wa haki za kikatiba za CDM kuchanganya na madai ya uongo wa mchana kweupe!!!!!!!! Mbona hakutaja yule mbunge wa sisiemu Arusha kwamba si mbunge wa jimbo mojawapo au kiti kwa ajili ya mkoa wa Arusha????? -mbunge halali wa CDM akawekwa pembeni na mbunge batili wa sisiemu akahesabiwa haki katika baraza la madiwani Arusha; Hii ni sawa sawa na mbinu walizotumia katika uchaguzi wa rais-Kikwete 27% ndiye rais, na Slaa 64% ni wa pili!!!!!!!!!; Hata katiba mpya nayo itakuwa hivyo hivyo!!!!!!!!; yaani matakwa ya mafisadi ndiyo yatakuwa dira ya katiba hiyo!!!!!!; It is very big shame maana kwenye vyombo vya kimataifa wanajitangaza kwamba ni watawala bora na safi wa kuigwa na nchi zingine za Afrika!!!!!!!!!! VERY BIG SHAME!!!!!!!!!!!!!!!!
Siku zote vitendo vya kudhulumu walio wengi Mungu huingilia kati- na katika hili mwisho hauko mbali!!!!!!!!!! Sasa inaanza kudhihirika sisiemu ni chama cha magaidi na mafisadi. Ndiyo maana sisiemu/serikali yake na RA &Co ni kama chapati na kikaango!!!!!!!!!
Sisi ambao matukio haya yanatuumiza roho tunawaambia CDM kuwa Mungu ameonyesha njia kwa mifano ya Tunisia, Misri na Yemen!!!!!!!!!! Mbinu za uungwana hapa hazitaleta matunda yo yote; majambazi huwezi kuwakabili kidiplomasia hata siku moja!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Magaidi ni majambazi!!!!!!!!!!!!!!! Dawa ni PIPOOOOOOOOOOOZ PAWA!!!!!!!!!! tu ndiyo njia pekee iliyosalia!!!!!!!!!!
 
Tatizo si Lema kuleta ushahidi, tatizo ni je haki itatendeka? Inavyoonekana mpaka sasa ni kwamba Lema hana adabu, hata huo ushahidi wake hauwezi kukubalika maana kumuumbua PM si rahisi na jambo ambalo silitegemei kutoka katika Bunge hili. Ajiandae tu kwa adhabu atakayopewa huo ndo ukweli wenyewe

Nakubaliana na wewe na hasa kwa wito wa kumwomba Lema ajiandae na Adhabu. Mimi nyongeza yangu napenda kumfariji Lema atayarishe ushahidi wake kama ukweli ulivyo ATAKUWA AMEFIKISHA UJUMBE hata akiadhibiwa.

Pili wabunge wote wa CDM wampige taf hata kulikomalia bunge ikibidi basi waadhibiwe wote.
 
Pinda is making lame excuses in desparate attempt to save his ass and make his govt look good. Mheshimiwa you can not save your ass. In short your days and your party's days are numbered! Tumechoshwa na machozi yako ya kinafki.
 
Nakubaliana na wewe na hasa kwa wito wa kumwomba Lema ajiandae na Adhabu. Mimi nyongeza yangu napenda kumfariji Lema atayarishe ushahidi wake kama ukweli ulivyo ATAKUWA AMEFIKISHA UJUMBE hata akiadhibiwa.

Pili wabunge wote wa CDM wampige taf hata kulikomalia bunge ikibidi basi waadhibiwe wote.
Waambieni CDM watambue wanadeal na majambazi na mafisadi wa kimataifa-njia za kidiplomasia na kijetumen hapa itazidi tu kutuletea uchungu!!!!!!!!!!!!!! Wajenge hoja za kuamsha hisia za wananchi wanaoumia kama vile wanavyuo, machinga, wale asilimia 88% walimaliza form four ambao wasitarajie mema yo yote katika maisha yao chini ya utawala wa serikali ya sisiemu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
...Mi nnasubilia kuona ni jinsi gani suala hili litakavyopindishwapindishwa na kuishia hewani!....
 
kuna mtu aliwahi kuuliza kwamba, Mbona wakati Chadema wanaandamana kwenda kuzika hayakutokea maafa yoyote???? nami pia narudia kukuuliza swali hilo hilo mkuu??:twitch:

Waziri anatamka uwongo wakusema watu wamepigwa risasi 50m karibu na kituo,hakupewa taarifa kuwa risasi zilipigwa uwanjani kabla ya mkutano,maneno makali yaliyotolewa katika mkutano ni baada ya risasi na wananchi ni mashahidi.
 
Ngoma inogile sasa, yaani kimewaka, hata kama wabunge wa CCM, wakikataa ushahidi wa LEMA , kudhibitisha kuwa kasema PINDA, kasema uongo, sisi wananchi ukweli TUNAUJUAA, ambao ndio wapiga kura wa 2015
 
Ahsante sana mama, hizi habari ni vizuri zikiwafikia pia wananchi wasio na nafasi ya kusoma huku ili wafahamu hali halisi nini kilitokea.
 
