Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,034
- 6,891
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema maendeleo ya kweli ya Taifa yanategemea kujenga wananchi wenye maadili, uzalendo, uwajibikaji na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha utawala wa sheria na taasisi za umma.
"Hakuna maendeleo ya kudumu bila kujenga watu wenye maadili, uzalendo na uwajibikaji. Kama Taifa tuna kila sababu ya kuendelea kuwekeza katika kujenga tabia ya wananchi pamoja na kuimarisha taasisi zetu," amesema.
Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumatatu, Julai 20, 2026) alipokutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Soma Pia: Dkt Mwigulu Nchemba: Ukitaka Siasa Anzisha Chama Chako Usipeleke Siasa Makanisani Kuvuruga Kanisa na kuleta Fujo
Katika mazungumzo hayo, Mzee Butiku alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake na juhudi anazoendelea kuzifanya katika kuiongoza nchi. Pia, alimpongeza Waziri Mkuu kwa mchango wake katika kumsaidia Mheshimiwa Rais kusimamia Serikali na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali unaendelea kwa ufanisi. Amesema amekuwa akifuatilia kwa ukaribu ziara za Waziri Mkuu mikoani na kujionea namna zilivyochangia kutatua changamoto za wananchi na kuimarisha utoaji wa huduma.