March 21, 2020
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ameonya juu ya upotoshwaji na utoaji holela wa taarifa kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababisha na virusi vya corona (COVID 19) unaofanywa na watu mbalimbali nchini.
Amesema kuanzia sasa taarifa hizo zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ikilazimika zitatolewa na Waziri Mkuu na ikilazimika sana zitatolewa na viongozi wakuu wa nchi ili kuepusha mikanganyiko.
Aidha Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ifuatilie watu wote wanaofanya upotoshaji kwa kupitia mitandao ya kijamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“Watu wote wanaopotosha umma na kuleta taharuki kuhusu ugonjwa wa corona badala ya kuelimisha namna ya kujikinga, wafuatiliwe na kuchukuliwa hatua,” amesisitiza.
Source: Azam TV
More info :
Baada ya mkanganyiko wa utoaji taarifa kuhusu gonjwa la SARS -:Covid - 19 coronavirus na tamko la waziri kivuli wa Afya kuhusu mkanganyiko huo.
Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa utaratibu mpya ya namna ya kutangaza uwepo wa coronavirus kuwa utaratibiwa moja kwa moja na wizara ya Afya na si vinginevyo.
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa anaongeza kuwa serikali imeamua kuweka utaratibu huu ili kuondoa hali ilivyo sasa ambapo taarifa zinarushwa na vyanzo vingi na kuleta mtafaruku na hofu bila uthibitisho wa wataalamu wa maabara kuu iliyo chini ya Wizara ya Afya.
Waziri Mkuu amesema kunapogundulika uwepo wa coronavirus ktk eneo lolote baada ya uthibitisho kwa vipimo, taarifa hizo kupitia waganga wakuu wa mikoa kwa kushirikiana na kamati zao za ulinzi za mikoa zilizo chini wa wakuu wa Mikoa / Wilaya, zipelekwe moja kwa moja Mganga Mkuu wa Serikali wa wizara ya Afya na waziri wa Afya wizara hiyo ndiyo amekasimiwa rasmi kazi ya kutangaza uwepo wa coronavirus.
MAJALIWA - Wapotosha kuhusu Corona kukiona
Published on 21 Mar 2020