Pole invisible firstlady of my invisible president. Pinda kasema uongo! Ameleta ushaidi kuwa chanzo cha vurugu ni kuongeza route za waandamanaji wakati hawezi kudhibitisha kuwa waliopigwa risasi ni wale tu waliotokea njia/route iliyokataliwa! Pia mhusika kwa mamlaka ya polisi yani mwema alitueleza kuwa intelligentia ilisema kuwa kutatokea uvunjaji wa amani,sasa je alienza kumpiga mwenzie ni nani raia au polisi?vyombo vya habari vilivyokuwa laivu vilionesha,pia kama mahakama haijahitimisha kesi,anayehitimisha anakuwa ni muongo na hana mamlaka ya kuiaminisha jamii kuwa yeye kama serikali alikuwa sahihi kuua. Pole mama mh. kwa yaliyokukuta pale Arusha,damu na chozi lako litalipwa na Mungu. Mwisho,naomba nimalize dinner ndo nije kuchangia kwa nini Lema ahoji zaidi,je yeye amesema kuwa PM kalidanganya bunge au ameomba mwongozo la kufanya endapo itadhibitika kuwa PM kasema uongo? Ikumbukwe anayeweza kudhibitisha nani muongo ni maamuzi ya mahakama ya tarehe 21/02/2011 kama ushaidi utakuwa umekamilika . Hivyo Lema hajasema pinda muongo kaomba aelekezwe ili pindi bunge likigundua kuwa Pinda muongo afanyeje! Pia mtu akiomba mwongozo,anapewa mwongozo. Maana ya mwongozo ni maelezo ya ziada. Mtu hawezi kuomba mwongozo,akapewa adhabu ya kuleta muongozo wa mbunge,hii ni dhana ya udikteta. Pia hapa kuna opportunity ya kulikabidhi bunge cd ya Arusha ambayo haijahaririwa!
 
Naweza kuongea hili kwa ujasiri wote kwasababu siku matukio yanatokea nilikuwa nafuatilia kwa kwa ukaribu sana.

Watanzania imefika wakati tuondoe uwoga na kutetea masilahi ya watu na si vinginevyo,Hali hii inauma sana na inasikitisha .


  1. Jambo la kwanza waziri amedanganya ama kwa kupokea taarifa za uwongo ni juu ya ratiba iliyokuwapo na taarifa zilizotolewa.
  2. Pili juu ya wabunge wa chadema kuingia na kutoka,Huu ni uwongo uliopitiliza.

  • Taarifa ya kwanza Kikao kilihairishwa bila kujulikana nini kitafuatwa kesho yake,kwani kulingana na ratiba the day next ilikuwa ya semina kwa wabunge wote.Copy attached.
View attachment 22569

  • wabunge waliachana bila kupeana taratibu sababu kikao kilivunjwa gafla.Lakini kilichofuata ni muendelezo wa ratiba ya what follows the next day.
  • Barua ya kuwarudisha kwenye mkutano barua ziligawiwa kwa wabunge wa CCM na TLP tu.Copy attached above.

Naongea haya kwa ujasili kwasababu nililifatilia na kuongea na RPC kwa kinywa changu mwenyewe.

watanzania na wanaJF ambao mnaendeleza kufanya ushabiki wakati Viongozi wakubwa wa nchi wanapotosha ukweli nijambo la kusikitisha.Najua wengine mmetumwa/ama ni wahusika naomba niseme tu the day is coming ukweli utabaki kuwa ukweli kwa Mungu anasikia,anaona na mwisho atatenda.

Jamani Waziri anapotosha hata ukweli wa vifo vya wahanga? Nooooooooooooooooo Pinda you have gone beyond,i was among the VICTIM,sikuhadithiwa na mtu.Maneno ya kinywa chako yatakuhukumu.

Marehemu wote waliokufa hawakuwa sehemu ya maandamano yetu.

Waziri mkuu nilitegemea angeomba msamaha ninaushahidi wa watu waliokufa mbele ya macho yangu na taarifa zao sijui ziko wapi.

kwanini nimeguswa na kulileta hapa,ni kwa sababu ya watu walioamua kuleta Tred ambazo zinapotosha umma nakufanya CHADEMA kuonekana ni watu wa haina flani,Lakini ukweli utabaki palepale na mwisho wa siku dhamira zetu zote zitakuwa wazi na Mungu ndipo atakapotoa hukumu yake.Kumbukeni hata wahathirika wanasoma maoni yenu.

Nawapongeza Viongozi wangu wa Chadema wametumia Hekima kubwa kuepusha shari kwa ukimya wao.

MALIPO NA HUKUMU ZA MUNGU HUWA NI HAPAHAPA DUNIANI.

View attachment 22572

Thanks Josephine!
 
Back
Top Bottom