Waziri Mkuu aitisha kikao cha Mawaziri

Waziri Mkuu aitisha kikao cha Mawaziri

Naona serikali ya awamu ya tano imeanza usanii wa kufanyia kazi kwenye media

Na huku uswazi mgao wa umeme umekuwa mkali zaidi. No new thinking
 
Sijui ni kwanini mantiki rahisi tu inatushinda! Well, Nyerere alikuwa PM na Mkuu wa nchi alikuwa nani?

Gavana mwakilishi wa malkia wa UK ndie alikuwa mkuu wa nchi huku nyerere akiwa PM mwaka 1961, baadaye tukawa jamhuri mwaka 1962 na nyerere akawa rais, kawawa PM.
 
Nyerere hakuwahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania, Nyerere alikuwa ni waziri mkuu wa Tanganyika tena kipindi ambacho Tanganyika haikuwa na rais hivyo Waziri mkuu ndio ilikuwa Post ya juu kabisa kisiasa.

Kwa kifupi kabisa, Hakuna waziri mkuu wa Tanzania ambaye alifanikiwa kuja kuwa rais wa Tanzania.

Kiongozi umejibu vyema sana sana.
 
Kwani hizi taarfa humu jamii forum kaleta waziri mkuu au watu wengine na mihemko yao,kwahyo media zisiruhisiwe kwenye matukio ya serikali sio,wakizuiwa mtasema wanaonewa,so whaaat!@
 
Gavana mwakilishi wa malkia wa UK ndie alikuwa mkuu wa nchi huku nyerere akiwa PM mwaka 1961, baadaye tukawa jamhuri mwaka 1962 na nyerere akawa rais, kawawa PM.

Usituchanganye! Mwaka 1960 Tanganyika ilipopewa mamlaka ya ndani hadi muda mfupi kabla ya Uhuru (9-12-1961) Nyerere alikuwa na title ya "Chief Minister - CM" na sio PM. Mara baada ya Uhuru akawa PM na mwaka uliofuata akawa Rais. Kipindi unachozungumza wewe cha Gavana kuwa Mkuu wa Nchi ni kipindi Nyerere akiwa CM na sio PM.
 
Baraza la Mawaziri kwa maana ya cabinet!? Manaibu hawaingii, huu uitwe mkutano wa Waziri Mkuu na Mawaziri namanaibu mawaziri.
 
Safari zimebaki za mikoani kufuatilia mambo ya maendeleo...linalowezekana leo lisingoje kesho. Tuijenge nchi yetu sasa...enough is enough
 
Usituchanganye! Mwaka 1960 Tanganyika ilipopewa mamlaka ya ndani hadi muda mfupi kabla ya Uhuru (9-12-1961) Nyerere alikuwa na title ya "Chief Minister - CM" na sio PM. Mara baada ya Uhuru akawa PM na mwaka uliofuata akawa Rais. Kipindi unachozungumza wewe cha Gavana kuwa Mkuu wa Nchi ni kipindi Nyerere akiwa CM na sio PM.

Ila huwezi kupingana na ukweli kuwa Nyerere hajawahi kuwa Pm wa Tanzania bali Tanganyika. Hivyo ni sahihi kuwa haijawahitokea Pm wa Tanzania kuwa Rais
 
Ila huwezi kupingana na ukweli kuwa Nyerere hajawahi kuwa Pm wa Tanzania bali Tanganyika. Hivyo ni sahihi kuwa haijawahitokea Pm wa Tanzania kuwa Rais

Hoja ya msingi hapa ni ukuu wa nchi; yaani mamlaka ya mwisho katika nchi. Kwa titles zote mbili PM na Rais, Nyerere alikuwa Mkuu wa Nchi iwe Tanganyika au Tanzania. Kinachogomba hapa ni mtu kutoka uPM kuwa Rais na wanatoa mfano wa Nyerere wakati Nyerere akiwa PM alikuwa Mkuu wa Nchi na akiwa Rais alikuwa Mkuu wa Nchi.

Pengine hoja ingeeleweka na wenye akili ndogo kama ingesomeka "hakuna aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kisha akawa Mkuu wa Nchi"; asiyeelewa tena atakuwa na matatizo.
 
Back
Top Bottom