Waziri Mkuu Majaliwa Kassim ameagiza Daktari wa Kituo cha Afya Mahuta Mtwara akamatwe, ni baada ya Wananchi kudai anahusika na wizi wa dawa kunakosababisha Wagonjwa kukosa dawa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo baada ya Wananchi kusimamisha msafara wake [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG]
Je alichofanya waziri mkuu ni sahihi? Je kama wananachi hawakuwa sahihi si atakuwa kamfedhehesha huyo daktari?

Ni aina mbovu kabisa ya uongozi. Ushahidi wa kuiba dawa anao au hao wananchi wanao?wananchi wanajuaga serikali yao ina mapesa mengi na huwa inamwaga tu madawa hospitalini. mbaya zaidi Kasimu anajua serikali huwa haipeleki pesa ya kutosha kwaajili ya dawa lakini ili afurahishe wananchi kaamua kumtia ndani jamaa.
Ni umbumbumbu wa waandishi wetu mkuu,wa kutokujua protokali za hawa viongozi wa juu.Kila kitu atachofanya Rais/waziri mkuu huwa kipo kwenye Ratiba ya ziara.Yaani watu mtoke tu huko mkusanyike kuzuia msafara?Je kama kati yenu kuna wauaji?Nimewahi kuona msafara wa waziri mkuu. Najiuliza kwa kasi yote ile ikitanguliwa na FFU, RPC,OCD wanazuiaje msafara?
Ni umbumbumbu wa waandishi wetu mkuu,wa kutokujua protokali za hawa viongozi wa juu.Kila kitu atachofanya Rais/waziri mkuu huwa kipo kwenye Ratiba ya ziara.Yaani watu mtoke tu huko mkusanyike kuzuia msafara?Je kama kati yenu kuna wauaji?
Wizi wa dawa na waganga wa Zahanati mkuu ni janga la taifa,kama lilivyo tatizo la matumizi mabaya ya fedha za Halimashauri na Wakurugenzi wa Wilaya.Naamini wananchi hawakukurupuka.Akamatwe tu.Waziri Mkuu Majaliwa Kassim ameagiza Daktari wa Kituo cha Afya Mahuta Mtwara akamatwe, ni baada ya Wananchi kudai anahusika na wizi wa dawa kunakosababisha Wagonjwa kukosa dawa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo baada ya Wananchi kusimamisha msafara wake [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG]
Je alichofanya waziri mkuu ni sahihi? Je kama wananachi hawakuwa sahihi si atakuwa kamfedhehesha huyo daktari?
Ukizikia eti msafara wa kiongozi umezuiliwa ujue hayo ni maigizo tuHakuna kitu kinachoitwa 'kuzuia msafara'.