Waziri Masauni aagiza uchunguzi maiti zilizookotwa kwenye viroba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamadi Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na mauaji ya watu wawili na kuwatupa wakiwa kwenye viroba.

Maiti hizo ziliokotwa Agosti 11, 2022 zikiwa kwenye viroba katika kata ya Tunguli wilayani Kilindi mkoani Tanga na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi.

Masauni ametoa agizo hilo leo Jumatano Agosti 17, 2022 baada ya kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi mkoani Tanga ilipohifadhiwa miili hiyo.

Waziri huyo amesema amesikitishwa na tukio hilo la mauaji lililotokea Wilayani humo na kuagiza Jeshi hilo lishirikiane na vyombo vingine vya usalama kuendeleza uchunguzi ili kuwakamata waliofanya mauaji hayo.

"Tukio hili ni la kinyama dhidi ya raia wenzetu wa Kitanzania, jambo hili halikubaliki kwa namna yoyote ile na sio utamaduni wetu. Kama Serikali tumelichukulia kwa uzito unaostahili na tutafanya kila linalowezekana ili vyombo vyetu vya usalama vinawabaini na kuwakamata wahusika," amesema Waziri huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amesema watu waliofanya tukio hilo linaonyesha ni wazoefu sababu namna walivyo wakunja kwenye kiroba cha kilo 50 lakini utazani nikilo 20.

Mgumba amesema kuwa dalili za awali zinaonyesha kuwa mauaji hayo hayajafanyika mkoa wa Tanga bali sehemu nyingine na kupeleka kutupa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Sofia Jongo amesema tayari Jeshi la Polisi nchini limeshaunda kamati kwaajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya, Abel Busalama amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa wanapokuwa na mashaka na kitu chochote katika maeneo yao.

Mbunge wa Kilindi (CCM) Omari Kigua amesema tukio hilo linaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuwekeza huku akiliomba Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliotekeleza tukio hilo la kinyama.

Chanzo: Mwananchi
 
Toka January ni blaah blaah tu, sijui kamati, lkn hakuna feedback wamewahi toa.

Vipi na hivi Viroba tumlaumu Dr John Magufuli ?

dhambi ya kumnanga yule Mzee haitowaacha salama wanafiki

sasa hivi wakosoaji wa Serikali hawasikiki kabisa japo uhuru umerudi

Magazeti yote, wanaharakati wote,wanasiasa wote wapo kwny foleni ya kuelekea kwny kibuyu…unahisi ukipiga kelele utachomolewa kwny folen
 
🥶🥶🥶
 
Waziri Masauni aagiza uchunguzi maiti zilizookotwa kwenye viroba

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamadi Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na mauaji ya watu wawili na kuwatupa wakiwa kwenye viroba.

Maiti hizo ziliokotwa Agosti 11, 2022 zikiwa kwenye viroba katika kata ya Tunguli wilayani Kilindi mkoani Tanga na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi.

Masauni ametoa agizo hilo leo Jumatano Agosti 17, 2022 baada ya kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali Teule ya Wilayani Kilindi mkoani Tanga ilipohifadhiwa miili hiyo.

Waziri huyo amesema amesikitishwa na tukio hilo la mauaji lililotokea Wilayani humo na kuagiza Jeshi hilo lishirikiane na vyombo vingine vya usalama kuendeleza uchunguzi ili kuwakamata waliofanya mauaji hayo.

"Tukio hili ni la kinyama dhidi ya raia wenzetu wa Kitanzania, jambo hili halikubaliki kwa namna yoyote ile na sio utamaduni wetu. Kama Serikali tumelichukulia kwa uzito unaostahili na tutafanya kila linalowezekana ili vyombo vyetu vya usalama vinawabaini na kuwakamata wahusika," amesema Waziri huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amesema watu waliofanya tukio hilo linaonyesha ni wazoefu sababu namna walivyo wakunja kwenye kiroba cha kilo 50 lakini ni kama kilo 20.

Mgumba amesema kuwa dalili za awali zinaonyesha kuwa mauaji hayo hayajafanyika mkoa wa Tanga bali sehemu nyingine na kupeleka kutupa katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Sofia Jongo amesema tayari Jeshi la Polisi nchini limeshaunda kamati kwaajili ya uchunguzi wa tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya, Abel Busalama amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa wanapokuwa na mashaka na kitu chochote katika maeneo yao.

Mbunge wa Kilindi (CCM) Omari Kigua amesema tukio hilo linaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuwekeza huku akiliomba Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliotekeleza tukio hilo la kinyama.
 
Nadhani ni wahamiaji haramu wanaokufa wakielekea South Africa,wakifa huwa wanazikwa wapi na nani huwa anawazika?Option ni hiyo tu nadhani.
 
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mgumba amesema maiti zilizokutwa zimetupwa wilayani Kilindi yawezekana zimetoka nchi Jirani na siyo Tanga

Mgumba amesema maiti hizo zilifungwa kwa ustadi mkubwa kwenye viroba vya kilo 50 hali inayoonyesha wauwaji ni wazoefu wa matukio
hayo

Watu wote wa Kilindi wameshindwa kuzitambua maiti hizo

Naye waziri wa mambo ya Ndani mh Masauni amesema wahalifu hai wanatafutwa na jeshi la Polisi kwa nguvu zote

Source ITV habari
 
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mgumba amesema maiti zilizokutwa zimetupwa wilayani Kilindi yawezekana zimetoka nchi Jirani na siyo Tanga

Mgumba amesema maiti hizo zilifungwa kwa ustadi mkubwa kwenye viroba vya kilo 50 hali inayoonyesha wauwaji ni wazoefu wa matukio
hayo

Watu wote wa Kilindi wameshindwa kuzitambua maiti hizo

Maybe waziri wa mambo ya Ndani mh Masauni amesema wahalifu hai wanatafutwa na jeshi la Polisi kwa nguvu zote

Source ITV habari
Ana uhakika kiasi gani kama hizo maiti zimetoka Nchi jirani, na siyo ndani, au nje ya Mkoa wa Tanga?
 
Back
Top Bottom